Search This Blog

Sunday, February 5, 2012

CHELESA VS MAN UNITED: MAMBO MANNE YA KIUFUNDI AMBAYO VILLAS-BOAS AKIFANYA YATAINUFAISHA CHELSEA DHIDI YA UNITED



Hapo zamani kidogo Chelsea waliweka rekodi ya kutofungwa katika mechi 86 walizocheza katika uwanja wao wa Stamford Bridge.
Ingawa sasa mambo ni tofauti, vipigo vya hivi karibuni dhidi ya Aston Villa, Liverpool na Arsenal vimebadili mtazamo wa kiwanja hicho maarufu kama darajani “Darajani”.
Hiki ni kitu ambacho Sir Alex Ferguson wa Manchester United atakitumia katika mchezo wa jumapili kwa sababu timu yake ina rekdi nzuri ya ugenini kuliko timu zote katika ligi msimu huu.
Haya mambo manne ya kiufundi ambayo Villas-Boas anapaswa kufanya ili kuweza kuwakalisha United darajani.


RYAN BERTRAND AANZE BADALA YA BOSINGWA KATIKA NAFASI YA BEKI WA KUSHOTO.
Ashley Cole amekuwa akicheza chini ya kiwango mno msimu huu, lakini amekuwa akicheza kila siku kwa kuwa hakuna mbadala anayeweza kushindania nae namba.
Lakini sasa, Cole akiwa amesimamishwa, Andre Villas-Boas amepewa nafasi ya kukaa na kufikiri vizuri.
Nani aanze upande wa beki wa kushoto?
Kuna washindani wawili: Jose Bosingwa na Ryan Bertrand.
Vilaas-Boas ansingekuwa na wakati mgumu kama angelijumlisha jina Bertrand katika kikosi cha champions league. Kama angefanya hivyo, Bertrand angeanza dhidi ya Bayer Leverkusen, mchezo ambao Ashley Cole aliukosa kutokana na maumivu ya enka.
Badala yake, Villas-Boas alilazimika kuidhoofisha timu yake kwa kuamua kumuanzisha Bosingwa katika upande wa kushoto, jambo lilopelekea Gonzalo Castro kumtawala beki huyo wa kireno ambaye yupo nje ya form.

Sidhani kama ni jambo la sahihi kwa Bosingwa kuanza katika mechi dhidi ya United  kwa naamini atakuwa anakimbiza kivuli cha mtu ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa moyo wa United dimbani Luis Antonio Valencia.

Pia kumtumia Bertrand in the deep end, manager wa Chelsea atapata majibu kwamba Bertrand ni mtu sahihi kumrithi Cole ndani ya kikosi cha Chelsea.

 LUKAKU APEWE MUDA WA KUCHEZA ZAIDI
Andre Villas Boas hakuwahi kumuhitaji Romelu Lukakau, kama ambavyo hakuwa akitaka kumsaini Kevin De Bruyne, na matokeo yake Portuguese manager ameiharibu confidence ya Lukaku, ambaye bado hajapewa nafasi zaidi.

Kwa wale ambao mnasema. “Oh bado hayupo tayari” – Kweli?
Akiwa na miaka 17, tayari ameshafunga magoli 39 na kutoa assists 14 katika michezo rasmi 95.

Nini walikuwa wanafanya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo walipokuwa na miaka 17? Walikuwa ndio kwanza wanaonja ladha ya soka la kulipwa.

Lukaku ni mtoto aliyepevuka kikubwa zaidi na inakatisha tama kuona Villas-Boas ameshindwa kukiendeleza kipaji cha  mtoto huyu mwenye nguvu kama watu wazima.

Kuliko kumpa sub Paulo Ferreira, Villas-Boas anahitaji kumpa Lukaku muda zaidi kiwanjani kutoka atleast dakika 20-30, ikiwa Fernando Torres ataendlea kuzingua dhidi ya United.

3: JONNY EVANS
Nini ni udhaifu wa Jonny Evans? Tackling, kwa sababu ana maamuzi mabovu.

Mifano hai ni kama tackle aliyoifanya dhidi ya Stuart Holden, kumfanya Oscar Coldozo wa Benfica kuonekana kama hatari zaidi ya uwezo wake na kubwa zaidi alivyomvuta Mario Balotelli.
Hii ndio sababu kubwa inabidi Villas-Boas inabidi ampange Juan Mata katikati, kwa kuwa mhispania huyu na uwezo wake utamfanya Evans acheze ovyo na kusababisha madhara kwa United.
Evans ana wastani mzuri wa kupiga pasi, ana asilimia 89.7. hivyo ni mmoja kati centre backs walio salama zaidi duniani linapokuja suala la kusambaza mipira.

Villas-Boas anapaswa kumlazimisha Torres kumpa presha Evans kipindi beki huyo wa United anapokuwa na mpira.
Kwa kufanya hivyo, itamfanya Evans akose kujiamini na kushindwa kupiga pasi vizuri hivyo kufanya makosa ambayo yatainufaisha Chelsea.

4: KUPIGA MASHUTI YA MBALI IKIWA DE GEA ATAKAA LANGONI.

Huku Anders Lindegaard akiwa nje, David De Gea lazima atakuwa ni no.1, lakini hayupo katika form.

Chelsea watajidhoofisha wenyewe kwa kumuanzisha David Luiz na labda Jose Bosingwa, hivyo hata Manchester United watafanya hivyo kwa kumuanzisha De Gea katika milingoti mitatu.
Ni jambo la kushangaza kuona United walimnunua De Gea huku akiwa na matatizo ya macho.

Na ndio maana haishangazi kuona yeye ndiye aliekuwa golikipa aliyefungwa zaidi kwa mashuti ya mbali katika msiimu wa 2010-11 wa la liga. Hivyo Chelsea wanachotakiwa kufanya ni kupiga mashuti ya mbali kila wanapopata nafasi na hali hiyo itaongeza  presha kwa De Gea na mwishoanaweza kufanya makosa ambayo yatainufaisha Chelsea.

No comments:

Post a Comment