Search This Blog

Wednesday, December 14, 2011

IVI GERVINHO NA KR MULLA HAWANA MAHUSIANO ?

Waswahili wasema duniani wawili wawili , kila mtu lazima anafanana na mtu fulani ambaye anafahamiana naye au asiyefahamiana naye , kuna wengine hufanana kiasi cha mtu kudhani wana undugu fulani wa karibu mathalani wamezaliwa pamoja , umewahi kumtazama kwa karibu Winga wa Arsenal ya England anayetokea Ivory Coast Gervinho na mwanahiphop toka kundi la wanaume halisi KR Mulla , Jibaba mziki CD 700 kama anavyojiita . Hawa jamaa wamefanana balaa , utadhani wamezaliwa pamoja , sasa cha kujiuliza ni je KR ndio kaibia toka Ivory Coast hadi Bongo au Gervinho ndio kaibia toka Bongo hadi Ivory Coast, Swali gumu kujibu lakini itabidi tumhoji vizuri KR na mshua wake watuambie kunani pale kati au Mungu akijalia tukwae pipa hadi Ivory Coast halafu tukwee lingine hadi London tumhoji Gervinho juu ya ukweli wa suala hili.




























HAPA NIKIWA NA ' GERVINHO '











2 comments:

  1. acha masiharaa shaffih,ukiwa na gervinho ? huyo si KR Mula huyo

    ReplyDelete
  2. aah kaka huyo KR bwana,ila uwezi juwa bwana wazee wa zamani walikuwa wanapelekwa utumwanilabda mzee wake KR alikuwa everycost......

    ReplyDelete