Search This Blog

Friday, February 10, 2012

ERIC ODHIAMBO: MTANZANIA PEKEE KUCHEZA LIGI KUU SCOTLAND





MSHAMBULIAJI  chipikuzi mwenye asili ya Tanzania, Eric Geno Sije Odhiambo, anaweza kuwa na mchango mkubwa kwa timu yake ya Inversness Caledonian Thistle ya Scotland. Eric ambaye alijiunga na timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya saba katika ligi kuu ya Scotland mwaka 2009, amekwishacheza michezo 55 na ameifungia mabao 7. Hiyo imempelekea kuwa mchezaji kipenzi cha kocha wake Muingereza Terry Butcher.


Kijana huyu aliyezaliwa katika jiji la Oxford huko England, ni mwenyeji wa Mkoa wa Mara kiasili; na miaka michache iliyopita alikuja nchini kumzika baba yake Mzee Sije Odhiamo pamoja na nduguze ambao pia ni wanasoka wa kulipwa nchini England.






Eric ametokea kuwa mshambuliaji wa kutegemewa wa Inversness Thistle baada ya kupata 'msoto' katika vilabu vya Leicester City ambako ndiko alipoanzia katika academy yao. Alikuwa katika kikosi cha Leicester City kuanzia mwaka 2006-2009 lakini alikuwa akipelekwa kwa mkopo katika timu za Southend United ambako alicheza mechi 5 na hakufunga bao lolote. Hiyo ilikuwa mwaka 2007. Mwaka 2008 alipelekwa kwa mkopo katika timu ya Dundee United inayocheza ligi kuu ya Scotland na alicheza mechi nne tu, kabla ya mwaka huo huo kupekwa kwa mkopo Brentford.


Timu ya Inversness Thistle, imeanzishwa mwaka 1994 miaka minne baada ya Eric kuzaliwa. Eric huvaa jezi namba saba katika kikosi cha timu hiyo na ametokea kuwavutia wengi kutokana na kipaji chake cha kufunga mabao.

Kwasasa Eric amejiunga na klabu ya Denizlispor inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uturuki.

3 comments:

  1. shaffi acha sound,michezo 55 goli 7 then awe mshambuliaji wa kutegemewa? otherwise toa justification zingine sio magoli na mechi
    chela wa dom

    ReplyDelete
  2. Shafii vp kuhusu huyu dogo kuchezea Stars, umesema ana asili ya Tanzania lakini je sasa hivi ni raia wa nchi gani?
    Brother hapo juu, kuhusu kuwa mshambuliaji wa kutumainiwa sio issue sanam maana muhimu ni ile pressure anayotoa uwanjani, je we huoni Kina Torres na Carrol?

    ReplyDelete
  3. Presha uwanjan ss ndo 2naangalia co wenze2 wanaangalia unauwezo gan wakcheza na izo nyavu kaka

    ReplyDelete