Search This Blog

Sunday, March 11, 2012

YANGA YATANDIKWA 3-1 NA AZAM - WAMPIGA MWAMUZI NA MASHABIKI WAO WAFANYA VURUGU UWANJANI.

BEKI WA YANGA NADIR HAROUB CANNAVARO AKITOLEWA UWANJANI CHINI YA ULINZI WA POLISI HUKU KOCHA WAKE KOSTADIN PAPIC AKIMSINDIKIZA BAADA YA KUMPIGA REFA NA KUPEWA KADI NYEKUNDU.

BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA WAKIMPA KICHAPO MWAMUZI BAADA YA NIYONZIMA KUPEWA KADI NYEKUNDU.



BONDIA CANNAVARO AKITOLEWA NJE YA UWANJA HUKU AKIPOOZWA NA KOCHA WAKE.
HIVI NI BAADHI YA VITI VILIVYONG'OLEWA BAADA YA VURUGU KUTOKEA KATIKAJUKWAALA YANGA



HAPA NAHODHA WA YANGA NSAJIGWA AKIJARIBU KUMZUIA CANNAVARO ASIWEZE KWENDA KUENDELEZA FUJO KATIKA MCHEZO HUO.







         
M
Mwamuzi Israel Mkongo pamoja na wasaidizi wake akitoka nje kwa kusindikizwa na askali wa kikosi cha kutuliza Ghasia FFU mara baada ya kupuliza kipenga cha mwisho kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu ya Yanga ya Jangwani na timu ya Azam FC kutoka Chamazi ambapo Yanga imekandamizwa magoli 3-1 na wauza Sembe hao wa Chamazi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
 
Mwanzo ulikuwa ni mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza, mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima aliendelea baada ya muda, alitolewa nje kwa kadi nyekundu, jambo ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na vurugu hizo na kuzua tifu lingine uwanjani.

No comments:

Post a Comment