Search This Blog

Saturday, April 14, 2012

PELE: MTU NAMBA MOJA ANAYECHUKIZWA NA MAFANIKIO YA LIONEL MESSI



Pindi unapokaa na kufikiri - labda mchezaji bora wa muda wote - asingeweza kusema kitu chochote tena cha kumkosea heshima au kumdharaulisha Lionel Messi, lakini ameongea ujinga tena kumuhusu Messiah wa soka wa zama hizi.

Je hii itaisha?

Hivi karibuni katika press conference ya kusherehekea mafanikio ya soka ya Santos , mchawi wa soka maarufu kama Pele amesema tena maneno ya kumshusha Messi kwa kusema hivi:

"Sasa kila mtu anaongea kuhusu Messi, yule ni maarufu. Lakini kwa Messi kuwa ndio mchezaji bora wa muda wote, inabidi lazima kwanza ampite au awe bora kuliko Neymar."

OK, mtu aniambie ni lini Neymar alimpita au kufikia uwezo wa Messi kama mchezaji bora katika dunia? Labda mie sipo katika ulimwengu wa Pele, inawezekana nilipitiwa na usingizi kwa takribani miaka kadhaa nikakosa kushuhudia Neymar akimpita kwanza Wayne Rooney, Cristiano Ronaldo na hatimaye Lionel Messi na kuwa mchezaji bora wa dunia.

Pele pia alisema kwamba hana kinyongo chochote dhidi ya mtu mwingine anayesemwa na watu wengine kama mchezaji bora wa muda , Diego Maradona.

"Nyie waandishi wa habari siku zote mnasema kwamba mmi ni hasimu wa Maradona, lakini sio kweli. Sijawahi kuwa hasimu wake, na yeye alikuwa kiungo mzuri dimbani."

Sijui hata nianzie wapi?

Sitaki kuamini wala kusema kitu ambacho kipo wazi kabisa, lakini hata chizi ambaye anafuatiliwa soka atakuambia Lionel Messi ndio mchezaji bora katika dunia kwa sasa. Huku wengine wakidiriki tayari ni mchezaji bora wa muda wote .

Naelewa Pele anataka kumsifu na kujiletea sifa kwa Neymar. Pele anataka mbrazili awe mchezaji bora duniani, lakini hii sasa inafikia katika pointi ambapo Pele anaanza kupoteza heshima ya mashabiki na maoni yake ya kipambavu na yenye majivuno.

Pele siku zote ataendelea kuheshimika kwa mchezaji wa soka aliyekuwa, lakini anapoteza heshima kwa kutomuheshimu na kumdidimiza Lionel Messi.

Huu uhasama wa Brazil vs Argentina umekuwepo kwa miaka mingi sasa na utaendelea. Kwa hakika mie mwenyewe sitaki uhasama huo upotee. Nani hapendi upinzani wa jadi wa soka la kimataifa - kama vile England vs Germany, Italy vs France au Nertherlands vs Germany?

Lakini kitu ambacho kinaniudhi mimi na mashabiki wengi wa soka, pamoja na kuwa ushabiki tofauti au utaifa , kama mchezaji wa mchezo wowote anastahili kuitwa mchezaji bora, inabidi apewe heshima yake kama mchezaji bora wa mchezo huo. Hakuna kitu chochote kibaya kwenye hilo.

Sasa kwanini Pele asiweke utaifa pembeni na kumtambua pamoja na kumpa heshima yake Messi kama mchezaji bora katika soka hivi sasa?

Pengine wachache kati yenu mnaweza kusema Neymar ni bora kuliko Messi ndio kitu kweli anachoamini. Stop it! Pele anaujua ukweli. Labda Pele ni kipofu - kitu ambacho nina uhakika sio ukweli kwa sababu alisema Messi ni maarufu, hivyo amemuona akicheza soka - sasa ni vipi anaweza kuamini Messi siop mzuri kuliko Neymar?

Sina kinyongo wala tatizo lolote na Neymar; ni mchezaji mwenye kipaji kizuri. Lakini katika kila kitu Leo anachofanya uwanjani - rekodi zote anazozivunja, makombe yote ambayo ameisadia Barcelona kushinda; yote akiyafanya akiwa na miaka 24 tu - ama kwa hakika Messi ndio mchezaji bora wa dunia kwa sasa. Je ni vipi Pele hayaoni haya?

