Search This Blog

Friday, February 10, 2012

Kaseja: Tutawafuta machozi kwa Azam

NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja, amesema wachezaji watawafuta machozi washabiki kwenye mechi dhidi ya Azam Jumapili ijayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaseja alisema wachezaji wa Simba wanajua maumivu waliyonayo washabiki mara baada ya kupoteza mechi dhidi ya Villa Squad na ndiyo maana wanataka kurekebisha mambo.
Jumamosi iliyopita, Simba ilifungwa na Villa bao 1-0 katika pambano lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini, matokeo ambayo yaliwauma washabiki wengi ikizingatiwa kuwa timu hiyo ndiyo inayoshika mkia kwenye ligi.
“Soka ni mchezo wa ajabu sana. Kuna kipindi kunakuwa na matokeo ambayo hakuna anayeyategemea. Ila mimi ni muumini wa dini na ninaamini kuwa kuna wakati Mungu naye anakuwa na mipango yake. Alipangalo Mungu haliepukiki,” alisema.
Hata hivyo, Kaseja alisema ana imani washabiki watasahau kuhusu mchezo wa Villa iwapo Simba itaibuka mshindi katika pambano gumu dhidi ya Azam Jumapili ijayo.
Alisema ndiyo maana sasa wachezaji wote wa Simba wameleekeza nguvu zao zote katika pambano hilo wakifahamu fika kuwa matokeo ya mchezo huo yakiwa mazuri, Simba itatulia.

2 comments:

  1. matokeo ngapi ngapi kati ya hao mapuga wawili

    ReplyDelete
  2. Simba kashinda 2-0 magoli yote Okwi,umenipata mkuu wa Mapuga hao wawili?

    ReplyDelete