Search This Blog

Thursday, March 8, 2012

MABEKI WATANO WANAOFAA KUMRITHI PATRICE EVRA KATIKA KIKOSI CHA MAN UNITED




 Patrice Evra amekuwa katika kisicho kizuri katika ukuta wa Manchester United msimu huu. Perhaps ni muda sasa Sir Alex Ferguson akaanza kutafuta mbadala wake katika mbavu ya kushoto ya kikosi cha United.
Dhidi ya Chelsea at Stamford Bridg, Evra alikuwa ndio uchochoro katika magoli yote matatu  ambayo United walifungwa. At Anfield wiki moja kabla ya mechi ya Chelsea, pia alikuwa mwenye makosa kwa goli la ushindi la Liverpool.
Evra amekuwa akishuka kiwango tangu wakati wa 2010 World Cup, na kwa pointi iliyofikia sasa sio tena kupoteza fomu kwa muda mfupi  tu. Kila kosa analofanya uwanjani linatoa ishara kwamba Evra wa sasa sio yule miaka 3 iliyopita.
Evra inawezekana mmoja ya wachezaji waliocheza mechi nyingi kuliko wote katika kikosi cha sasa cha United  ndani ya kipindi miaka 3 iliyopita. Ni mara chache sasa unaweza ukamkosa katika first eleven ya United, na ndio maana imekuwa vigumu kumuona mchezaji mwingine akipata nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Huku ikionekana dhahiri kwamba beki  mwingine wa kushoto anahitajika, swali linabaki nani anafaa kumrithi Evra.
Hawa ni wachezaji watano ambao wanaweza kufaa kabisa kumsaidi na hatimaye kumbadili Patrice Evra kama beki wa kushoto wa United.


FABIO DA SILVA
Fabio da Silva ndio wa kwanza katika listi ya wanaofaa kumbadili Patrice Evra katika ukuta wa United.
Wakati pacha wake Rafael tayari amekuwa akipewa nafasi zaidi katika kikosi cha kwanza, upande wa kulia, Fabio amekuwa akihangaika kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Katika misimu minne pale Old Trafford, Fabio amecheza mechi 50 katika kikosi cha kwanza. Pia hali hii imetokana na majeruhi. Muda mrefu wa maisha yake nchini England ameutumia katika chumba cha  matibabu, na jambo hilo limekuwa kikwazo kwake kupata nafasi ya katika kikosi cha kwanza.
Pamoja na majeruhi lakini Fabio amecheza katika mechi kubwa kwa United. Huku kaka yake akiwa nje kwa majeruhi msimu uliopita, Fabio alikuwa anacheza  mara kwa mara katika shavu la kulia katika kipindi cha mwisho cha msimu wa 2010/11. Uwezo wake aliouonyesha kipindi kaka yake akiwa nje ya dimba hatimaye ulimsaidia kupata nafasi ya kucheza dhidi ya Barcelona katika 2011Champions league Final.
Pamoja na hayo, lakini mashabiki wa United wana wasiwasi na umakini wake.
Kinda hilo lenye miaka 21 ni mara chache amekuwa anadumu kwa dakika zote 90, na hiyo inasababishwa poor tackles,ambazo husababisha faulo au kujiumiza mwenyewe.
Huku Ferguson akiwa hajafanya usajili wa kuimarisha beki ya kushoto, then mtu pekee anayebaki sasa na ndiye aliyenae ni Fabio. Ikiwa Evra atakuwa dropped, then Fabio lazima awe wa kwanza kattika mstari wa kumrithi Evra.


EZEKIEL FRYERS
Zeki Fryers alicheza mechi yake ya kwanza kwa Manchester United msimu huu katika Carling cup dhidi ya Leeds United na tangu wkati amekuwa akihusishwa n asana na kikosi cha kwanza.
Fryers amecheza kwa mara ya kwanza katika champions league na premier league kwamara ya kwanza msimu huu pia, ikionekana kwamba Sir Alex Ferguson ana mipango mikubwa na kinda hilo ikiwa atasaini mkataba mpya.
Ingawa alitumia muda mrefu wa msimu uliopita kukaa nje kutokana na majeruhi, alirudi na kucheza baadae katika kikosi kilichochukua ubingwa 2010/11 FA Youth Cup.

