Search This Blog

Wednesday, October 5, 2011

VIDIC NA SABABU TANO KWANINI ANA UMUHIMU KATIKA MECHI DHIDI YA LIVERPOOL


Nemanja Vidic ni mapigo ya moyo katika safu ya ulinzi ya Manchester United, na sasa United wakiwa wanaeleka kucheza mahasimu wao wa jadi Liverpool F.C ndani ya siku 14 zijazo, uwepo wake katika mechi hiyo utaleta utofauti mkubwa sana kati ya kushinda na kufngwa.

Vidic amekuwa nje ya uwanja kwa maumivu ya misuli ya nyuma ya mguu tangu katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya West Bromwich Albion ambapo aliweza kucheza kwa dk 45 za mchezo.

Ilifikiriwa kwa mara kwanza kwamba majeruhi ya Vidic ni madogo, lakini baada ya vipimo kufanyika vizuri ilionekana kuwa serious.

Vidic sasa amekuwa nje kwa takribani wiki 5-akikosa michezo dhidi ya Tottenham Hotspur, Arsenal, Bolton, Chelsea, Stoke City na Norwich.

Pamoja na kutokuwepo kwa Vidic, United wamefanikiwa kushinda mechi zao zote za EPL msimu huu kasoro mechi dhidi ya Stoke City.

Japokuwa, uwepo wa Vidic kwa mchezo wao wa ugenini dhidi ya Liverpool siku zote ni muhimu sana, na hata kocha wa United Sir Alex Ferguson amedhihirisha juu ya hili juzi, akisema Vidic inabidi afanye kazi kuhakikisha anakuwepo fiti kwa ajili ya kuwakabili majogoo wa jiji.

Hizi hapa ni sababu kwanini United wanamuhitaji Vidic kwa ajili ya mechi hiyo.

1: UONGOZI

Vidic alichaguliwa kuwa nahodha wa kudumu wa United katika msimu wa 2010-11.

Kitambaa cha unahodha hakijabadilisha chochote kwa Vidic, kwani siku zote amekuwa kiongozi shupavu uwanjani bila kitambaa hicho.Lakini kitambaa hicho kinaonyesha imani ya Ferguson kwake Vidic.

Kama Vidic atakuwa fiti kucheza dhidi ya Liverpool, anaweza kujikuta yupo kwenye bench kama sub kwa sababu kadhaa.

Kwanza manager anaweza kutotaka kumuhatarisha kutonesha au kupata majeraha mengine, ingawa kwa sababu ya ubora wa uongozi wake awapo dimbani, Fergie anaweza kumpa nafasi kuongoza safu ya ulinzi.Na kama itakuwa hivyo basi United watakuwa imara zaidi.

Vidic ni mchezaji influence kubwa dimbani, na wachezaji wenzie wanajua wanaweza kumtegemea-especially kwa mabeki ambao ni wadogo kiumri kama vile Chris Smalling, Phil Jones, Jonny Evans na mapacha Rafael na Fabio Da Silva.

2: UWEZO WA KUZUIA

Vidic anajulikana kwa uwezo na ubora wake kuzuia kwa staili yake kucheza soka la kutumia nguvu na akili.

Aina hii ya mentality ni nzuri na bora, tena zaidi ukiwa unaichezea United dhidi ya mahasimu wao Anfield.

Vidic alitajwa kama mchezaji bora wa mwaka wa Barclays Premier League na defenda bora wa msimu wa 2010-11.

3: MFUNGAJI WA MABAO

Hata kama kuna watu kama Wayne Rooney, Nani, na Danny Welbeck wamekuwa waking’ara kwa kufunga mabao msimu huu lakini katika mechi dhidi ya Liverpool wanaweza wakawa kwenye hali ngumu kutupia kambani.

Vidic ambaye amefunga mabao 18 katika mechi zote alizoichezea United.Hii ni idadi ambayo watu wanaweza kuibeza lakini kuna mabeki wengine wanamaliza muda wao wa kucheza bila hata kufunga bao.

Vidic ni hatari sana kwa set-pieces, Liverpool wanafahamu hili na watakuwa makini kumlinda ili asiwadhuru ndani 18.

4: MCHEZAJI WA MECHI KUBWA

Hii mechi ni moja ya mechi kubwa sana duniani.Hii ndio mechi ambayo kila kocha anategemea wachezaji kujituma na kucheza vizuri zaidi.Kama kuna mchezaji mwenye sifa hizi basi anaweza kuwa Vidic.

5: LIVERPOOL F.C

Hakunaga mechi ambayo haisisimui wanapokutana na Man United na Liver na Vidic akiwemo uwanjani.Ameshawahi kupewa red card katika mechi tatu dhidi ya majogoo wa jiji, na mara zote alizotolewa nje Liverpool walishinda.

Ingawa, katika mechi mbili kati ya 3 zilizopita dhdi ya Liver, Vidic alifanikiwa kucheza kwa dk zote 90, na kama hiyo haitoshi United walishinda mechi hizo.

No comments:

Post a Comment