Kinyongo cha Pele kwa Messi kimeanza muda mrefu uliopita. Kumekuwepo na muda ambapo Pele alizungumza maneno ya kumkejeli Messi, pia alipoulizwa anadhani kwamba Messi atakuja kuwa mchezaji bora wa muda wote Pele alijibu, " Kipindi Messi atakapofunga magoli 1,283 kama mimi, pindi atakaposhinda makombe matatu ya dunia, hapo ndipo tutakapoongea."

Muda mwingine, tena Pele alisema kwamba Argentina inahitaji kuamua nani ndio mchezaji bora kutoka nchini kwao - Maradona au Messi kabla ya kuwepo kwa mjadala nani ndio mchezaji bora wa muda wote. Inawezekana alisema hivyo ili kuonyesha dharau kwa Argentina, lakini mimi naona hapa alikuwa anatoa sifa, Arentina imetengeneza wachezaji azuri ambao lazima waingie katika listi ya wachezaji bora wa muda wote.

Kigezo kingine Pele anachokitumia kumkandamiza Pele ni mafanikio katika timu ya taifa.

Messi hahitaji kushinda makombe matatu ya dunia, lakini anahitaji kuiongoza nchini yake kushinda katika mechi kubwa, zaidi labda katika World Cup.

Hivi itakuwaje ikiwa Messi ataweza kuiongoza Argentina kushinda kombe la dunia mwaka 2014? Kushinda kombe ndani ardhi ya Brazil - wenyeji wa mashindano, Nyumbani kwa akina Pele na nchi hasimu mkubwa wa soka wa Argentina - fikiri Pele atauweka wapi uso wake. Hapo ndipo vita yake ya maneo kumdidimiza na kumkosea heshima Messi itakapoisha pia pamoja na kumaliza ubishi nani ndio mchezaji bora wa muda wote.

Lionel Messi hajawahi au hatowahi kumjibu Pele na maoni yake. Hayupo hivyo, lakini kitu muhimu kabisa, Messi ameacha uwezo wake wa uwanjani kujibu mashabulizi yake yote.

Diego Maradona anamtetea Messi na pia amekuwa akimjibu Pele. Diego nae kama huwa anajibu "Mchezaji wa nchi yangu ni mkali kuliko wa nchi yenu."
Lakini tofauti na Pele, Maradona ana pointi anaposema mchezaji bora wa dunia anatokea nchini kwao.

Labda Pele amuulize Neymar nani ndio mchezaji bora wa dunia.

"Siku zote nimekuwa nikisema Lionel Messi ndio mchezaji bora wa dunia." - Neymar

Pamoja na haya yote lakini bado Pele ameendelea kumkosea Messi, na inasikitisha kwa jinsi anavyojishushia heshima kwa maoni yake ya kijinga juuu ya Lionel Messi.  Ikiwa bado anaendelea kuamini kwamba Neymar ni bora kuliko Messi labda ni kweli Pele haangalii La Liga, UEFA Champions League au vipindi vya michezo ulimwenguni- au inawezekana vyombo vya Brazil haviaandiki wala kuonyesha habari zinazomhusu Messi kama ambavyo wanafanya kwa Neymar.

Lakini tuache utani pembeni, Pele anaujua ukweli chini ya uvungu wa moyo wake kwamba Lionel Andres Messi ndio mchezaji bora wa duniana anaweza kuja kuwa bora wa muda wote. Hilo linamuumiza zaidi na tena sana kwamba mtu fulani atakuja na kuuteka ulimwengu wa michezo - sio tu soka, na kuheshimika, kusifiwa na kupendwa na wengi.

Inawezekana Maradona hakuwa anapendwa na wachache na kutoheshimwa na wengi, kwa goli lake la mkono wa mungu, tabia chafu, matumizi ya madawa ya kulevya na mdomo mchafu uwanjani.

Messi anaweza akawa hapendwi na baadhi, lakini tofauti na Maradona, Messi anaheshimika dunia nzima.

