Search This Blog

Wednesday, March 7, 2012

MANCINI: BALOTELLI FANYA UOE UTULIE


Kocha wa Manchester City Roberto Mancini amedai kuna njia moja tu ya kumrudisha kwenye mstari sahihi Mario Balotelli nayo ni kumpata mwanamke wa kumuoa.

Mshambuliaji huyo mwenye vituko kwa sasa yuko na mchumba wake mwanamitindo Raffaella Fico inavyoonekana kuwa ni wazo zuri kwao kufunga ndoa.

Kocha Manchester City, Mancini amekuwa akihumiza kichwa kutafuta dawa ya kumtuliza  Balotelli kutoka kwenye vitendo vyake.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 21, alitawala vyombo vya habari wakati alipojaribu kufunga bao kwa kisigino dhidi ya Los Angeles, aliwasha moto kwenye chumba chake na tukio la karibuni zaidi ni lile la kwenda katika klabu ya usiku wakati wakijiandaa na mechi ya Jumamosi dhidi Bolton.

Mancini alisema: "kwa sasa bado ni kijana, lakini wakati atakapofikisha miaka 25 au 26 itakuwa ni vigumu kwake. Kama hatokuwa na maisha mazuri yake binafsi hatoweza kucheza kwa kiwango cha juu. Utakuwa ni muda wake wa kuoa? Anatakiwa kuoa."

Wakati huohuo; Beki Kolo Toure anamatumaini ya kusahau sababu za kufungiwa kwake kwa kutumia dawa kwa kuhakikisha anaisaidia Manchester City kutafuta ubingwa.

Ataungana na Carlos Tevez ambaye alioneka mbele ya watu akiwa kama mchezaji wa akiba wakati City ilipocheza dhidi ya Bolton.Maisha ya soka ya Toure yaliharibika baada ya kubaini kutumia dawa za kuongeza nguvu.

Beki huyo wa Ivory Coast, 30, alitumia dawa za mkewe za kupunguza uzito na kufungiwa kwa miezi sita. Lakini kwa sasa nahodha huyo wa zamani wa -City anatarajiwa kurudi upya kwenye timu hiyo.

Alisema: "Ninafuraha kubwa leo. Nilikuwa mwenye hasira sana siku za nyuma.

No comments:

Post a Comment