Search This Blog

Sunday, March 18, 2012

FABRICE MUAMBA AZIDIWA -HALI YAKE NI MBAYA SANA. BOLTON WATHIBITISHA.

Kiungo wa Bolton Fabrice Muamba yupo katika hali mbaya zaidi akipigania maisha yake katika chumba cha ICU, katika kituo cha magonjwa ya moyo ndani ya Hospitali ya Chest, London, klabu yake imethibitisha.
Madaktari wakiwa wanahangaika kuokoa maisha ya

Kiungo huyo mwenye miaka 23 alianguka ghafla katika mechi ya raundi ya sita ya kombe la FA dhidi ya Tottenham  na akapewa huduma ya kuushtua moyo pale pale uwanjani.
Gareth Bale akiwa anamfariji mchezaji mwenzioe Defoe.

Mapema jioni ya leo hii baada ya kuanguka, iliripotiwa kwamba hali yake imeimarika, lakini sasa Bolton wametoa tangazo rasmi.
Huku mechi ikiwa 1-1, mchezaji huyo wa kikiso cha England under 21 alionekana akidondoka na mara moja madaktari wa timu zote mbili waliamua kushirikiana kujaribu kuokoa maisha yake.
Van Der Vaart akiomba dua kwaajili ya Muamba.

Baada ya kutibiwa kwa dakika 6 dimbani Muamba alichukuliwa na machela akiwa amefungwa oxygen na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Kutokana na tukio mechi hiyo iliaghirishwa.
Zilisomwa dua nyingi katika kuhikisha Muamba anarudia afya yake.

1 comment:

  1. Shaffih,
    Nilikuwa nikiangalia ile mechi ya Bolton na Totenham. Lile tukio la kuanguka kwa Fabrice Muamba, nikalihamisha ghafla katika mazingira ya soka la bongo nikaona hakuna ambavyo Fabrice Muamba angeweza hata kufika kwenye Ambulance akiwa bado anapigania maisha yake, nikaona nijinsi gani ambavyo Fabrice angekatikia palepale. Lakini lengo langu sio hilo, lengo langu nikuwaomba muanzishe mjadala wanamna gani tunatoa huduma za kwanza michezoni, nimekuwa nikihudhuria sana viwanjani huko nyumbani utakuta mtu ameaumia watu wahuduma ya kwanza wanakimbia na chupa za maji ya uhai au spray ya kutuliza maumivu (kama timu inajali sana vinginevyo hakuna kitu) kwenda kutoa huduma za kwanza. Mie nafikiri umefika wakati sasa tujifunze nayanayotoke kila leo viwanjani. Mie nafikiri TFF imefika wakati wawe na sheria hata mechi zetu za michangani wanohusika kuziratibu wahakikishe kunakuwa na uhakika wa huduma ya kwanza iliyobora hii ndio iwe pre-requisite kama hakuna hiyo basi hakuna mechi, unakuta mtu ameanguka watu wanampepea tu! Kama Fabrice jana angeishia kupepewa asingefika leo.Tujitahidi hata tuwe na mitungi midogo ya oxygen kwa watoa huduma ya kwanza. Ile gari ya wagonjwa "Ambulance iwe full equiped sio iwe na kin'gora tu halafu ndani hamna kitu"
    Hii iwe ni changamoto.

    ReplyDelete