Search This Blog

Friday, October 21, 2011

CHANZO CHA UHASAMA NA UADUI MKUBWA KATI YA JIJILA MARSEILLE DHIDI YA ARSENE WENGER

JAPO ARSENE WENGER AMEKUWA AKICHUKIWA NA MASHABIKI WA TIMU PINZANI ZA ENGLISH PREMIER LEAGUE KUTOKANA NA KIBURI CHAKE NA KWA BAADHI YA MASHABIKI WA KLABU YAKE YA ARSENAL KUTOKANA NA UWEZO MDOGO WA KUSOMA ALAMA MUHIMU ZA NYAKATI , CHUKI HIZI SI CHOCHOTE UKIFANANISHA NA CHUKI ILIYOKO DHIDI YA WENGER KWENYE JIJI LA MARSEILE .SABABU KUU YA CHUKI HII NI KWAMBA WENGER ALIKUWA MOJA YA SABABU KUU ZILIZOUMALIZA UFALME WA MARSEILE KWENYE SOKA LA UFARANSA MIAKA 20 ILIYOPITA .



MAPEMA MWANZONI MWA MIAKA YA 90 , MARSEILE WALIKUWA TIMU KUBWA BARANI ULAYA , KAMA ILIVYO BARCELONA AU MANCHESTER UNITED KWA MIAKA YA HIVI KARIBUNI.TIMU HII ILIKUWA IMETWAA UBINGWA WA LIGI YA UFARANSA MARA TANO MFULULIZO NA MSIMU WA MWAKA 1992-93 WALITWAA UBINGWA WA ULAYA WAKIIFUNGA AC MILAN BAO MOJA BILA.

UTAMU WA USHINDI HUU WA KIHISTORIA HATA HIVYO ULIGEUKA NA KUWA SHUBIRI CHUNGU KWA MASHABIKI WA MARSEILE NA WAFARANSA WOTE BAADA YA KUGUBIKWA NA KASHFA YA RUSHWA AMBAYO ILILILAZIMU SHIRIKISHO LA VYAMA VYA SOKA BARANI ULAYA UEFA KUWAVUA MARSEILE UBINGWA .

KASHFA HII ILIIBUKA BAADA YA BEKI WA KLABU YA VALENCIENNE JACQUES GLASSMAN KUFICHUA SIRI JUU YA JINSI MARSEILE KUPITIA KWA RAIS WAKE BERNARD TAPIE WALIVYOKUWA WAKIPANGA MATOKEO KWA KUWAHONGA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA TIMU NDOGO .

UPANDE WA PILI ARSENE WENGER ALIKUWA AKIIJENGA KLABU MOJA YA MONACO HUKU AKIWA NA WACHEZAJI HATARI KAMA KINA GEORGE WEAH NA GLENN HODDLE , MONACO ILITWAA UBINGWA WA UAFARANSA MWAKA 88 NA WAKATI MARSEILE WAKIWA MABINGWA MONACO NDIO WALIKUWA WAPINZANI WAKE WAKUBWA . ARSENE WENGER ALIAMINI KUWA MONACO NDIO WALIOSTAHILI MAFANIKIO WALIYOKUWA WAKIYAPATA MARSEILE LAKINI HAIKUWA HIVYO KWA KUWA TIMU YAKE HAIKUWA NA MSULI WA KIFEDHA HIVYO WALIKUWA WAKICHEZA MECHI UWANJANI PEKE YAKE TOFAUTI NA WENZAO WALIOKUWA WAKICHEZA NDANI NA NJE YA UWANJA .

MAWAZO YA WENGER YALIUNGWA MKONO NA ALIYEKUWA KOCHA WA KLABU YA VALENCIENNE BORO PRIMORAC AMBAKO MCHEZAJI WAKE ALIFICHUA JANJA YA MARSEILE . KWA SASA PRIMORAC NI KOCHA MSAIDIZI WA ARSENAL CHINI YA WENGER . PRIMORAC ALIFICHUA SIRI KUWA RAIS WA MARSEILE ALIMFUATA NA KUMPA HONGO ILI APINDISHE USHAHIDI NA KUMLINDA LAKINBI HAKUFANYA HIVYO NA MATOKEO YAKE YALIKUWA KUVULIWA KWA TAJI LA MARSEILE .

KWA MASHABIKI WA MONACO WENGER ALIKUWA SHUJAA KAMA ALIVYOKUWA BEKI WA VALENCIENNE GLASSMAN NA KOCHA WAKE PRIMORAC MBELE MASHABIKI WAO , LAKINI UKITOKA NJE YA VILABU VYAO WATU HAWA WATATU WALICHUKIWA NA UFARANSA NZIMA KWA KULIAIBISHA SOKA LA NCHI YAO NA KWA MASHABIKI WA MARSEILE WATU HAWA WALIONEKANA ZAIDI YA WASALITI . UAMUZI WA GLASSMAN WA KUZUNGUMZA WAZI JUU YA MAOVU YA MARSEILE ULIMFANYA APEWE TUZO YA FAIR PLAY YA FIFA MWAKA 1995 WAKATI HUO HUO AMBAO ARSENE WENGER ALIFUKUZWA KAZI NA MONACO KWA MASHANGAO WA WENGI NA ALITIMKIA HUKO JAPAN KUFUNDISHA KLABU YA GRAMPUS 8.

HADITHI YA MARSEILE ILIISHIA HAPO KWANI WALIVULIWA TAJI LA ULAYA NA TAJI LA UBINGWA WA UFARANSA PIA NA HAIKUISHIA HAPO KWANI WALISHUSHWA DARAJA HUKU RAIS BERNARD TAPIE AKIFUNGWA GEREZANI . TANGU MIAKA HIYO HAWAKUREJEA KUWA TIMU KUBWA KAMA ILIVYOKUWA ENZI HIZO NA NI UJIO WA NAHODHA WA ZAMANI DIDIER DESCHAMPS NDIO ULIOREJESHA HADI YA MARSEILE KAMA TIMU YA KUOGOPWA UAFARANSA KWANI CHINI YAKE WALITWAA UBINGWA WA MWAKA 2009/ 2010 .

No comments:

Post a Comment