Search This Blog

Thursday, September 8, 2011

TENGA: SAHAUNI WAZO LA KAMPUNI KUENDESHA LIGI KUU YA TZ BARA.

Raisi wa TFF Leodegar Tenga amezitaka klabu za Ligi Kuu kusahau habari ya ligi kusimamiwa na kampuni na sasa yupo mbioni kuunda chombo kitakachoendesha ligi hiyo.
Tenga anadai migogoro inayoendelea katika nchi za Kenya na Uganda ni kwasababu ya ligi ya nchi hizo kuendeshwa na kampuni.
Akasisitiza kamati ya utendaji ya TFF ndio itakayoteua majina ya viongozi watakaounda chombo maalum cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza ili kuwe na uwiano sawa.

1 comment:

  1. namuunga kono Tenga kwa asilimia 100%maana yanayowakuta Kenya sio mabo yakuchekea

    ReplyDelete