Search This Blog

Friday, October 7, 2011

TWIGA STARS KUANZA NA NAMIBIA MATAIFA HURU YA AFRIKA


Timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imepangwa kucheza na Namibia katika mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za nane za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 13, 14 na 15 mwakani wakati mechi ya marudiano ya raundi hiyo ya awali itachezwa Dar es Salaam kati ya Januari 27, 28 na 29 mwakani.

Alisema iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Namibia, katika raundi ya kwanza itacheza na mshindi wa mechi kati ya Ethiopia na Misri ambazo pia zinaanzia raundi ya awali.

Mechi ya awali ya raundi ya kwanza itachezwa ugenini kati ya Mei 25, 26 na 27 mwakani.

Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Juni 15, 16 na 17 mwakani. Timu ambazo zinaanzia moja kwa moja raundi ya kwanza kutokana na kuwa juu katika viwango vya ubora ni Afrika
Kusini, Cameroon, Equatorial Guinea na Nigeria.

Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano hayo ni Guinea, Ivory Coast, Kenya, Msumbiji, Zambia, Malawi, Morocco, Tunisia, Senegal, Burundi, Botswana, Zimbabwe, Uganda,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mali na Ghana.

No comments:

Post a Comment