Search This Blog

Saturday, October 29, 2011

UKWELI KUHUSU LUIS NANI: KUTOKA KATIKA DIMBWI LA UMASKINI MPAKA KUWA TAJIRI NA SHUJAA WA MANCHESTER UNITED.


May 2007. Aurelio Pereira alipokea simu kutoka kwa Carlos Queiroz, rafiki wake wa zamani na msaidizi wa Sir Alex Ferguson @ Manchester United.

Kuna kitu kinamsumbua Queiroz.

Amewasili Ureno na bosi wake David Gill kufanya mazungumzo ya uhamisho wa winga mpya kutoka kituo cha kukuza vipaji cha Sporting Lisbon, hivyo Queiroz alikuwa anataka kuhakikishiwa kuwa United wanafanya uamuzi mzuri kwa kulipa £17million kwa Luis Carlos Almeida da Cunha aka Nani.

“Carlos alikuwa hotelini in Lisbon,” anakumbuka Pereira, mwenye umri wa miaka 64 na kiongozi wa jopo la maskauti wa kuibua vipaji katika klabu ya Sporting ambaye ana heshima kubwa nchini Ureno kwa kuvumbua vipaji vya nyota kama Luis Figo, Cristiano Ronaldo, Paul Futre na Ricardo Quaresma.

Anaendelea Pereira, “Quieroz alikuwa anataka kujua kuhusu mentality ya Nani na kama angeweza kuhimili presha ya kuichezea United.

“Hakutaka kujua kama alikuwa na miguu mizuri.Alijua kila kitu kuhusu hilo.Alitaka kufahamu kuhusu tabia yake, vipi angeweza kukabiliana na mazingira ya nchi mpya na timu mpya.

“Yalikuwa majukumu mazito kwa Quieroz kwa sababu ulikuwa ni uhamisho wa Euro million 25 na alitaka kuwa uhakika kwa 100%.Nilimtuliza na kumuhakikishia alikuwa anamnunua mchezaji aliyekamilika.”

Masaa kadhaa baadae United walikamilisha uhamisho wa kumsajili kijana wa miaka 20 kwenda Old Trafford, na ukurasa mpya wa maisha ya Luis Nani ukawa umefunguliwa.

< MJI WA SANTA FILOMENA ALIPOKULIA LUIS NANI>

Nani alikulia katika mji wa Santa Filomena, mji mdogo uliojengwa katika mteremko wa vilima vya Amadora kaskazini magharibi mwa jiji la Lisbon.

Asilimia 30 ya watu kwenye sehemu hiyo wenye umri kati ya miaka 15 na 30 wote wana rekodi mbaya za uhalifu.Haishauriwi kwenda kutembelea eneo hilo kama hauna uhusiano na watukama Alcides Mendes, mwanzilishi na Raisi wa Espaco Jovem, taasisi ya vijana ambayo ilimsaidia Nani kuwa mbali na uhalifu baada ya kutenganishwa na wazazi wake ambao alitoka nao katika Visiwa vya Carpe Verde vilivyopo barani Afrika akiwa na umri mdogo kabisa.

Baba yake Domingos alirudi Santa Filomena on holiday wakati Nani ana miaka 7 na tangu wakati huo hakuwahi kurudi.Mama yake Maria do Ceu aliondoka Ureno na kwenda Uholanzi Nani alipokuwa na miaka 12, na kumuacha Nani akiishi na Aunty yake Antonia pamoja na familia yake, wakiwa wanalala watu sita katika chumba kimoja.

Kupitia madirisha ya nondo unapata nafasi ya kuona vizuri njia ya reli ambayo Nani angetembea kwa miguu kwa umbali wa maili 6 kwenda mazoezini na klabu yake ya kwanza Real Massama.Muda mwingine, kama alikuwa amechelewa, basi alidandia treni na kumkwempa kondakta.On the other hand, umbali wa mwendo wa dakika 2 kutoka nymbani kwao kulikuwa na uwanja mdogo wa kuweza kuhimili wachezaji watano uwanjani - uwanja ambao alijifunza soka la mtaani.

“Hilo soko kubwa kwetu,” anasema Pereira. “Watoto wa kiafrika kama Nani.Hata unaweza kuona anavyochanganya high level performance na tricks kutoka mtaani.”

