Search This Blog

Monday, November 14, 2011

ULIKUWA MCHEZO WA KIRAFIKI, LAKINI SASA NI DHAHIRI SPAIN WANAHITAJI "PLAN B" ILI KUENDELEZA UTAWALA WAO KWENYE SOKA.


Timu ya taifa ya Hispania ni ndio timu inayocheza mchezo mzuri kuliko timu ulimwengu kwa sasa. Hata waanzalishi wa mpira wa miguu wakicheza katika dimba lao la nyumbani Wembley, walijikuta wakicheza ndani ya nusu yao ya uwanja ili kujihakikishia japo nafasi finyu ya kupata matokeo chanya dhidi ya vijana wa Vicente Del Bosque. “Ilikuwa ndio njia pekee ya kushindana nao,” alisema kocha Fabio Capello.

Alikuwa sahihi kabisa.

Spain waliutawala mchezo sana na walitengeneza nafasi na kufanya mashambulizi mengi katika mchezo wao dhidi ya England. Kitu pekee kilichokosekana kwa upande wao, ni goli.

England nao walikuwa na bahati baada ya Davidi Villa kugongesha mwamba, Cesc Fabregas nae alipiga shuti ambalo lilitoka nje kidogo ya goli katika dakika ya mwisho, hizi ni baadhi ya nafasi nyingi Spain walizopoteza. Ndio, Spain walistahili kushinda, lakini tatizo ni nini?

NOT-SO-FRIENDLY MATCHES | Spain's defeats since winning the World Cup

RivalPlayed in
Date
Result
Argentina
Buenos Aires07/09/2010Lost 4-1
Portugal
Lisbon17/11/2010Lost 4-0
Italy
Bari
10/08/2011Lost 2-1
England
London12/11/2011Lost 1-0

Rekodi za hivi karibuni za Spain katika mechi za kirafiki zinaonyesha hali ni mbaya sana kwa vijana wa Del Bosque. Tangu washinde World Cup, ‘La Roja’ wamekuwa na matokeo mabaya katika mechi zisizo za mashindano. Vicente Del Bosque’s men walihangaika kupata droo na Mexico, kabla ya kufungwa 4-1 na Argentina mjini Buenos Aires na baadae kutandikwa 4-0 na Ureno.

Pengine walijitahidi kushinda 4-0 dhidi ya Marekani na 3-0 dhidi ya Venezuela lakini ilikuwa wakicheza na timu ambazo ni dhaifu kwa upande wao, lakini wakicheza dhidi ya wapinzani wa levo zao wanakuwa wana-struggle sana, hasa wakiwa timu inayocheza mchezo wa kuzuia zadi.

Hali hii ilionekana zaidi katika World Cup katika mchezo wa kwanza wa dhidi ya Switzerland ambao walifungwa, kabla ya kuwafunga Portugal, Paraguay, Germany na kumaliza kwa Uholanzi katika mechi ngumu ambayo iliamuliwa kwa ushindi wa goli moja tu. Spain walistahili kushinda mechi hizi, lakini walipata shida, na bahati inaweza isiwe upande wao kama ilivyokuwa jumamosi iliyopita @ Wembley.

Muda huu , wakiwa wanaonekana kama timu bora ulimwenguni, Spain wanaonekana kujua kucheza aina moja tu ya mchezo, ambayo mara nyingi imekuwa ikiwapa matokeo mazuri, lakini mbinu mbadala zinahitajika ili kujihakikishia ushindi katika mechi ngumu. Ndio maana Del Bosque ni mpenzi mkubwa wa mchezaji wa Athletic Bilbao Fernando Llorente, ni sababu mojawapo kwanini bado ana imani kubwa na uvumilivu kwa mchezaji wa Chelsea Fernando Torres: wanatoa mchango tofauti timu inapokabiliana na wapinzani wagumu. Pia Fabregas akicheza kama namba tisa wa uongo, huku David aki-operate kama Lionel Messi na Del Bosque anaweza kuunda ukuta wa watu watatu dhidi ya timu isiyoshambulia sana, kama ambavyo Barcelona wamekuwa msimu huu.

Japokuwa mafanikio ya Euro na World Cup, Spain ni hatari wanapokuwa wametanguliwa kufungwa. Comebacks dhidi ya Chile na Czech Republic zilithibitisha wanaweza, lakini michezo yote miwili walitegemea kushinda, Anyway. Kutanguliwa kufungwa na moja ya timu kubwa barani ulaya mara zote umekuwa ni mtihani mgumu kwa upande wao, na hii ndivyo ilivyotokea katika mechi nyingine ya kirafiki waliyofungwa na Italy 2-1 mwezi August. Afadhali Spain walisawazisha ikawa 1-1 kwenye mechi hiyo, lakini walishindwa kufanya hivyo katika mechi dhidi ya Switzerland au katika mechi nyingine zote za kirafiki walizofungwa.

Hizo ndio zilikuwa mechi za kirafiki na ni fair kusema Spain watacheza vizuri katika mechi za mashindano – kama ilivyo kwa timu nyingine. Kwa sasa timu nyingi barani ulaya ambazo Spain ni wapinzani wao watakuwa wameshajizatiti namna ya kucheza dhidi ya mbinu ya uchezaji ya La Roja. Hivyo Spain aka La Roja ili kuweza kuwa timu ya kwanza kushinda Euro, then World Cup na baadae kufuatiwa na ushindi wa kombe lingine la bara mfululizo, then a “Plan B” Inahitajika ili kuweza kuitimiza ndoto hiyo.




No comments:

Post a Comment