Search This Blog

Thursday, March 1, 2012

MAONI YA BAADHI YA WADAU JUU YA SOKA LA BONGO!

Mara tu baada ya mchezo baina ya TANZANIA na MSUMBIJI hapo jana kumalizika, niliandika article ya kuachwa kuitwa kikosini mshambuliaji Mbwana Samatta yenye kichwa cha habari,

Jan Poulsen hawezi kukwepa lawama za kutomuita Mbwana Samatta

kuachwa kwa Samatta kwenye kikosi cha Stars kwa mtazamo wangu ni kama vile kenya kuacha kumuita mshambuliaji Dennis Oliech ama Argentina kutangaza kikosi bila ya Messi au Ureno bila Ronaldo.
haya ni baadhi ya Maoni ya walioisoma hii article...

Kaka shafi napingana na wewe.

Kwa muda mrefu kumejengeka tabia ya waandishi ya habari za michezo kutoa uchambuzi wa michezo kwa kutegemea matokeo ya mechi husika.Mathalani ikitokea siku timu imeshinda, mchambuzi atatoa uchambuzi wenye kuonyesha ubora au uimara wa timu iliyoshinda huku mapungufu yakiwekwa kapuni (hata kama mapungufu yalikuwepo mengi tu). Wachezaji watapambwa na kusifiwa pasipo kifani utafikili walicheza mpira kama ule tunaoushuhudia ukichezwa na timu bora barani ulaya! Vilevile, wachambuzi hawa wamekuwa na mtazamo wa kuangalia performance ya mchezaji mmoja mmoja zaidi, wakati mpira wa kisasa unategemea zaidi timu kucheza pamoja yaani teamwork. Kuna timu zina wachezaji hawana majina makubwa lakini zinaogopwa kwa mchezo wao wa pamoja. Mfano mmoja ni Napoli ya italia! Kwa bongo si ajabu kusikia timu haikushinda kwa sababu mchezaji fulani alikosekana!

Lately kumekuwa na habari kwenye media eti national team jana haikushinda kwa sababu mbwana samatta hakuwepo. Napingana na hoja hii. Hiyo ni short sight, huyo ni mtu mmoja na sio kweli kama ana uwezo kama inavyoelezwa. Waandishi na wachambuzi hawa wanapaswa kuwa makini na wanayoyaongea. Wakati wa maximo wananchi wakisukumwa na waandishi/wachambuzi hawahawa walikuwa wakimshinikiza kocha kuchagua wachezaji fulanifulani. Leo hii watu haohao wanamponda mzungu pulsen wanasema afadhali ya maximo!. Jamani huyo mzungu habahatishi! hiyo ni taaluma yake kaisomea! Huyo ni mtaalam wa ngazi ya juu haitaji wiki nzima kumtazama mchezaji na kujua kama anamfaa au la!. Kwa mtazamo wangu, mwalimu alipata fursa ya kumwona samatta na naamini hata maamuzi ya kumwacha yalizingatia uchambuzi wake wa kitaalam kama mwalimu. Siamini kama angeweza kumwacha tu pasipo na sababu ya msingi, kwani timu ikishinda ni sifa kwake pia!.


Kwa upande mmoja tunatambua kuwa waandishi/wachambuzi wanapaswa kuandika au kusema! Kwao hii ni kazi! Na naamini wanalipwa kwa kazi hiyo! Hivyo ni lazima waseme au waandike! Lakini kwa upande wa pili naamini waandishi wana jukumu la kutoa taarifa sahihi pasipo kupotosha umma. Na ili waweze kutoa taarifa sahihi wanapashwa wajielimishe ili wajenge ‘competence’ kwenye eneo hili. Kwani si kila mtu anaweza kuandika habari za michezo, ni lazima awe amepata taaluma ya michezo! Jamani michezo ni taaluma inasomewa kama zilivyo taaluma zingine. Nimesema hivi kwa sababu ni rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuamini kile anachokisoma au kukisikia kwenye media.

Mtazamo wangu kuhusu michezo hapa nchini ni kuwa tunahitaji kufanya uchambuzi mpana zaidi wa mfumo mzima wa mpira nchini na kuufanyia kazi. Mfano Je kuna Sera na Mkakati na Programu kuhusu michezo? Je kuna mfumo wa kitaasisi wa kutekeleza sera, mkakati na program? Je mfumo unakidhi au unahitaji maboresho? Je sera, mkakati na program vinatafsiriwa vipi kivitendo? Je mfumo unatoa fursa ya utambuzi, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji? Muundo wa timu zetu ukoje? Je mfumo wa timu zetu unatoa fursa ya utambuzi, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji?
Vinginevyo hizi hadithi za kulaumu makocha na wachezaji hazitaisha NG’O!

