Search This Blog

Sunday, December 25, 2011

Yanga Tabata kukutana Boxing Day


WANACHAMA wa klabu ya Yanga tawi la Tabata wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa mwaka utakaofanyika kesho Jumatatu (26 Desemba, 2011) kwenye Ukumbi wa Afisa Mtendaji Kata huku ajenda kubwa ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa tawi hilo, Michael Warioba alisema, wanachama wa tawi hilo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mkutano huo utakaoudhuriwa na vingozi wa kitaifa wa timu hiyo.

“Vitu vingi tutavizungumzia kama vilivyoorodheshwa katika ajenda zetu, lakini kubwa ni maandalizi ya timu katika mzunguko wa pili wa ligi kuu, pia mchezo wetu na Zamalekh (Kombe la Shirikisho Afrika).

“Tunaomba wanachama wajitokeze kwa wingi saa 4:00 asubuhi katika mkutano huo ili tuweze kuijenga klabu yetu na kutetea ubingwa wa Bara,” alisema Warioba.

Pia Warioba amewataka wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza kuchukua kadi za uanachama wa Yanga ili waweze kupata nafasi ya kutoa mchango wa hali na mali katika kuhakikisha timu inafanya vizuri kwenye michuano mbalimbali.

1 comment:

  1. Mnakutana kuzungumzia mzunguko wa pili wa ligi pamoja na mchezo wenu thidi ya Zamaleki ya misri na mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa Yanga Afrika, Yanga umoja wa mataifa. Hivi ndugu yangu unayeitisha huo mkutano unaelewa kwamba timu ina wiki nzima haijafanya mazoezi, wachezaji wana miezi 2 hawajalipwa mishahara yao, kocha anaishi nyumba maji,umeme vimekatwa kisa klabu imeshindwa kulipa bili, nafikiri mkutano huu unakuja na unaonyesha jinsi viongozi wetu wasivyo na habari wewe unaitisha mkutano wa namna hiyo wakati maslahi ya wachezaji na kocha havipatikani. Sioni tija ya huo mkutano ni kupoteza muda.

    ReplyDelete