Search This Blog

Monday, September 19, 2011

TIMBE: NAISUKA UPYA SAFU YA USHAMBULIAJI, VILLA SUBIRINI KIPIGO.



Kocha mkuu wa Yanga, Sam Timbe amepanga kuifanyia kazi safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya kupata ushindi katika mechi ijayo dhidi ya Villa Squard itakayochezwa kesho kutwa kwenye uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam.
Hiyo, imetokana na safu ya ushambuliaji inayoongozwa na wachezaji wa kulipwa Davies Mwape, Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza kushindwa kutumia nafasi wanazopata kutoka kwa viungo wake.
Timbe alisema, amepanga kutumia siku mbili kuwanoa washambuliaji wake kwa kuwapa mbinu za kufumania nyavu katika mechi hiyo ya keshokutwa kwa kuanza na leo na kesho.
Kocha huyo aliendelea kusema, hilo linawezekana kutokana na wachezaji kuhitaji kuongezewa vitu vichache ambayo muhimu kama wakivizingatia watapa matokeo mazuri .
“Safu ya Ushambuliaji ndiyo inaangusha, wameshindwa kutumia pasi na krosi wanazopata kutoka kwa viungo wangu,” alisema Timbe raia wa Uganda.
Mapungufu hayo Timbe aliyona wakati timu hiyo ilipocheza na Azam FC, matokeo yaliyomalizika kwa Yanga kukubali kipigo cha bao 1-0 kupitia kwa mshambuliaji wake, John Bocco.

No comments:

Post a Comment