Mdau wa Michezo,
George

1.     Asalam alaykum wadau,
Nakushkuru sana kaka Shaffih kwa kutupatia maelezo/maoni/ushauri wa kina kuhusu soka la Tanzania. Hii ni faraja kwangu binafsi na baadhi yetu kwani tunapata sehemu ya kuanzia ama kuongezea pale ulipopaacha wewe.
Sikuweza kuiona mechi hii lakini kutoka na malezo yako nimepata picha fulani na mimi sasa naendeleza kidogo kama ifuatavyo:
Sijui pattern or system or formation waliyocheza lakini ki uhalisia kama walikuwa beki wa kati wanakwenda pembeni kuficha nafasi ya Mwasika nadhani huu ni utaratibu hasa pale timu inapomtumia beki kama winger ama kiungo, na hapo ilitakiwa viungo wa kati (Nditi/Kazimoto)na/au mawinger (Nizar/Barnabas) kuingia kati kuficha nafasi iliyoachwa na beki wa kati aliyekwenda kumfichia makosa beki wa pembeni huku Mwasika (beki wa pembeni) akirudi kwa style ya kuingia kati. System hii huchezwa zaidi timu inapocheza 4-4-2 au 4-4-1-1.

Kwa suala la timu kufanya vibaya naweza kusema inatokana na wachezaji kutokujiami, wachezaji wetu hawajiamini hata kidogo, wamezidiwa na papara kuanzia mabeki mpaka wafungaji isipokuwa kwa wachache sana ambao nathubutu kuwataja kuwa ni Shaaban Nditi, Mbwana Samatta na Shomari Kapombe. Wadau wanapiga kelele Samatta Samatta Samatta nawaunga mkono japo kuwa hawajui undani na ukweli wa Samatta. Uzuri wa Samatta ni utulivu anapokuwa na mpira ambao unamjengea kujiamini, kitu ambacho asilimia kubwa ya wachezaji wanakikosa. Chukulia mfano mechi ya nyumbani tulipocheza na Algeria, goli alilofunga Samatta ni kutokana na utulivu na kujiamini. Tunahitaji wachezaji wa namna hii na ndio maana wadau wanataja Samatta.
Wachezaji wenye utulivu na kujiamini wanaweza kupatika kuanzia soka la yosso (vijana wa umri mdogo), mchezaji anapoanza kucheza soka la ushindani akiwa mdogo anajijenga kujiamini, sio leo mtu ana miaka 27 (ya ukweli 35)ndio anaanza kucheza timu ya Taifa kwa mara ya kwanza, hivi unadhani kutakuwa na kujiamini hapo?
Wakati umefika kwa TFF (kamati ya ufundi/kocha) kuwaamini vijana, hii namaanisha kwa vile hivisasa wapo vijana wengi walioibuliwa kutoka michuano mbali mbali, kama vile Uhai Cup, Coca cola n.k inapotokea mashindano basi tusilenge kwamba lazima tuchukue kombe, badala yake watumiwe vijana ili kuwajengea kujiamini na utulivu, hii itasaidia kwa michuano ya baadae ambapo tutakuwa na timu nzuri na imara yenye kujiamini, wenzetu ndivyo wanavyofanya hivyo, wachezaji kama Henderson,Sturridge, Welbeck, Walcott na wengineo ndivyo wanavyokomazwa. Kama tunakumbuka mchezo wa kirafiki kati ya Stars na Zambia uliochezwa Morogoro na matokeo yalikuwa 1-1, Zambia walichezesha vijana wengi ambao kimsingi walikuwa wanawapa ukomavu, na ndio vijana wale leo walioiletea heshima nchi yao. Lakini kwetu ikitokea hata Stars inacheza mechi ya kirafiki hakuna sura mpya za vijana wanaokomazwa. Hapo ndio tunamkumbuka Marcio Maximo pamoja na lile la kuhamsisha wachezaji na wananchi kuipenda timu yao.

Maasalaam.

Bebeto.

