Search This Blog

Sunday, March 18, 2012

HATUA TANO KABLA YA BAO LA YANGA DHIDI YA VILLA SQUAD.

Hii ndiyo hatua ya tano la goli la Yanga dhidi ya Villa

 Kipa wa Villa Sguad Daud Mwasongwe akiwa amelala chini akishuhudia namna ambavyo mshambuliaji wa Yanga Pius Kisambare anaondoka na mpira kabla ya kutoa pasi kwa Hamisi Kiiza na kufunga bao la ushindi huku beki wa Villa Gerald Lukindo akishangaa mashabiki jukwaani wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga ilishinda bao 1-0


Hii ndiyo hatua ya nne kabla ya Kiiza kufunga goli dhidi ya Villa

Mshambuliaji wa Yanga Pius Kisambare akichukuwa mpira mgongoni mwa Kipa wa Villa Sguad Daud Mwasongwe baada ya Kipa huyo kuanguka chini kabla ya kumpa Hamisi Kiiza pasi na kufunga bao la ushindi.

Hii ndiyo hatua ya tatu la goli la Yanga dhidi ya Villa

Mpira ukiwa mgongoni mwa Kipa wa Villa Squad huku mshambuliaji wa Yanga Pius Kisambare akijaribu kuuwania kabla ya kumpa  Hamisi Kiiza pasi na kufunga bao.
Hatua ya pili la goli la Yanga dhidi ya Villa

 Mpira ukimponyoka Kipa wa Villa Squad Daud Mwasongwe kichwa ni mwa mshambuliaji wa Yanga Pius Kisambale uku Hamisi Kiiza wa yanga akijiandaa kumsaidia.

Hii ndiyo hatua ya kwanza ya goli la Yanga dhidi ya Villa

Kipa wa Villa Sguad Daud Mwasongwe akidaka mpira kichwani mwa mshambuliaji wa Yanga Pius Kisambare huku Hamisi Kiiza akijiandaa kumsaidia wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 kwa hisani ya http://www.japotz.com/

No comments:

Post a Comment