Hapa ndipo Nani alipojifunzia namna ya kutumia miguu miwili, ubora anaoutumia kuonyesha kipaji chake katika wing ya kulia @ Manchester United.

“Nilikuwa natumia masaa kulenga sehemu ya duara kwa kutumia miguu yangu miwili,nilikuwa nataka sana kujua kucheza vizuri kwa kutumia miguu yangu yote,” anasema Nani.

Kati ya takribani watoto maskini 80 in Santa Filomena, Alcides Mendes anakumbuka Nani ndiye alikuwa mtoto pekee ambaye hakuacha kuzimbikiza ndoto zake.

“Nani alikuwa na mtindo wa kuchagua wachezaji dhaifu kwa upande wa timu yake ili muda wote aweze kumiliki mpira yeye,’ anasema Mendes. “Kwenye pitch walikuwa wanacheza wachezaji watano watano(mtoano), na mshindi anabaki uwanjani kucheza na watano wengine, na muda mwingine timu yake ilipofungwa alikuwa anakasirika sana. Akili yake ilikuwa katika kushinda tu. Muda wote alikuwa anataka kushinda na kuendelea kucheza tu, nothing else.

“Ilikuwa ni vigumu sana kwa watoto kujua ulimwengu nje hapa. Tatizo ni kwamba hapa watu wengi waishio hapa sio wahamiaji lakini pia sio Wareno pia.

“Wamezaliwa hapa lakini wazazi wao wanatokea katika makoloni ya zamani ya Ureno kama Cape Verde, hivyo wanakuwa wanatengwa na jamii (Nani hakupata uraia wa Ureno mpaka alipofikisha miaka 18).Hata mashuleni kuna madarasa maalum kwa ajili yao.

“Nyumba aliyokuwa anaishi Nani ilikuwa ndogo lakinifamilia yao ilikuwa ina umoja sana na walikuwa na mahusiano mazuri katika yao. Kaka yake mkubwa alikuwa mtu muhimu sana kwake. Alikuwa anafanya kazi katika ujenzi na muda mwingine Nani alikuwa naenda kumsaidia kazi.”

Pamoja na ugumu wa maisha, Nani ana kumbukumbu nzuri kuhusu makuzi yake. Mchezo mwingine aliokuwa anaupenda akiwa na taasisi ya Espaco Jovem, ulikuwa ni Capoeira, muunganiko wa Brazilian martial art na music.Hata tabia yake ya kuruka someraults (sarakasi) ambayo ndio huifanya kila anapofunga ni kitu ambacho ni cha kawaida sana katika mitaa ya Santa Filomena.

“Rafiki zangu walisema nilikuwa kichaa lakini nilikuwa nataka kupata kitu Fulani kutoka capoeira na ndio maana siku zote nashangilia kwa kuruka sarakasi,” alisema Nani katika mahojiano ya TV in Portugal wiki nne zilizopita. “Watu siku zote walikuwa wanazungumza kuhusu Nani(jina alilopewa na dada zake), yule mtoto mwenye nywele za curly.

“Maisha yalikuwa magumu lakini ya furaha. Tatizo pekee lilikuwa njaa. Tulikuwa na hali mbaya sana nyumbani, hukukuwa na chakula, alikuwa kaka yangu Paulo ambaye alileta chakula kidogo nyumbani.

“Tulifikia hatua ya kuiba matunda na vitu vingine vya kula. Nilienda katika tabia zisizo nzuri lakini siku zote nilifanikiwa kurudi katika mstari ulionyooka.

“Hauwezi kubadilisha wala kuuficha ukweli huu ya maisha yako ya zamani, na sioni aibu juu ya sehemu nilipozaliwa au maisha magumu niliyopitia. Kama nimefika hapa nilipo ilikuwa kwa sababu ya juhudi zangu na moyo wangu wa kujituma.”

Nani anakataa kwamba baba yake alimtekeleza, anasisitiza sheria na kanuni za Ureno zilizomzuia kurudi kwa familia yake.Wanaume hawa wawili walikutana tena mwaka 2006 na Nani anakumbuka: “Alijaribu kunielezea kwamba hakunitekeleza, lakini nilimzuia asiendelee na mazungumzo yale na nilimwambia: “Hauhitaji kujieleza, nipo poa.Nina furaha, nafahamu kilichotokea, hivyo hahitaji kunielezea chochote.”

