Search This Blog

Sunday, September 11, 2011

klabu za Simba na Yanga zinahitajika kuongeza umakini katika usajili wa wachezaji wa kimataifa ili kuleta changamoto kwenye ligi.

Niyonzima amchongea mwamuzi TFF

KUFUATI kadi nyekundu aliyopewa kiungo wao mchezeshaji, Haruna Niyonzima uongozi wa Yanga umepanga kumshtaki mwamuzi, Alex Mahagi aliyechezesha mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting. Yanga katika mechi hiyo, ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema wameshangazwa na maamuzi tofauti kutoka kwa mwamuzi wa kati ambaye ameonekana kuipendelea wapinzani wao. Sendeu alisema, wamepanga kwenda kwenye makao ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili kumshtakia mwamuzi huyo kufuatia maamuzi aliyokuwa anayotoa yenye lengo la kuivuruga Yanga. “Hatutajua lini tutapeleka ripoti hiyo TFF, hadi viongozi tutakapokutana itajulikana tumekerwa na maamuzi ya mwamuzi wa kati, kadi nyekundu aliyopewa Niyonzima haikustaili . “Mwamuzi huyo tunamjua muda mrefu ni shabiki wa Simba na mara nyingi tumekuwa tukimuona

klabu za Simba na Yanga zinahitajika kuongeza umakini katika usajili wa wachezaji wa kimataifa ili kuleta changamoto kwenye ligi-Mutengwa Selemani

KOCHA mkuu wa Ruvu Shooting, Mutengwa Selemani amesema uwepo wa mastaa wengi Yanga ndiyo sababu ya kufanya vibaya kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara inayoendelea katika viwanja tofauti. Jeuri hiyo, ameipata baada ya kuvuna pointi moja dhidi ya Mabingwa hao watetezi kwa kutoka sare ya 1-1, mechi iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Selemani alisema kuwa maproo hao wanahitajika kuongeza uwezo binafsi ndani ya uwanja na siyo kuridhika kutokana ushindani wa ligi uliopo. Selemani alisema, klabu za Simba na Yanga zinahitajika kuongeza umakini katika usajili wa wachezaji wa kimataifa ili kuleta changamoto kwenye ligi. “Wachezaji baadhi wa Yanga waliosajiliwa na Yanga viwango vyao vinafanana na wazawa, hivyo wanatakiwa kuongeza umakini katika kusajili maproo. “Sisi tutaendelea kuwapa nafasi wazawa kwenye timu yetu, tunaamini mitaani wapo wengi wenye uwezo watakaoleta ushindani,” alisema Selemani.

Machaku atuliza machungu Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Salum Machaku ameitaka klabu kuacha papara badala yake kucheza soka licha ya kuanza vibaya ligi kuu ya Tanzania Bara. Machaku hivi karibuni alifungwa bandeji gumu (P.O.P.) kwenye mguu wake wa kushoto baada ya kupata majeraha katika kidole akiwa kwenye timu ya taifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Machaku alisema ligi bado mbichi na watani wao wa jadi Yanga wanaweza kufanya vizuri kutokana na uimara wa kikosi chao. Kiungo alisema, wanachotakiwa kuondoa presha ndani ya uwanja badala yake kucheza soka katika kutetea ubingwa wao. “Yanga sasa hivi wanapresha baada ya kupoteza mechi moja na kutoa sare tatu, wanachotakiwa kutulia na kucheza mpira timu yao nzuri,” alisema Machaku. Machaku kabla ya kutua Simba alikuwa akiichezea Mtibwa Sugar ya Manungu kwenye msimu huu wa ligi inayoendelea.

No comments:

Post a Comment