1.     habari kaka shaffih mimi napenda sana soka, imi ni mdada napenda sana sana sana namizwa na viongozi, mackocha na wachezaji wenyewe, tufike mahali tuseme asante kwa maximo, japo halaiki ilimponda sana, nimekuwa nikikata tamaa hata kwenda kuangalia mechi za Taifa starz kwa sababu kubwa kuogopa kuumia kwa kufungwa, naona bora kesho yake niblog kwako nione, hii ni kwasabu hawana au hawatoi mvuto kwa mashabiki,na wapenzi wa soka. jamani vijana wadogo wanaochipukia wapo waitwe waunde timu ya taif nzuri na imara. tujifunze hata kwa hawa tuliocheza nao leo, wamepikwa tangu 2006 leo ije kuwa sisi tunakurupuka tu kutoka huko tutokako na kupasha siku 2 au 3 tu kisha tunawavaa jamii iliyoandaliwa vizuri, si vizuri jamani kocha pamoja na wadau wengine wakae waone huyu ibilisi anayetushikilia sisi kila mara anaitwa nani katokea wapi na wamkemee nasi siku moja tuone timu yetu kwenye nusu au robo fainali ya World cup jamani, kaka natamani sana kuongea mengi maana ninauchungu sana na timu yangu. kwa upande mwingine kama tumeshindwa kumkeamea huyu ibilisi kwa wakaka basi tumzibiti kwa wadada nao asiwaharibu pia, maana hao kidogo nyota inang'aa huenda tukaona neema kupitia wao, KAKA NAUMIZWA SANA NA MATOKEO MABOVU YA TIMU YETU HASA YA TAIFA STARS.

Ndimi mpenzi, mdau na shabiki wa timu zetu za TANZANIA, NAITWA LUCY IZENGO,

MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU IBARIKI TAIFA STAZ NA TWIGA STAZ AMINA.

2 comments:

  1. mawazo/maoni yaliyotolewa na wadau hapo juu si mabaya sababu kila mtu anamtazamo wake kwenye kila jambo anapolitazama au kulifikiri. Ila mimi nataka kupingana na Bw. GEORGE [Mchangiaji wa kwanza kama ilivyoorodheshwa hapo juu] kwa hoja zifuatazo.

    1. Timu yoyote ile ambayo ina uhai hapa duniani hata kama ikicheza team work 100 percent ni lazima pawepo na mtu angalau mmoja au wawili ambao watatumia uwezo binafsi na umakini wao kuleta ushindi kwenye timu, hilo huwezi kulipinga kutokana na mpira wa sasa ulivyo. Kwa mfano: Man United bila ROONEY utaona wanapata tabu sana kushinda, au ARSENAL ya leo bila ROBIN Van PERSIE pale mbele na pale kati akikosekana SONG BILLONG utata huonekana kwenye perfomance ya team. Hiyo ni mifano michache tu ingawa ipo mingi na yenye mantiki. Tazama mabingwa wapya wa Africa [ZAMBIA] pale kati walikuwepo watu wawili muhimu sana ISACK CHANSA na KALABA kukosekana kwa hawa watu zambia ingekuwa na wakati mgumu sana...pia pale mbele alikuwepo captain mwenye CHRISTOPHER KATONGO huyu mtu balaa bana we acha tu.

    2. Napenda kukukumbusha tu kuwa NAPOLI ni timu moja nzuri yenye kucheza ki-team work huku ikiwa na wachezaji muhimu inaowategemea kufanya matokeo yawe mazuri kwao, utaizungumziaje NAPOLI bila EDINSON CAVANI na EZEQUIEL LAVEZZI pale mbele, au MAREK HAMSIK pale kati!!??? kama ni mpenzi wa mpira na unafuatilia serie A kwa karibu na si kusubiri uione NAPOLI kwenye UCL hapo utakuwa unakosea sana kaka

    MWISHO, napenda kusema kuwa SAMATTA ni muhimu sana kwenye timu ya Taifa [TAIFA STARS] na kukosekana kwake ni tatizo kubwa sana, kuna kitu ambacho Kocha POULSEN anashindwa kufanya uamuzi wa maana, kuwa mfungaji bora wa league haimaanishi hata ukiperfom vibaya then watu wakae kimya eti kisa kwenye VPL unafunga magori. Huyu JOHN BOCCO hawezi kutufikisha kokote kule kwenye hii safari yetu, hebu jiulize kwanza tangu aanze kuvaa jezi ya timu ta taifa kafunga goli ngapi? then ukipata jibu ndo utajua kwanini wadau tunalia na uwepo wa SAMATTA pale mbele
    NASHUKURU SANA KWA MJADALA HUU

    ReplyDelete
  2. Huyo mdau wa kwanza george aende shule ya muzik aachane na mpira kbsa.bac watu wasimlahumu wenger kwa anachokfanya,asilaumu viongoz wa nchi yke kwa wanayoyafanya,wao c wataalam yeye ni mbumbumbu!mtu akikosea na imeonekana wazi lazma aambiwe kuwa amekusoea NO ONE IN THIS WORLD IS 100% PERFECT. In short huyo kocha na huo mfumo wake wa uzeeni hatufai.

    ReplyDelete