Search This Blog

Sunday, February 5, 2012

CHELSEA VS MAN UNITED: ANTONIO VALENCIA MCHEZAJI MWENYE FUNGUO YA USHINDI WA UNITED DHIDI YA CHELSEA



Manchester United wanakutana na Chelsea leo hii katika mchezo ambao unaweza ukawa moja ya ficture muhimu sana za msimu huu. United waliwafikia City kileleni katikati mwa wiki hii, hivyo watahitaji kuendelea na performance nzuri kama wanataka kujisogeza wenyewe kileleni katika nafasi ya kwanza.

Wakienda kwenye mechi, Chelsea itakuwa bila wachezaji weake muhimu wawili. Ashley Cole ana adhabu kutokana na kadi mbili za njano alizopata katika mchezo dhidi ya Swansea, na John Terry atakuwa nje kwa majeraha ya goti. Kwa hakika huu ni muda muafaka kwa United kuwaadhibu tena Chelsea.

Ama kwa hakika ukimtaja mchezaji ambaye yupo katika form nzuri kwa United msimu huu lazima atakuwa Antonio Valencia, na mechi hii dhidi ya Chelsea itakuwa nafasi kubwa kwake kuitawalana kujivalisha taji la Winga bora wa United msimu huu. Huku Ashley Cole nje, Valencia ana uwezekano mkubwa wa kucheza dhidi ya aidha bwana mdogo Ryan Bertrand au Jose Bosingwa aliye nje ya form, kati ya hawa wote wawili simuoni wa kumkabili in-form Valencia.

Ukweli ni kwamba wakati mashabiki wengi wakisema Micheal Carrick ndio the most underrated player katika kikosi cha United, mtu angestahili title hii ni Valencia  mpaka wiki chache zilizopita. Katika miezi michache iliyopita Valencia amethibitisha kwamba yeye ni moja ya wachezaji muhimu sana  katika United squad.

Wakati Nani akibaki kama mchezaji mwenye kipaji binafsi zaidi katika klabu, consistency ya Valencia ni balaa. Katika mechi 11 alizoanza za EPL msimu huu amefunga magoli mawili na kutoa assists 9.

Naweza hata nikasema kwa sasa Valencia ndio winga wa kulia mzuri kuliko wote katika premier league. Rivals wake wa karibu wanaweza kuwa Theo Walcott au Aaron Lennon, ambao kati yao hakuna aliyeonyesha mambo ya kutisha kama alivyofanya “Tony V” katika wiki chache zilizopita.

Wakati udhaifu dhahiri wa Valencia ni kushindwa kucheza na mguu wa kushoto, lakini hili jambo bado halijaonekana kuwa kikwazo kikubwa kipindi cha mechi kwani mara nyingi huwa anafanikiwa  kuurudisha mpira katika upande wake wa kulia na kutoa krosi nzuri na zenye madhara katika lango la adui.

Kwanini naamini Valencia atakuwa mwamuzi mkubwa wa mchezo huu? Well, kama nilivyosema mwanzoni watu watakaopewa jukumu la kumkaba ni aidha bwana mdogo ambaye hana uzoefu Ryan Bertrand au Bosingwa. La muhimu zaidi, uwezo wake wa kutoa pasi za mwisho na kumtoa mchezaji wa upinzani nje ya box utaendelea kuwa tishio kwa ukuta wa Chelsea uliodhaifu tena wakiwa wanamkosa Terry.

Huku mtu ambaye amekuwa akifanya makosa kila kukicha David Luiz akitegemewa kuanza pamoja na Gary Cahill, uwezo wa Valencia unaweza ukazua balaa katika final third ya Chelsea. Krosi za Valencia ni hatari zaidi, na kuwa-pair Luiz na Cahill linaweza kuwa tatizo jingine la kushughulika nalo.

Huku Young akiwa anarudi kutoka katika majeruhi, inabidi ushangae ni vipi ataweza kurudisha namba yake kwa form hii aliyonayo “Tony V”. Valencia ni mchezaji ambaye kwa sasa ni muhimu zaidi katika kikosi cha United, na ataendela kuwa hivyo katika mchezo dhidi ya Chelsea leo Jumapili. Tegemea magoli.
NAWASILISHA.

5 comments:

  1. Wewe ni nani wakutuambia kuwa Valencia hakuna mtu wa kumkaba......kwani yeye ni nani...huu ni mpira bwana.
    Mdau
    Washington

    ReplyDelete
  2. kiukweli tony v ndiye key maker wa united jamaa hashuki kiwango kibaya kwake akich

    ReplyDelete
  3. Yani uko sahihi kabisa,unachokisema wewe namimi ndo ninachokiona katika timu zote mbili!

    ReplyDelete
  4. Kiukweli mimi ni shabikiki wa La Liga,ila kwa EPL,nipo ila sio kivile lakini mechi hii ya Leo Kati ya Red Devils na The Blues,hapana shaka karata yangu naipeleka kwa wazee wa Stanford Bridge,hawa Mafaza acha., wakiwa kwao aisee mtu hatoki. Tukija kiufundi utaona kama Man U ni wazuri kwenye Midfielders na Left wing,ila nao Chelsea ni wako Fit kwa upande wa Defence,japo Terry ndo hivo hatokuwepo.
    So sidhani kama Luis Nani,au Valencia watapita kirahisi pale.
    Mwisho naweza kutabiri japo mie sio Sheikh Yahya.
    Chelsea 2-1 Man U
    magoli yote yatafungwa kipindi cha pili.
    Ni hayo tu Shaffih.

    ReplyDelete
  5. Shafii hiyo me naona ni mawazo yako, ni kweli valencia n bora kuliko walcot?,angalia magori 22 aliyofunga van magori(RVP), je Walcot ametoa assist ngapi?.Mechi ya leo kwa maoni yangu Torres atafufuka but pia akipangwa bekimbadala wa cole atamdhibiti vizuri valencia coz atakuwa hamjui. CHELSE ATASHINDA PALE DARAJANI.

    ReplyDelete