Baadhi ya watu wamesema kwamba Pele ana wivu dhidi ya Messi. Mimi nafikiri Pele ana wivu na umaarufu wa Messi ambao umefikia hatua mpaka watoto wa baadhi ya wachezaji wa timu pinzani mfano watoto wa John Terry wenye miaka mitano wanampenda kiosoka kuliko wanavyompenda baba yao - Messi amekuwa akipendwa mno na habari zake zimekuwa zikikumbatiwa mno na media na mashabiki duniani kote kuliko ambavyo ilikuwa kwa Pele.

Messi amekuwa globally known tena na hii teknolojia inavyorahisha mambo kutoka pande zote za dunia, amekuwa lulu kwa kampuni za matangazo kiasi kwamba ndio amekuwa mchezaji anayeingiza mkwanja mrefu kuliko wote duniani. Hili kosa la Pele, ni utandawazi wa dunia ya sasa, media na teknolojia ambayo ipo sasa, na haikuwepo wakati wa enzi za Pele kama mchezaji, hivyo Pele hapaswi kuwa na wivu na umaarufu namafanikio ya Messi.

Kama Pele ana wasiwasi kwamba watu watamsahau jina lake/ ikiwa Lionel Messi atakuwa mchezaji bora wa muda wote, anahitaji kutokuwa na wasiwasi. Pele ni moja ya wachezaji bora wa muda wote, aliuteka ulimwengu wa soka na inawezekana ndio aliyeshinda sana katika historia ya mchezo. Hakuna atakayeshinda makombe matatu ya Dunia.

Pele jina lako halitosahaulika ikiwa Messi atakuwa mchezaji bora wa muda wote. Tafadhali uache kumdidimiza kipaji alichopewa na mungu Lione Messi, badala ashangalie namna mtoto huyu wa kiargentina anayolipenezesha soka kwa aina ya mchezo wake.

5 comments:

  1. kaka kwa bahati mbaya sijawah juoba full time game la pele zsid ya clips tu,na kwa kawaida clips ndo vipande muhimu hata ktk kumuuzia mchezaj lakin hamna kitu baba kwa kulinganisha na huyu mtoto,huyu mtoto ni mkali pele sijaona mambo aliofanya kma alilnayo messi.

    ReplyDelete
  2. kaka kwa bahati mbaya sijawah juoba full time game la pele zsid ya clips tu,na kwa kawaida clips ndo vipande muhimu hata ktk kumuuzia mchezaj lakin hamna kitu baba kwa kulinganisha na huyu mtoto,huyu mtoto ni mkali pele sijaona mambo aliofanya kma alilnayo messi.

    ReplyDelete
  3. Kaka shaffi mikuna point moja nataka uione ambayo nahisi Pele anataka watu waione, unajua Messi nimchezaji bora wahichi kizazi hiyo aina upinzani ila kusema kuwa his the best player ever nahisi nimapema sana..Messi kwenye kabati lake la medali amekosa kitu kimoja tu nacho ni medali ya kombe ladunia wote tunajua barca ya sasa ndo timu takatifu na bora ambayo aijawai tokea kwaio huyu jamaa anachezeshwa na viungo bora walio unganisha nguvu namzungumzina Xavi na iniesta naiyo ndosababu kubwa inayo mfanya huyu jamaa a shine zaidi sizarau anakipaji namuda mwingine ana beba timu ila hawa watu wana mtumia vizuri..ndomana Messi anaitaji kuchukua kombe ladunia hasa kwenye ardhi ya Brazil pale uwanja mkubwa wa maracana..mdau wa Malaysia

    ReplyDelete
  4. Mchezaji mkali ni yule unayempeleka timu yoyote na akacheza kwa kiwango kilekile. Kwa hiyo Mess anatakiwa a-prove hilo. Naungana na Pele.

    Mchezaji mkali kama Eto'o ni wachache sana. Eto'o angekuwa sio mtu mweusi najua angelnganishwa na Pele pia.

    ReplyDelete
  5. da mdau umesema ETOO angekuwa mzungu angelinganishwa na pele kweli kabisaaa
    ila ARGENTINA HAIWEZI KUCHUKUA la dunia.
    etooo the fils

    ReplyDelete