Search This Blog

Thursday, December 29, 2011

KWANINI BERBATOV HAPASWI KUONDOKA UNITED JANUARY?


Performance ya Dimitar Berbatov dhidi ya Wigan na Fulham could be described as “come and get me” plea kwa timu yeyote inyomtaka, lakini Je Fergie atakuwa radhi kumuacha mbulgaria huyo aliyemnunua kwa fedha nyingi aondoke Old Trafford?

Tangu kipindi kilichopita cha usajili kilipofungwa, kumekuwepo na vilabu vingi vilivyohusishwa na kumsaini Berba, zikiwemo Paris Saint Germain, Valencia, Fulham, Galatasary, and Anzhi Makhachkala. Ingawa hivi taarifa zimetoka kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kurejea katika klabu yake ya zamani, Bayern Leverkusen.

Mkataba wa Berbatov unamalizika mwishoni mwa msimu, hivyo United wanapaswa kufanya maamuzi juu ya kumuongezea mkataba mpya kabla ya January 2, vinginevyo Mbulgaria huyo anaweza kukubaliana na klabu yoyote kwa ajili ya kujiunga nayo atakapomaliza mkataba wake next summer.

Huku wengi wakisema Berba anataka timu ambayo atapata nafasi kikosi cha kwanza, manager Sir Alex Ferguson amewahi kukaririwa akisema Berbatov bado yupo katika mipango yake, “Unahitaji kuwa washambuliaji wengi wazuri ndani ya kikosi katika mpira wa siku hizi. Kama utaangalia nyuma in 1999, tulikuwa na washambuliaji wazuri wane. Wote waliplay part zao, na hilo ndilo litakalotokea sasa.” –Fergie

Wakati Rooney, Berbatov, Chicharito and Welbeck wakiwa hawana chemistry kama waliyokuwa nayo Cole, Yorke, Sheringham na Solskjaer unaweza kujua nini Ferguson anamaanisha nini.

Msimu uliopita Berbatov alishinda tuzo ya ufungaji bora ingawa hakuwahi kuwa chaguo la kwanza kabisa katika kikosi cha kwanza. Alifunga mabao 20 katika mechi 32, including hat-tricks dhidi ya Birmigham na mahasimu Liverpool, and ofcourse his magnificent 5 goals dhidi ya Blackburn katika ushindi wa 7-1 @Old Trafford.

Moja ya vitu vizuri kuhusu Berbatov as a person as well as a player ni tabia yake anayoionyesha kwa manager na klabu kwa ujumla. Pamoja na kutochezeshwa katika michezo mingi, Berba hajawahi kutoka nje na kuzungumza kwenye media kwa kutoheshimu maamuzi ya kocha wake. Halazimishi kwamba anataka kuanza katika kila mechi, tabia yake nzuri ndani na nje ya uwanja tofauti na wachezaji wengine wa EPL.

Kitu anachofanya ni ku-prove uwezo wake kiwanjani. Following his hat trick dhidi ya Wigan, hatolazimisha kuanza au ku-suggest kwamba yeye ni mzuri zaidi ya Rooney, Chicharito na Welbeck. Kitu atakachofanya ni kutulia na kusubiri muda na nafasi yake nyingine, and then atathibitisha ubora wake kwa vitendo.

Kila kocha anataka mchezaji wa namna hii, mchezaji/wachezaji ambao wataheshimu maamuzi yao na kutolalamika kuhusu maamuzi hayo ila pale wanapopata nafasi wanazipokea kwa mikono miwili. I have nothing but admiration kwa wachezaji wenye tabia kama ya Berbatov, ambao huweka maslahi ya timu mbele ya matamanio yao.

Je Berbatov ataendelea kuichezea United baada ya tarehe 31, January? Naamini ataendelea kuwepo THEATRE OF DREAMS.

5 comments:

  1. Hi
    Nimeupenda sana uchambuzi huo ulioufanya kuhusu Berbatov kwa kweli hakuna la kuongeya natamani angepata nafasi ya kuusoma pia.
    I appreciate.
    Mike

    ReplyDelete
  2. yap uchambuz umesimama,thumb up berba

    ReplyDelete
  3. Uchambuzi mzuri Shafih hata mi nadhani aendelee kuwepo OT.

    ReplyDelete
  4. Uchambuzi mzuri na hizo sifa kweli ni za berb ila tatizo cc washabiki wa Man U tunataka atumie kila nafac anayopata ndiyo maana huwa tunamlaumu sana anapokosa magoli yanayoitwa ya 'wazi'. Ila kwa uwezo Berb yuko juu mno.

    ReplyDelete
  5. Yap yap huyo ndio Baba Magoli, hat -trick nyingine inakuja kesho. Respect Him Bulgari Goal Machine

    ReplyDelete