Search This Blog

Monday, March 5, 2012

ZLATAN IBRAHIMOVIC: KWANINI NILIKATAA KUJIUNGA NA ARSENAL?



Zlatan Ibrahimovic amefichua kwamba alikataa kuhamia Arsenal kwa sababu Arsene Wenger alitaka mshambuliaji huyo aanzie kwanza kwenye majaribio.
AC Milan player alikuwa mdogo kiumri alipokutana na Wenger in 2000 kuzungumza juu ya uwezekano wa kuhamia London ya kusini.
Ibrahimovic, 30, aliliambia gazeti la The Sun: ‘Arsene alinipa jezi maarufu ya rangi nyekundu na nyeupe – ikiwa imeandikwa jina langu na namba tisa mgongoni, nilifurahi sana hata nikapiga picha na jezi ile.
“Ulikuwa ni wakati mzuri kwangu. Arsenal walikuwa na kikosi kizuri sana lakini wakanifuata mie huku jezi namba 9 ikiwa na jina langu mgongoni.
“Hivyo nikasubiri Wenger anishawishi nijiunge na Arsenal. Lakini hata hakujaribu.
“Hakuwahi kunipa ofa iliyo serious, ilikuwa like “Nataka kuona unajua kucheza vizuri kiasi gani, yaani nifanye majaribio”
“Sikuweza kuamini kwa sababu uwezo wangu alishauona. Zlatan hawezi kufanya majaribio.
“Niliwaza “Aidha hunijui au unanijua na kama hunijui basi huwezi kunitaka mimi”.
“Unaona , hata nilipokuwa mdogo nilikuwa najiamini sana hata kama nilikuwa mdogo.
“Nina hakika kwamba kuna baadhi ya wachezaji wachanga wangeweza kukubali kufanya majaribio kwa sababu ilikuwa ni Arsenal na Yule alikuwa na Arsene Wenger.
“Lakini nilijua haikuwa tu ni Arsenal waliokuwa wakinitaka – Roma na Ajax zote zilikuwa zikipigania saini yangu.
“Hivyo nilisema “Hapana na mwisho wa siku nilisaini kwa Ajax, Lilikuwa chaguo sahihi.
Ibrahimovic badala yake akajiunga na Ajax , ambapo alichukua makombe 8 mfululizo, na baadae akaenda Juventus – ambapo alishinda makombe mawili ambayo baadae walipokonywa kutokana na scandal ya Calciopoli kabla hajaenda Inter, Barcelona na sasa yupo Milan.


Pia alikuwemo katika kikosi cha Milan kilichoshinda goli 4-0 dhidi ya Arsenal katika Champions league, na akafunga hat-trick jana usiku dhidi ya Palermo.
Arsenal wanacheza na Milan jumanne iajyo katika mechi ya pili ya hatua ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment