Search This Blog

Friday, April 13, 2012

MAMBO MATANO YATAKAYOTOKEA IKIWA YAYA TOURE ATASTAAFU KUICHEZEA IVORY COAST

Mchezaji bora wa bara la Afrika mwaka 2011, Yaya Toure, , amepata mafanikio makubwa katika miaka 11 ya career yake, ambayo inajumuisha ubingwa wa Uefa Champions League akiwa na Barcelona na kombe la FA akiwa na Manchester City.
Japokuwa, kujiuzulu ama kustaafu katika soka la kimataifa na timu yake ya Taifa ya Cote d'Ivoire akiwa tu miaka 28, bila kupata tatizo lolote litakalopelekea kuchukua uamuzi huo, uamuzi huu unaonekana hauna mashiko kwa mchezaji ambaye anaonekana kuwa katika kilele cha kiwango chake cha soka.

Nini tatizo lilopelekea uamuzi wake. Whatever the reason nyuma ya uamuzi huu ambao ameupanga kuuchukua hivi karibuni kujiengua kutoka kwa Tembo wa Afrika, utapelekea kutokea kwa vitu kadhaa ambavyo havitaepukika kutokea kutokana na uamuzi wa Yaya kustaafu kucheza soka la kimataifa.

5. KUCHUKIWA NA MASHABIKI
Yaya Toure kwa sasa ni mchezaji maarufu na anayependwa kuliko na mashabiki wengi nchini kwao nyuma ya Didier Drogba. Mchezaji huy wa zamani wa Barcelona ni role model na anaangaliwa kama mfano wa kuigwa na vijana wengi wanaocheza soka na wenye ndoto za kuwa kama yeye.

Ni mtu anayesaidia sana katika mapambano dhidi ya HIV-aIDS,  amefanya matangazo mengi ya TV. Kuondoka kwake katika timu ya taifa kutaanza kuonekana katika mashindano makubwa ya timu ya taifa kama vile AFCON, au World Cup.

Kwa hakika mashabiki watakuwa wakiombeleza kutokuwepo kwake na wanaweza hata kumbadilikia na kumchukia kwa kutoonyesha mapenzi kwa timu yake ya taifa, kutokana na kujiuzulu bila sababu za msingi.

ATAPOTEZA HESHIMA YA KUDUMU
Ikiwa timu ya taifa ya Ivory Coast itafanya vizuri na kufanikiwa kucheza kwa mafanikio katika michuano ya AFCON 2013 au 2014 World Cup bila kuwepo kwa Yaya, mchezaji huyo atakuwa amefanya kosa kubwa sana katika maisha yake ya soka.

Ikitokea hivyo Yaya atapoteza heshima kubwa aliyokuwa amejiwekea, legacy itapotea kama upepo, na wachambuzi wa soka nchini kwao watakuwa wa kwanza kuwakumbusha mashabiki kwamba hakuwa na umuhimu mkubwa katika kuiletea mafanikio Ivory Coast.

Mashabiki siku zote huwa na mapenzi na waliopo na sio waliopita, au huwa wana tabia ya kusahau historia pale mambo yanapowaendea vizuri na timu zao wanazoshabikia, na haitowachukua muda mrefu kumsahau Yaya ikiwa nchi yao itaingia katika zama za ushindi bila yeye.

MADHARA KWA KWACHEZAJI WENZIE
Ni namna gani hali ya kuondoka kwa Yaya katika timu ya taifa kutawaathiri wachezaji wenzie ndani ya timu ya taifa? Wengine walisema wataachia jahazi kwa vijana ikiwa timu ya taifa itashindwa kuchukua ubingwa wa AFCON 2012. Timu ikafungwa kwenye fainali na Zambia na huku hakuna hata mchezaji mmoja aliyesema anajiuzulu baada ya mchuano kumalizika.

Je kujiuzulu kwa Toure kunaweza kuchochea kuondoka kwa wengine, katika njia moja kama ilivyokuwa kwa Zinedine Zidane alipojiuzulu kucheza timu ya taifa wachezaji wengine walimfuata kama vile Lizarazu, Marcel Desailly, Claude Makelele na Lilian Thuram. Je wachezaji wakubwa wa Ivory Coast hawatofuata mfano wa akina Lizarazu baada ya Toure kuondoka ikizingatiwa walishasema watawapisha vijana ikiwa watafeli kuchukua kombela afcon 2012.

IVORY COAST KUPOTEZA MCHEZAJI MUHIMU
Kuondoka kwa Toure kutaleta utofauti mkubwa katika kikosi cha The Elephants. Ni mchezaji muhimu katika timu kwenye nafasi ya ulinzi na mashambulizi, na kutokuwepo kwake kutaleta mianya ambayo iliwafanya wawe wagumu katika kushindana nao siku za nyuma.

Mchezaji huyu Manchester City anakamilisha namba ya wachezaji wa class ya dunia wanaoipa Coted'Ivoire uwezo mkubwa wa kiakili na kinguvu na uwezo wa soka.
Jukumu lake la kuvunja mashambulizi ya wapinzani, kugawa mipira, kupiga mashuti na ku-cover ukuta wake likumuangukia mtu mwingine katika kikiosi cha kwanza, hakuna guarentee kwamba mbadala wake atakuwa na uwezo kama wake au kupata mafanikio kama ya mdogo wake Kolo Toure.

KUMKOSA KIONGOZI
Timu ya Ivory Coast itammiss uwezo wa Yaya kuzuia na kugawa mipira katika midfield, ikizangatiwa kwamba mchezaji wa zamani wa Tottenham Didier Zakora, ambaye alikuwa ndio the best katika eneo hilo kwa sasa ndio anaishia, na mchezaji wa Newcastle Cheik Tiote bado hajaweza kujitengenezea nafasi wala jina katika timu ya taifa.

Na huku michuano ya AFCON 2013 ikikaribia, itakuwa taabu sana kupata mbadala halisi wa Yaya kama kiongozi wa asili pale  katikati ya dimba na mchezaji aina ya TIOTE, haswa pale presha ya kufanya vizuri inapoongezeaka ndani ya kikosi wachezaji wengi wenye uzoefu ndio wangeweza kuhimili mikikimikiki.

Kwa maana hiyo kumkosa Toure katika situation za namna ni pengo  la kiuongozi ndani ya kikosi .

No comments:

Post a Comment