“Sikuwa namkumbuka sasa kwa sababu kaka Zangu alikuwa katika nafasi yake. Walinipa kila aina ya sapoti na mapenzi. Nilikuwa mdogo, nalindwa na hakuna aliweza kunigusa.”

Nani hajasahau kipindi alipokuwa anategemea timu yake yake ya Real Massama kwa ajili ya chakula na rafiki zake kwa ajili ya nguo.

Nilikuwa na marafiki wengi waliokuwa wananisaidia sana na kunisapoti kwa sababu nilikuwa na maisha magumu. Nilikuwa sina uwezo wa kununua nguo nzuri hivyo rafiki zangu walinipa zile ambazo walikuwa hawazivai tena. Sometimes walikuwa wananialika kwenda kukaa kwao hata wiki.

“Nilikuwa mtoto wa Real Massama.Walinipa kila kitu-viatu na chakula.Nilikuwa Napata huduma kuliko mtu yeyote katika klabu ile.”


Mshauri wa Nani katika klabu hiyo ya daraja la pili, Luis Dias, anakiri Nani angeweza kujiunga na Benfica badla ya Sporting Lisbon na Manchester United.Dias, sasa ni kocha wa timu ya vijana ya Sporting, na alikuwa kocha wa Nani katika timu ya under 11 kipindi Massama walipoalikwa kucheza @ Stadium of Light (Estadio de Luz) na kocha wa zamani wa Benfica Graeme Souness.

“Ni kweli alifanya mazoezi na Benfica na Sporting,” anasema Dias. “Benfica waliwapeleka Massama kucheza katika uwanja mkubwa mbele ya mashabiki wote kabla ya mchezo wao na Boavista.

“Lakini mvua ilikuwa inanyesha sana siku hiyo na Souness alisema watoto hawatocheza kwa sababu wangeharibu majani.Unapotoa ahadi kwa mchezaji wa umri wa namna ile, unatakiwa kuitimiza, lakini Benfica walishindwa.

“Baada ya muda kidogo, walimfuata Nani kwa ajili ya kumsajili lakini Nani alifikiri hawakuwa na heshima kwake .Hakutaka kuwa bidhaa kwa Benfica. Ingawa alikuwa maskini lakini Nani na kiburi sana.”

Katika kutambua machungu ya Nani ya kubeba viatu vyake katika mfuko wa plastiki (Rambo), Dias aliandaa mchango kutoka kwa wachezaji wakubwa kumchangia Nani pesa ananunue mfuko mzuri.Ilikuwa ni moja ya sehemu ya special attention aliyokuwa akipewa Nani.

“Nilikuwa zaidi ya kocha, nilikuwa saikologisti, daktari, na dereva sometimes. Nilijua kazi yangu haikuwa kumfundisha tu. Pia nilitakiwa kuwa mwalimu wake, ku-control chakula anachokula, wapi alikuwa analala, kwenda shule na kuhakikisha alikuwa anaudhuria darasani. Hivi ni vitu ambavyo wazazi wanafanya.

“@ Massama, alikuwa anakula chakula cha mchana kabla ya mazoezi na kula dinner baada ya hapo. Kilikuwa ni kitu ambacho watoto wengine hawapati. Kama alikuwa hajakula akiwa klabuni basi asingekuwa amekula kabisa.”

Ni mwendo wa nusu saa kutoka Lisbon, kusini maili 11 kutoka katika daraja la Vasco da Gama na mdomo wa mto Tagus, kabla hujafika vijijini around Alcochete, ndipo mahali Nani alipong’arisha kipaji chake.

Hapa ndio kilipo chuo cha Academica do Sporting Clube de Portugal.

Ni takribani miaka 10 tangu Sporting walipojenga hii complex, ikiwa na viwanja saba vilivyokamilika na hotel ya watoto 50 kati ya 130 ambao wanajifunza mahala pale. Inagharimu zaidi ya £4m kuiendesha academy hiyo, lakini Diogo Matos, mkurugenzi wa academy, anakisia academy hiyo tayari imeshaipa klabu ya Sporting faida ya £150 million kupitia mauzo ya mastaa kama Cristiano Ronaldo na Nani.

“Tuna kitu Fulani maalum kinachoendelea hapa,” anasema Matos ambaye matunda yake ya sasa ya wachezaji under 19 wameibuka kuwa moja ya timu bora barani ulaya katika michuano ya NextGen Series(champions league for under19).

