Search This Blog

Friday, September 9, 2011

Bolton vs Manchester Utd : Preview

Manchester United wanaingia kwenye mchezo huu utakaopigwa kwenye uwanja wa Reebok wakitafuta rekodi ya asilimia mia moja baada ya kushinda michezo yote mitatu huku wakiwa kileleni mwa ligi.
Kukweli United imeanza msimu huu ikiwa na sura na swagga mpya ambayo ni tofauti na kile kilichoonekana msimu uliopita.
Katika misimu ya Ligi kuu ya England imezoeleka kuwa United huaanza kwa staili ya marathon yaani wanaanza ligi kwa mwendo wa taratibu lakini wanakuja kushika kasi kuanzia miezi Fulani ya katikati ya ligi na hatimaye kumalizia vizuri. United ya sasa hivi imeanza ligi vyema huku ikiwa na kikosi kichanga.
Katika mchezo United inatarajiwa kuwakosa wachezaji ambao waliumia mwanzoni mwa msimu, mabeki Rio Ferdinand na Nemanja Vidic watakosa pambano hili sambamba na Rafael Da Silva.

Sidhani kama hili litakuwa tatizo sana kwa United kwa kuwa wana watu ambao watacheza kwenye nafsi za wachezaji hawa vizuri tu.
United pia itamkosa mshambuliaji Danny Welbeck ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Arsenal.
Bado siri ya ushindi wa United itaendelea kuwa ‘patnership’ ya Wayne rooney na Ashley Young ambayo imeonekana kufanya kazi vizuri sana huku viungo Anderson na kinda Tom Cleverly wakiunganisha mambo katikati mwa uwanja huku Darren Fletcher akitarajiwa kurejea pia baada ya kupona tatizo la kirusi lililokuwa linamsumbua ambapo amecheza vyema kwenye mechi mbili za timu yake ya taifa.

Kitu pekee kinachoweza kuwa tatizo kwa United ni kipa David De Gea ambaye hakika Owen Coyle lazima atawapa maagizo wachezaji wake hasa Martin Petrov na Ivan Klasnic ya kupiga mashuti ya mbali wakijua fika kuwa David De Gea ana tatizo kubwa la kucheza mipira ya mbali na hili linakuja kama changamoto kwa viungo na mabeki wa United kumpa De Gea ulinzi wa kutosha na kuepusha mianya ambayo wachezaji wa Bolton wanaweza kupiga mashuti.
Kwa upande wa Bolton kocha Owen Coyle atamkosa kiungo Marcos Alonso ambaye ana jeraha kubwa la mguu pamoja na lundo la wachezaji kama Tyrone Mears , Lee Chung-Yong , Stuart Holden, Sean Davis , Sam Ricketts , na Ricardo Gadner ambao wana majeraha ya muda mrefu.
Mshambuliaji aliyesjailiwa toka Liverpool David Ngo’g anaweza kuwa mtu muhimu ambapo huenda akatumika kama mbadala wa Kevin Davies na Ivan Klasnic watakaoanza kwenye safu ya ushambuliaji.
Kutakuwa na ‘batlle’ kubwa kati ya walinzi wa Bolton kina Gary Cahil , Paul robinson na Zat Knight ambao watakuwa na kazi kubwa ya kuwachunga Rooney na Young pamoja na Luis Nani.

Sir Alex Ferguson amekuwa akiwatumia Ashley Young na Luis Nani pembeni mwa uwanja huku Young akicheza kushoto na Nani akicheza kulia.
Young amekuwa hatari sana anapocheza kushoto ambako anaingia ndani na kujipasia kwenye mguu wa kulia anaoutumia kupiga mashuti kama alivyofanya kwenye mechi dhidi ya Arsenal na hata mechi dhidi ya West Brom ambapo alifunga mara mbili kwenye mechi ya Arsenal na alisababisha bao kwenye mechi ya West Brom.
Katikati Fabrice Muamba na Nigel Reo-Coker watapambana na Anderson na Cleverly au Fletcher au hata Michael Carrick , kumbuka United wanaweza kualzimika kupumzisha baadhi ya wachezaji wakiwa na wazo juu ya mchezo wao wa ligi ya mabingwa dhidi ya Benfica wiki ijayo.
Rooney anatarajiwa kuanza na Javier Hernandez upande wa juu wa United japo Dimitar Berbatov atakuwa benchi.
Bolton inaye mtu aliyewahi kuwa winga wa United Chris Eagles ambaye anaweza kutumia uwezo wake binafsi na jinsi anavyoijua United kiundani baada ya kuwa mchezaji wake kwa muda mrefu.
Bolton Wanderers wamewahi kushinda mara moja tu kati ya mara 17 za mwisho walizokutana na vija wa Sir Alex Fergusson.
Bolton wamekuwa wenyeji kwa Man United mara zisizopungua 58 kwenye mechi za ligi ambapo wameshinda mara 25 , wamefungwa mara 18 na wametoka sare mara 15.
Katika michuano yote waliyowahi kukutana Bolton wamefunga mabao 159 na United wamefunga mabao 187
Hadi sasa United imeshinda michezo yote mitatu ya ligi tangu mwanzo, wakifunga mabao 13 huku wakiongoza ligi.

Bolton wao wameshinda mchezo mmoja huku wakiwa wamefungwa miwili .
Wayne Rooney na Ashley Young wamefunga mabao saba kwa pamoja katika mnichezo mitatu ya United na ukihesabu na ile ya England wamefunga mabao 10.
Iwapo United itashinda utakuwa ushindi wake wa 200 wakiwa ugenini kwenye mechi ya ligi kuu ya

1 comment:

  1. nice summary.. ila nilikua nasajest ungekua unaandika na muda ambao mechi zinachezwa kwa masaa ya kiswahili coz kubadili mda wa kwao kule sometimes tunaweza kukosea kwa kuongeza au kupunguza masaa.. all in all, this is a nice article.. thanx

    ReplyDelete