Search This Blog

Friday, April 13, 2012

SABABU 5 KWANINI BARCELONA ITAENDELEA KUTAWALA ULIMWENGU WA SOKA KWA MIAKA 10 MBELE.

Kikosi cha sasa cha Barcelona bila shaka wala kelele ndio timu yenye  ubora kuliko zote kuwahi kutokea katika soka.

Hii ni imani ambayo imejengeka kwa waandishi na wachambuzi wa habari za michezo,  wacheza soka, makocha na mashabiki wa mchezo huu kwa wingi wakiamini hii ndio timu bora kabisa kuwahi kutokea kwenye soka - labda uwe unaishi jijini Madrid.

Pep Guardiola na kikosi chake wanacheza mpira ambao timu nyingine zinaweza tu kuota kucheza vile.

Miaka 3 iliyopita pale Nou Camp kumekuwepo na mataji 11, yakiwemo back to back la liga, 2 champions league, 2 Uefa Super Cup na 2 FIFA World Club Cup.
Listi itaendelea na kwa hakika inaweza ikaongezeka msimu huu, kwa kuwa bado wapo katika nusu fainali ya Champions league dhidi ya Chelsea huku wakiwafukuza kwa Karibu Madrid katika La Liga.

Lakini je ni lini utawala huu wa Barcelona utaisha? Wengi wamediriki kujiuliza hilo swali huku wengine wakidiriki kusema mwsiho wa Barcelona haupo mbali.

Lakini ukweli ni kwamba hakuna sababu inayoweza kukufanya usiamini kama timu itaendelea kupata nguvu na kutawala soka tena sio kwa mwaka mmoja au miwili - bali ni kwa takribani muongo mmoja.

Hizi ni sababu tano kwanini...........................


 
5 . PEP GUARDIOLA
Timu bora duniani ina kocha bora bora ulimwenguni na hiyo ndio kombinesheni ya kutisha kwa mtu yeyote kuivunja.

Guardiola amekuwa akihusishwa na klabu nyingine especially nchini England, lakini ishara zote zinaonyesha kwamba kocha huyo mwenye miaka 41 atakuwa Catalunya kwa muda mrefu na hiyo ni habari nyingine nzuri kwa mashabiki wa Barca na mbaya kwa wapinzani.

Mhispania huyo anaamini mafanikio yanakuja katika miaka 4 au 5 ya ukocha, akiacha maswali mengi kwamba anaweza kuondoka Catalunya na kuangalia changamoto nyingine sehemu tofauti.

Lakini Bodi ya Bacelona inajua ni mtu wa namna gani wanamhitaji na yupo incharge kwa sasa. Ikiwa Guardiola atakubali kusaini mkatanba mpya , hilo linamaanisha atakaa kwa miaka mingine 6 au 7.

Ikiwa Guardiola ataondoka, hawatokuwa na upungufu wa makocha dizaini ya yake ambao watambadili , akiwemo kocha wa Roma Luis Enrique  na kocha wa Athletic Bilbao Marcelo Biesla ndio watakaoongoza mbio hizo.

4. WACHEZAJI VIJANA WA BARCA
Ushindi wa 4-0 dhdi ya Bate Borisov katika champions league mwishoni mwa December last year ungeweza kuwafanya watu waishtuke, lakini wangepatwa na mshangao mkubwa asubuhi yake watakaposoma kikosi kilichocheza

Guardiola aliwapanga watoto wa Academy katika kikosi cha kwanza, waliokuwa na wastani wa umri wa miaka 20.

Kijana mwenye miaka 19 kiungo mwenye uwezo Sergio Roberto alifungua ukurasa wa magoli, akafuatiwa na Martin Mantoya.

Pia katika kikosi hicho walikuwemo Thiago Alcantara na 18-year old Rafinha.

Lionel Messi na wenzie wengi walikuwa nje wakiangalia namna vijana wakilitandaza soka la kutisha na kupata matokeo mazuri.

 
3. UTAWALA KATIKA SOKO LA UHAMISHO
Hakuna draft katika soka; wachovu hawapati wachezaji wazuri. Wachezaji wazuri wanataka kucheza katika timu bora.

Barcelona wana jina, mafanikio  na fedha za kununua wachezaji wazuri na kwalea wenye umri mdogo katika kuwasaidia kuwa masupastaa wa ukweli na kuifanya timu hiyo kuwa na mlolongo wa wachezaji wazuri, kila anayeingia na anayetoka dimbani wana viwango sawa ndivyo Barca ilivyo.

Mfano, mshambuliaji wa kibrazili Neymar ndio gumzo kwa sasa katika soko la uhamisho duniani na inaonekana magiants wa Catalunya wanaelekea kushinda vita dhidi ya Juventus, Madrid,Juventus na Chelsea katika kumuwania kinda hilo.

