Search This Blog

Thursday, December 29, 2011

RAMBIRAMBI MSIBA WA RASHID MOYO






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa, Rashid Moyo kilichotokea usiku wa Desemba 25 mwaka huu kwao Msambweni, Tanga.
Moyo ambaye aliichezea timu ya Taifa kwenye miaka ya 70 alizikwa Desemba 26 mwaka huu kwenye makaburi ya Mabawa mkoani Tanga. Pia alikuwa mchezaji wa timu ya Coastal Union ya mkoa wa Tanga.
Msiba huo ni pigo kwa familia ya Moyo, TFF na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana na mchango alioutoa kwa Tanzania hasa wakati akiwa mchezaji. TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Moyo, Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA) na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 100,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke roho ya marehemu Rashid Moyo mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment