Arsene Wenger amekiri jana usiku kwamba kama kikosi chake cha Arsenal kitafanya maajabu jioni ya leo basi hiyo ndio itakuwa mechi ya mafanikio kuliko zote.
Arsenal inabidi washinde zaidi ya 4-0 katika mechi ya pili ya Champions league.
Wenger alisema: “Itakuwa ni siku yangu ya furaha kabisa. Nitakuwa na furaha kupita kiasi na jambo hilo.”
Na bosi huyo wa Gunners alitoa ishara kwamba anaweza kuwapanga washambuliaji wanne huku akiwa viungo wawili.
Mikel Arteta yupo nje kama tahadhari kwa sababu ya majeruhi ya kichwa aliyoyapata dhidi ya Liverpool huku majeruhi wengine Abou Diaby na Aaron Ramsey nao wapo nje.
Alex Song na Tomas Rosicky wapo fiti lakini Rosicky ana matatizo na korodani.
Wenger pia anaweza kumchezesha Alex Oxlade-Chamberlain kama kiungo mchezeshaji.
Wenger pia alisema: “Sina uhakika kama Rosicky atakuwa yupo fiti au vipi. Kama hayupo fiti nitakuwa katika wakati mgumu sana.
“Jana aliniambia kwamba atacheza lakini jopo la madaktari hwana uhakika. Naweza nikacheza kamari kwa sababu sina chaguo lingine.”
No comments:
Post a Comment