Angalia wachezaji wengine kama Jordi Alba na Thiago Silva ambao watakuja kuimarisha zaidi ukuta wa Barca.

Lakini kuongezwa kwa Neymar katika kikopsi cha Barcelona ndio balaa zaidi. Ikiwa atasajiliwa ina maana Fabregas atarudi chini zaidi kuungana na Iniesta na kumpisha dogo mbele na Mchawi Messi.

Kiukweli ukiachana na Ronaldo, jakuna mchezaji mwingine anayetajwa kufananinshwa kiuwezo na Messi kama Neymar- fikiria sasa wakiwa wanacheza timu moja kutakuwa na balaa kiasi gani.


2. BRAND YA BARCELONA
Ingawa kumekuwepo na malalamiko kuhusu dili lao la udhamini na Qatar Foundation, Barcelona bado hawajaitupa UNICEF logo.

Kunaonekana kuna kuongezeka kwa ubora na thamani ya klabu na kuwa timu kubwa na inayotengeneza faida zaidi katika soka duniani.

Pia hivi karibuni wamesaini dili la ushirikiano na Boca Juniors, dili ambalo kwa hakika litawapa faida kubwa ya kuweza kukusanya vipaji kutoka nchini Argentina, huku dili lao la udhamini wa jezi likiwapa uhakika kuwa na fedha za kutumia na kutanua mabavu katika soko la usajili kwa miaka kadhaa ijayo.

Pia wana Academy ambayo ina nguvu, inatengeneza wachezaji bora kabisa duniani, LA masia ni sehemu bora na inatajwa kuwa academy bora duniani kwa sasa kutokana na wachezaji inawotengeneza na waliopo tayari ambao ni masupastaa katika dunia ya soka.

Kwa vitu hivi vyote ni dhahiri future ya Barcelona ipo salama, na vitaongeza na kusaidia utawala mwingine wa Barca katika soka kwa miaka mingi ijayo.


 
1. LIONEL MESSI
Ni jina gani jingine ambalo tunaweza kulitumia kumzungumzia huyu kiumbe ambaye bila shaka ndio mchezaji bora wa soka la kisasa na inawezkana mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea ulimwengu.

Maradona na Pele wanaweza wakabishana juu ya hili, lakini kuna watu wengi wanaamini muargentina huyu ni hatari na hajawahi kutokea kama yeye katika historia ya soka duniani.

Tuzo tatu za mfululizo za dunia zinakamilisha tuzo nyingi ambazo amezifungia nyumbani kwake, ambazo wachezaji wengi duniani wanaota tu kuzipata.

Lakini jambo la kutisha zaidi mchezaji huyu bora wa soka la kisasa ndio kwanza ana miaka 24 tu.

Hilo tu litakufanya uanze kufikiria mara mbili mbili huku likiwaumizavichwa mabeki katika ulimwengu wa soka, kwa sababu  katika zama hizi wapo wengi dizaini yake lakini Messi ni habari nyingine - simply unplayable.

Bado unajiuliza kwanini Barcelona itaendelea kutawala kwa miaka mingine 10 ? Jibu ni kwa sababu mchawi huyu ataendelea kuwepo katika klabu hiyo.

3 comments:

  1. Shaffih kwanini hamsaidii kutoa taaluma na uelewa kuwa Tanzania kama nchi twaweza kujenga mfumo kama huu wa Barca? Siasa kila mahala hakuna professionalissim.Simba yanga tu hakuna lolote la maana kila siku no development. Hivi nyinyi mna tofauti gani na viongozi wetu wa kisiasa wanaosafiri nje kila siku lakini no lessons wanazoleta na kutekeleza khs maendeleo hata yale ya mipango miji zaidi ya kukaa kusifia ya wengine? Najua with this critical components unaweza kuamua kuto pulish my comments lakini jamani sisi tumelaaniwa au? Inaumiza sana!!!

    ReplyDelete
  2. Maendeleo yeyote yanataka kujitoa mhanga na kuwa na watu wavumilivu. Mfumo mpya huja kwa kuuwa wa zamani au kuufanyia adjustments. Turudi kwenye basics kwa kuandaa talents, kuziguide Na kufanya rathimini. Tuwekeze na kuwapa nafasi wenye taaluma kufanya kazi, sio kujuana kwa wingi wa vikombe vya kahawa na kashata za Nazi.

    ReplyDelete
  3. SHAFIHH: UMEHOJI NI KWA NINI PELE ALISEMA HIVYO..???TAFUTA HABARI YENYEWE , AAFU UACHE KUKOPI BROO NI AIBU KUKOPI NA KUBADILI KWA KISWAHILI WE NEED UR IDEA

    ReplyDelete