Search This Blog

Sunday, February 12, 2012

WAPENZI WA YANGA IUNGENI MKONO TIMU YENU KWENYE MCHEZO DHIDI YA ZAMALEK.





Zimebakia siku kadhaa huku nyingi zikiwa zimeshapita kuelekea mchezo wa kihistoria kwa
klabu ya Dar es salaam Young Africans dhidi ya Zamalek Sc toka Misri. Yanga ambao masaa 24 yaliyopita wamesherehekea miaka 77 ya kuzaliwa kwake .


Kwa kawaida klabu za nchi za magharibi kama vile ulaya , Marekani ya kusini na hata za
hapa Afrika kwetu kama afrika kusini na misri wanakotoka za Zamalek zina utaratibu wa
kusherehekea miaka Fulani ya kuzaliwa au kuanzishwa kwa vilabu vya kwa staili ya aina
yake. 


Utakuta maandalizi yanafanywa kwa kutengeneza kumbukumbu za kudumu kwa muda
mrefu na si vitru vya kupita . Mfano mzuri ni Man United ambao misimu michache iliyopita
walitengeneza jezi maalum za kumbukumbu ya ubingwa wake wa kwanza wa ulaya uliopatikana mwaka 1968 kwa kuifunga Benfica ya Ureno. 


Arsenal nao waliwahi kutengeneza jezi maalum za kuadhimisha miaka 100 ya uwanja wa Highbury na nyingine nyingi huwa zina utaratibu kama huo , Yanga nao wangeweza kutengeneza japo jezi ambazo zingekuwa zimeandikwa miaka 77 kwenye nembo yake . 


Hawajachelewa kufanya hivyo na zawadi pekee kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga katika kipindi hiki ambcho shamrashamra za maadhimisho ya miaka 77 ya kuanzishwa kwa Yanga bado mbichio itakuwa matokeo mazuri kama si ushindi katika mchezo dhidi ya Zamalek.


Historia haimpi hamasa mwanajangwani yoyote Yule kuwa na matumaini na mchezo wa
mwishoni mwa wiki ijayo lakini historia hizi hizi zimewekwa ili zivunjwe na watu wanaoandika makala kama hii hapa wapo kwa ajili ya kuwakumbusha watu wote kuwa mwaka Fulani historia Fulani iliwekwa na mwaka Fulani historia hii ilivunjwa na mtu Fulani.


Yanga wamekuwa na muda wa kutosha kujiandaa kwa mchezo huu hivyo hakuna anayetegemea kusikia sababu za hakukuwa na muda wa kufanya maandalizi ya kutosha .


Pamoja na hayo Yanga wamekuwa wakionyesha mchezo mzuri kwenye michezo ya ligi ambapo wameweza kupata ushindi katika michezo miwili mfululizo baada ya kuwa wameanza raundi ya pili vibaya kwa sare na Moro United . Kuitumia ‘perfomance’ ya Yanga kwenye ligi ya Vodacom kama kipimo cha jinsi watakavyocheza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zamalek inaweza kuwa sio sahihi lakini matokeo mazuri yanawajengea wachezaji hali ya kujiamini jambo ambalo ni muhimu kwa mchezaji yoyote kuelekea kwenye mchezo mkubwa na hali hii itakuwa hivi hivi kwa Yanga ambao washambuliaji wao kina Hamis Kiiza na Kenetth Asamoah watakuwa wanajiamini vyema kutokana na hali nzuri waliyo nayo kuelekea kwenye mchezo huo.


Moja ya mambo ambayo yanaweza kuisaidia Yanga kufanya yale yasiyotarajiwa na wengi hasa kwenye mchezo dhidi ya Zamalek ni kuungwa mkono na mashabi na wapenzi wake
watakaojitokeza uwanjani siku ambapo wanajangwani watakuwa wanashuka dimbani kuwavaa waarabu. 


Kwa kawaida mashabiki wa soka la Tanzania wamekuwa na ‘negative mindset’ au kwa lugha rahisi ‘mawazo hasi’ kuzihusu timu za nyumbani kaka timu za taifa na klabu za Simba na Yanga.


 Kiukweli mazingira ya soka la ‘bongo’ hayamfanyi mtu awe na moyo kama alio nao shabiki wa Liverpool kwa timu yake lakini kila mtu anapaswa kuipenda timu yake anayoishabikia na kuwa tayari kuiunga mkono pale inapomhitaji pasipo kujali yale yanayotokea nyuma ya pazia .


Na hii inawahusu mashabiki wote wa Yanga na hata ikiwezekana wa timu pinzani kwao ya Simba kwani ikifanikiwa Yanga hata Simba imefanikiwa kwani wote kwa pamoja wanapeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la soka la kimataifa.


Umuhimu wa mtu ambaye kwa soka amekuwa akifahamika kama mchezaji wa 12 ni wa kipekee na michuano ya kombe la mataifa ya Afrika iliyomalizika huko Gabon na Equatorial Guinea jana imeonyesha hilo. 


Pasipo kutarajiwa na mtu timu kama Equatorial Guinea ambayo iliingia kwenye michuano ikiwa ya mwisho kwenye viwango vya ubora vya CAF na vya FIFA iliweza kufika robo fainali ikitandaza soka safi na kuzifunga timu ngumu kama Senegal na Libya , si wengi wangetarajia haya toka kwa timu hii lakini ukachilia mbali yale yaliyokuwa yanaendelea uwanjani mashabiki walikuwa na mchango mkubwa kuwafanikishia yale waliyoweza kuyatimiza na sioni kwanini hili lisiwe soma kwetu watanzania. 


Mashabiki wa Yanga wakipiga kelele tangu mwanzo hadi mwisho wa mchezo wachezaji uwanjani watapata nguvu ya kuamini kuwa wanaweza kutimiza yale waliyoagizwa na mashabiki maelfu waliofika uwanjani na hata wale ambao wameshindwa kupata nafasi ya kwenda uwanjani .


Kwenye mchezo wa marudiano kati ya Yanga na Zamalek utakaofanyika kule mjini Cairo ndio mashabiki wa Yanga watashuhudia ukweli wa haya yanayozungumzwa hapa kwani waarabu wanaiunga mkono timu yao mwanzo mwisho na mapenzi wanayoyaonyesha kwa mashujaa wao wanaopambana uwanjani ndio yanayowachagiza wachezaji 11 kufanya vizuri hivyo ni vyema mashabiki wa Yanga wakaanza kwa kuipa sapoti timu yao huku wakijua kuwa Yanga watakutana na hali tofauti mjini Cairo.


Kila mtu anaelewa kuwa huu ni mlima mrefu sana kwa Yanga kuupanda lakini penye nia pana njia na wachezaji na viongozi wa Yanga wameonyesha nia kwa kuiweka timu kwenye mazingira mazuri kwa upande wa viongozi na wachezaji wameonyesha matumaini kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakicheza kwenye michezo ya hivi karibuni , Mungu Ibariki Yanga , Mungu ibariki

No comments:

Post a Comment