Search This Blog

Wednesday, December 14, 2011

SPURS NAO WAPO TAYARI KULIPA £20MILLION.


Boss wa Tottenham Harry Redknapp amesema timu yake ipo tayari kumsajili Carlos Tevez kutoka Manchester City kwa ada ya £20million.

The tittle-chasing Londoners wanajipanga kukiongezea nguvu kikosi chao ambacho ndio kimefunga magoli machache kuliko timu yoyote kwenye EPL Top 5.

Katika kuonyesha wapo serious na kuhitaji huduma za Tevez, Spurs tayari wameshaongea na maofisa kutoka Etihad Stadium juu ya uhamisho wa £20million kwa ajili Muargentina Carlitos.

Chanzo cha habari kutoka White Hart Lane kilisema: “Spurs wapo serious juu ya kuhitaji huduma za Tevez, kikwazo pekee kitakuwa ni kama City watakuwa tayari kufanya biashara na moja ya timu ambazo ni wapinzani wao wakuu katika kugombea ubngwa.”

Mshahara wa Tevez pia ni kikwazo lakini Spurs wapo tayari kulipa mshahara huo wakiamini kumpata Tevez ni investment nzuri itakayolipa vizuri.

AC Milan pia wanamtaka Tevez lakini kwa mkopo na makamu wa Raisi wao Adriano Galliani alisema: “Tunajua tayari tuna makubaliano binafsi lakini tunatumai hatokubaliana na klabu nyingine,”

No comments:

Post a Comment