Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema haina mamlaka (jurisdiction) ya kusikiliza shauri lililowasilishwa mbele yake na aliyekuwa mgombea uenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Michael Richard Wambura.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kamishna Mstaafu wa Polisi Alfred Tibaigana, Wambura aliwasilisha rufani mbele yao akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumuengua kugombea uongozi katika chama hicho.
Tibaigana alisema Kamati yake ambayo ina wajumbe saba, kabla ya kusikiliza shauri hilo ilitaka kwanza kujua kama ina mamlaka (jurisdiction) hayo. Kamati ilizitaka pande zote (bothi parties)- mlalamikaji na mlalamikiwa kueleza kama ina jurisdiction au la.
Mwanasheria wa Wambura, Audax Kahendaguza aliwasilisha hoja zake za kwa nini anadhani Kamati ina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo wakati Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alieleza kwa nini anaamini Kamati hiyo haina mamlaka hayo.
Baada ya hapo, Kamati ilizitoa nje pande zote mbili na baadaye kufanya uamuzi. Uamuzi wa Kamati kuwa haina mamlaka hayo ulikariri Ibara ya 12(4) ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF inayosema: “The decisions of the TFF Elections Committee are final and conclusive and shall not be monitored by any body.”
No comments:
Post a Comment