Search This Blog

Thursday, October 6, 2011

BREAKING NEWS: WHITECAPS YAMZUIA NIZAR KUJIUNGA NA STARS-KUKOSA MCHEZO WA MOROCCO

Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Nizar Khalfan hatokuwemo katika kikosi cha Taifa Stars kitakachokwenda Morocco kwa ajili ya mechi ya mwisho na muhimu ya michuano ya kugombea nafasi ya kushiriki kombe la mataifa ya Afrika litakalofanyika mwakani nchini Gabon na Equatorial Guinea.

Nizar amezuiliwa na klabu yake ya Vancouver Whitecaps kujiunga na Taifa Stars baada ya shirikisho la soka nchini TFF kuchelewa kupeleka barua kwa klabu hiyo kumuombea ruhusa kiungo huyo kuja nchini kujiunga na timu ya taifa.

Kwa mujibu kwa Vancouver Whitecaps ni kwamba barua ambayo ilitumwa na TFF ilichelewa kufika hivyo timu hiyo imegoma kumruhusu Nizar kuja Bongo.

Tanzania inakabiliwa na mtihani mgumu wa kuhakikisha inaifunga Morocco nyumbani kwa idadi ya mabao yasiyopungua 3-0 ili kujihakikishia walau nafasi moja ya kushiriki AFCON 2013.

No comments:

Post a Comment