Msimu alianza vizuri na kikosi cha reserves na baadae aliitwa katika kikosi cha kwanza . Katika mechi 6 alizocheza ameonyesha uwezo mkubwa katika nafasi zote mbili anazocheza dimbani beki wa kati na wa kushoto.
Ingawa tatizo lake linaweza kuwa uzoefu lakini Fryers anaonekana kuwa composed/kutulia katika ulinzi na kuungana vizuri na walinzi wengine. Kucheza vizuri katika safu ya ulinzi ya United akiwa na miaka 19 tena katika nafasi mbili tofauti , vitu hivyo vinaongea kila kitu kuhusu uwezo wake.
 Anahitaji uzoefu amabo ataupata taratibu akiwa anaendelea kupata nafasi katika kikosi cha kwanza msimu huu katika premier league na hata kwenye Europa league,na hatimaye ikitokea Evra anapumzishwa Fryers anaweza kuchukua nafasi yake.

JORDI ALBA
Jordi Alba alipata nafasi ya kuanza kuichezea timu ya taifa ya Spain mapema msimu huu, na Manchester United watakuwa na busara sana kama watamsajili kinda hilo lenye potential kubwa ya kufanya vizuri kabla ya Barcelona hawajamnyakua.
Alba amekuwa tegemeo la safu ya ulinzi ya Valencia katika misimu mitatu iliyopita akicheza mechi 117, akitoa pasi za mwisho 6 na akichangia upatikanaji wa magoli 8. Alba, 22, tayari ana uzoefu ameshacheza mpaka ligi ya mabingwa wa ulaya na anaonekana ataweza kutoa msaada mkubwa kwa United.
Pia ana uwzo wa kucheza kama winga wa kushoto,Alba ana provides versatility. Ana uwezo wa kuzuia na kushambulia na pia anaweza kucheza kama winga asilia ikitokea kama United watakuwa wana majeruhi wengi kama ambavyo imewakumba msimu huu.
Ikiwa United wataamua kumsajili Alba kama mbadala wa Evra, litakuwa nichaguo sahihi sana kwa kuwa mhispania huyo ana kipaji kikubwa na anafaa kuchukua nafasi ya mfaransa huyo.

EMILIO IZAGUIRRE
Emilio Izaguirre amewahi kusema Manchester United walikuwa wamevutiwa nae kipindi kilichopita cha usajili na Sir Alex Ferguson itabidi kweli aamue kumfuatilia mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu.
Izaguirre alijiunga na Celtic mwezi wa August 2010 na kwa haraka akachukua namba na kujiweka katika listi ya mabeki wazuri wa kushoto katika ligi kuu ya Scotland.
Katika msimu wake wa kwanza, Izaguirre alizawadiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka YA SPFA, Clydesddale Bank SPL Player of Year, mchezaji bora wa mwaka wa wachezaji wa Celtic na mchezaji bora wa chama waandishi wa habari.
Pamoja na kuwa mlinzi mzuri, Izaguirre pia ni hatari mno katika kushambulia.Ana kasi, mwepesi na anajua sana kutoa pasi, huku mara nyingi akiwa anatoa krosi nzuri kutoka wingi ya kushoto. Kwa mtindo huu anafanana sana Evra lakini mara nyingi amekuwa hajisahau kurudi kukaba kama ilivyo kwa mfaransa huyo.
Izaguirre ambaye ameshaichezea timu yake ya taifa ya Hondurus mechi 45, alivunjika enka  mwezi wa nane 2011 na sasa amerudi tena dimbani akijaribu kuitafuta tena fomu yake aliyokuwa nayo.
Kama ataendelea kucheza katika levo aliyokuwa akicheza kabla ya majeruhi, Izaguirre ni chaguo sahihi katika mbio za kumtafuta mrithi wa Evra.

LEIGHTON BAINES
Leighton Baines moja kati ya mabeki wa kushoto wenye uwezo mkubwa kwenye premier league, ni mtu ambaye anafaa zaidi kumrithi Patrice Evra at Manchester United.
Msimu uliopita, Baines alicheza kila dakika ya kila mchezo  wa Everton katika premier league. Alikuwa nab ado ndio mchezaji mwenye thamni sana katika kikosi cha David Moyes. Kwa uwezo wake aliouonyesha in 2010/11, Baines alizawadiwa tuzo ya mchezaji bora wa Everton na mchezaji bora wa wachezaji wa Everton.
Ni mlinzi mzuri sana na anajua pia kushmabulia na kupandisha timu kutokea upande wake wa kushoto. Katika msimu wa 2010/11, Baines alikuwa na assists 11 kwa Everton – idadi kubwa kuliko mlinzi yoyote katika premier league. Pia alifunga magoli saba, huku mkwaju wake dhidi ya Chelsea katika FA Cup ukichagukiwa kuwa goli la mwaka la Everton.
Baines anatakiwa kuwa chaguo la kwanza kumbadili Evra pale Old Trafford. Akiwa na miaka 27, Baines tayari ana uzoefu na ameshathibitisha kuiweza ligi kuu ya England.

No comments:

Post a Comment