Search This Blog

Friday, March 23, 2012

WANAMICHEZO 10 WENGINE WALIOTAWALA KWENYE MICHEZO YAO KAMA LIONEL MESSI KWENYE SOKA





Bila shaka zama hizi za soka ni zinamilikiwa na Massiah wa soka bwana Lionel Messi, hivyo blog yako pendwa leo inakuletea wanamichezo wengine kutoka kwenye michezo mingine, kwakutawala michezo wanaocheza na kuvunja rekodi mablimabli kama Messi.

BOXING -MUHAMMAD ALI
Kuna tofauti kati ya kuongea na kutembea. Muhammad Ali alifanya vyote kama ambavyo hajawahi kufanya bondia yoyote kabla yake. Alikuwa ndio bondia wa kwanza kushinda ubingwa wa uzito wa juu duniani mra tatu, 'The Louisville Lip' alipigana mapambano mengi maarufu kuliko katika historia ya mchezo huo. Pia aliutumia umaarufu wake vizuri kuliko mtu yoyote kwenye listi kwa kupigania haki za kiraia nchini Marekani katika miaka 1960s. Muhamad Ali-The Greatest.

USAIN BOLT - RIADHA
Binadamu mwenye kasi kuliko wote katika historia, Bolt anashikilia rekodi kwa mita 100 na 200: rekodi ambazo sio tu alizivunja bali aliziharibu haribu kabisa. Bingwa huyo wa Olympic na Dunia ameweka rekodi ambazo ni watu wachache walidhani inawezekana. Na kikubwa zaidi kijana wa watu bado mdogo sana ana miaka 25 tu fikiria akifikia umri wa Haile Gab. itakuwaje? atakuwa kavunja rekodi ngapi. Kama Messi vile.

ROGER FEDERER - TENNIS
Wengi wanaamini ndio mwana tennis bora kuwahi kutokea kwenye historia ya mchezo huo. Mswiss huyo amevunja rekodi na kuchukua grand slams mara 16 tangu aanze kucheza tennis. Hakuwahi kutetereka alipokuwa kwenye peak yake, Federer amecheza mara 18 kati ya 19  grand slam finals kati ya Wimbledon 2005 na Australian Open ya mwka 2010. Akiwa bado anaendelea kucheza Federer ana mengi ya kufanya katika Tennis mpaka atakapokuja kustaafu.

WAYNE GRETZKY - ICE HOCKEY
Wanamuita 'The GreatOne', mcanada anayekubalikadunia nzima kama mwana hockey aliyebarikiwa kuliko wote katika historia ya mchezo huo. Wayne amedumu kwa miongo miwili katika Hockey huku akivunja kila rekodi katika kitabu cha hockey. Mcananda huyu anabkia kuwa mfungaji bora wa muda wote wa NHL.




 MICHEAL JORDAN
Mchezaji bora wa muda wote wa mpira wa kikapu na pia ndio mchezaji aliyekuwa akikubalika kiniashara kuliko wote katika historia ya mchezo huo. Uwezo wake ulimfanya awe mwanamichezo aliyekuwa maarufu kuliko wote dunianai kwa sababu ya mambo aliyokuwa akiyafanya pale Chicago Bulls katika miaka ya 1990s. Jordan alishinda ubingwa wa NBA mara 6 kwa ujumla na alitajwa kama NBA MVP kwa mara tano mfululizo. 



JONAH LOMU
Superstar wa Rugby namba moja duniani, Jonah Lomu aliushangaza ulimwengu mzima kwa uwezo mkubwa aliounyesha kwa New Zealand katika World Cup1995. Akisimama mita 1.96 huku akiwa na uzito 125 kg, Lomu alikuwa na kasi na nguvu kuliko mchezaji yoyote aliyewahi kuonekana kwenye Rugby. Alikuwa anaitwa 'freak' na Will Carling baada ya The All Blacks winga kuwapita wachezaji wote wa timu yake ya England katika nusu fainali. Kwa bahati the top tryscorer katika World Cup, career yake aliingiliwa na matatizo ya figo na akaacha. 


MICHEAL PHELPS
Anatajwa kwamba ni bora kuliko wote katika Olympic, muongeleaji wa kimarekani amechukua medali nyingi za dhahabu kuliko mtu yoyote  - Phelps alishinda sita kati ya hizo mjini Athens in 2004 - akiweka rekodi kabla ya kuivunja mjini Beijing kwa kushinda medali nane za dhahabu na kuvunja rekodi Mark Spitz aliyechukua medali saba za dhahabu katika mchezo mmoja in Munich mwaka 1972, huku michuano ya 2012 pale London ikikaribia Phelps sasa anategemewa kuwa ndio mwanamichezo aliye na historia ya mafanikio katika olympic na kumfikia Larisa Latynina mwenye medali za dhahabu 18.




 
MICHEAL SCHUMACHER
Hata kama bado kuna mjadala kama Micheal Schumacher ndio dereva bora wa formula one, lakini mjerumani huyu alitawala mchezo kuliko ambavyo imehawi kutokea kabla yake kipindi ambacho ferrari ilitamba vibaya mno, ambapo alishinda mara tano mfululizo ubingwa wa mbio za magari ya formula one. Hivyo kufikisha mara 7 kwa jumla ya ubingwa huo. Kama ilivyo kwa Wayne Gretzky kwenye mchezo wake, mjerumani huyu pia ndio amechukua ubingwa mara nyingi katika mchezo wake. 


SACHIN TENDULKAR
.The leading run-scorer and century maker in Test and international one-day cricket, the Indian is, with all due respect to Donald Bradman, now rated by many as the finest batsman in history. ‘The Little Master’ made his Test debut, against Pakistan, at just 16 and has been breaking records ever since. Indeed, Tendulkar, now just a month shy of his 39th birthday, only last week became the first man to rack up 100 international centuries.


TIGER WOODS





Je Tiger Woods ni mchezaji bora wa gofu wa muda wote? Mjadala unahitajika, ukiangalia sasa haonekani kama atafikia rekodi ya Jack Nicklaus ya kushinda makombe makubwa. Japokuwa, Woods aliingia kwa kishindo kikubwa kwenye mchezo huu na kuutawala kwa kipindi kirefu kwa takribani miaka 10 tena kwa kishindo. Akiwa ndio mmoja ya wanamichezo waliotengeneza pesa nyingi sana kupitia mchezo huu.

No comments:

Post a Comment