Robinho jana usiku aliwaambia Arsenal: Hamna nafasi ya kufanya maajabu katika mechi yetu ya Champions league.
The Gunners wapo nyuma kwa goli 4-0 baada ya kufungwa katika mechi ya kwanza mjini Milan – huku magoli mawili yakifungwa na Mbrazil huyo.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City Robinho alisema: “Nikiwa City, sikuwa na bahati sana lakini nimeonyesha nini naweza kufanya hapa Milan na nimedhamiria kuwa na siku nzuri tena leo usiku huu.
“Arsenal wameimarika tangu tulipowafunga lakini ni vigumu karibu na kutowezekana kwa wao kuweza kubadilisha matokeo ya mwisho.
“Tulikuwa wababe San Siro - 4-0 ulikuwa ni ushindi mzuri . Robin Van Persie ni mshambuliaji wa kutisha lakini hawezi kubadili matokeo leo hii.
“Sidhani kama atacheza vizuri katika mechi dhidi yetu kama alivyofanya kaatika michezo ya ligi hivi karibuni.”
No comments:
Post a Comment