Ingawa iliamuliwa kumbakisha Nani at Massama kwa sababu ya hali ya nyumbani kwao, lakini alikuwa akifanya mazoezi na Sporting kabla ya kujiunga na klabu hiyo akiwa na miaka 16. Nani alivuna mshahara wa £900 kwa mwezi akiwa kama mchezaji wa academy, lakini aliibuka kupata £10,000 aliposaini kama professional.

Pesa hiyo ilitumika kumuhamisha aunt yake Antonia nje ya Santa Filomena, na ameendelea kuisapoti familia yake kiuchumi hadi sasa anapopata mshahara mkubwa akiwa na United.Ni mzigo ambao Nani anapenda kuubeba lakini anakiri, hali hii imekuwa ikiingilana na career in premier league.

“Namshukuru Mungu kwa hali yangu ya sasa na mimi ni nguzo katika familia yangu.Kila linapotokea tatizo wanakuja kwangu mimi na sijawahi kusema hapana.Nafahamu wapi nilipitia kipindi nilipokuwa mdogo.Sipendi kuona mtu yeyote katika familia yetu akiwa na shida.

“Lakini matatizo binafsi yananifanya nipoteze umakini. Muda mwingine kiakili nachoka kabisa. Inaweza kuwa hata kabla ya mechi kubwa au derby, lakini nitapokea simu na kumpigia yeyote anayehusika kutatua tatizo lolote linaloikumba familia yangu.

“Napata pesa nyingi lakini hazikushuka tu kutoka mbinguni. Lazima nijitume. Nisipocheza vizuri, watu watanifukuza.”

Maisha nchini England hayakuwa mapesi kwa Nani. Ilichukua muda kupata imani kutoka kwa mashabiki na kuibuka kutoka kwenye kivuli cha Ronaldo at United. Kulikuwa na kipindi ambapo wasiwasi wa Queiroz juu ya Nani kuweza kumudu kucheza Old Trafford ilianza kuchukua nafasi.

Hata baada ya kuongoza kwa kutoa asisists nyingi msimu uliopita, alijikuta akiwa kwenye benchi katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Barcelona, na kuwasili kwa winga wa kiingereza Ashley Young kipindi cha kiangazi kulizusha speculations kwamba mreno huyo angeweza kuondoka Old Trafford.

In fact, Nani amethibitisha ubora wake akiwa na United msimu huu. Ana furaha nje ya uwanja na hata nyumbani kwake – Cheshire ambapo anakaa na mpenzi wake Daniela na mbwa wao wawili.

“Sikuwa na bahati nzuri kuzoea maisha ya England, tena ilikuwa vigumu sana kuishi peke yangu, huku nikiwa sijui kuongea lugha ya pale. Ilifikia kipindi nilikuwa naishi kwa Cristiano na nilijisikia vizuri sana Kulikuwa kuna watu poa sana na tulikuwa na kila kitu – swimming pool, Jacuzzi, tennis, kiukweli kipindi nakaa kwa Ronaldo sikuwahi kui-miss familia yangu.

“Lakini baadae ilibidi niondoke kwa Ronaldo kwa sababu ilibidi niwe na maisha yangu. Ilikuwa vigumu sana kwa sababu ilikuwa nyumba kubwa na usiku ilikuwa kama nyumba ya mchawi.

“Nilikuwa naogopa hata kuwa nyumbani. Sometimes sikuwa natoka hata chumbani. Nilienda kulala mapema bila kula vizuri kwa sababu sikutaka kula dinner peke yangu.”

Hata sasa, Nani anakiri, hawezi kuangalia movie za kutisha kwa sababu zilikuwa zinamfanya asilale kwa woga. Anapenda kukaa na Daniela na kuangalia tamthilia na kupig piano.


October 2011. Katika uwanja wa Porto Estadio Do Dragao. Nani alifunga mabao mawili ya mwanzo katika ushindi wa Ureno wa 5-1 dhidi ya Iceland, na kumfunika mchezaji mwenzie Ronaldo. Siku iliyofuata katika kurasa za mbele za gazeti la Correio da Manha na A Bola walieka picha zake akiwa anashangilia.

Mtoto kutoka Santa Filomena ametoka mbali sana.

No comments:

Post a Comment