Search This Blog

Friday, September 9, 2011

Arsenal mpya na Matarajio mapya...


Arsene Wenger amelazimika kukiongoza kikosi cha Arsenal kilichodhoofishwa na majeraha kwa wachezaji muhimu huku wengine wakifungiwa.
Bacary Sagna alikosa kipigo cha mabao manane dhidi ya Man United na baada ya hapo Thomas Vermaelen ambaye ndio kwanza alikuwa amerudi akiwa hajacheza hata mechi tano tangu akose msimu mzima uliopita naye ameumia tena safari hii akikosa miezi miwili kwa jeraha jipya la enka.

Vermalaen anaungana na Sebastien Squilaci ambaye ana jeraha kama lake,Kieran Gibbs ameumia misuli ya nyuma ya mguu na Jack Wilshere na Abou Diaby wote wana majeraha ya enka ambayo yanawafanya wakose miezi isiyopungua miwili kwa Wilshere na Abou Daiby amebakiza siku chache kabla ya kurudi uwanjani.

Sagna kwa upande wake anaweza kurudi ndani ya muda na kucheza mechu dhidi ya Swansea City na Gervinho, Alex Song na Carl Jenkinson wote wamefungiwa kucheza michezo kadhaa kwa kadi nyekundu walizopata kwenye michezo ya nyuma.
Kukosekana kwa Kieran Gibbs kunamaanisha kuwa njia ni nyeupe kwa Andre Santos kucheza mechi yake ya kwanza tangu asajiliwe toka Fernabance huku mchezaji mwingine mpya Per Mertersecker naye akitarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe toka Werder Bremen akisaidiana na Johan Djorou katikati kwenye safu ya ulinzi.

Sambamba na hao Mikael Arteta naye atavaa uzi wa washika bunduki kwa mara ya kwanza tangu aondoke Everton .
Mchezaji mwingine mpya toka Korea ya Kusini Park Chung Young atakuwepo benchi kwa kuwa bado ana uchovu wa safari ndefu na mechi ngumu aliyocheza mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa amerejea majuzi tu toka kwao Korea alikokuwa na timu yake ya taifa .
Kwa upamde wa Swansea Kocha Brendan Rogers hana wasiwasi wa kuwakosa wachezaji kutokana na majeraha mbalimbali kama ilivyo kwa Arsenal japoa atakosa huduma ya mchezaji Ferry Bodde ambaye anasumbuliwa na goti na Alan Tate ambaye anatarajiwa kukosa sehemu kubwa ya msimu kutokana na mguu wake kuvunjika.

Swanse wana habari njema za kurejea kwa Gary Monk ambaye hivi karibuni alifanya mazoezi na timu ya vijana baada ya kuwa majeruhi wa muda mrefu.

Wengi wataipa Arsenal nafasi kubwa ya kuondoka na pointi tatu kwa mara ya kwanza msimu huubaada ya kutoka sare na kufungwa michezo miwili huku kipigo cha bao nane toka kwa Man United bado kikipiga kengele masikioni mwa mashabiki wengi.
Kikosi cha Swansea kinashika nafasi ya sita kutoka mwisho wakiwa wametoka sare mara mbili na kufungwa mchezo mmoja na hadi sasa hawajaweza kufunga bao lolote tangu waje kwenye ligi kuu ya England.
Robin Van Persie akicheza na Theo Walcott pembeni yake huku Mikael Arteta akiwa nyuma yao kama mpishi mkuu wa mipira ya mwisho, Arteta atakuwa akisaidwa na Emanuel Frimpong ambaye atarejea toka kwneye adhabu ya kadi mbili za njano alizopata kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.
Ni dhahiri Arsenal watakuwa na nafsi kubwa ya kushinda japo kila mmoja anangoja kuona kama homa yao imepona au la na kwa upande wao bado hawajashinda hadi leo wakitoka sare mara mbili na kufungwa mechi mbili.


Timu hizi mara ya mwisho zilicheza kwenye msimu wa mwaka 1982-83 ambapo Arsenal walishinda nyumbani na ugenini kwa matokeo ya 2-1.
Msimu wa kabla ya hapo Swansea wao ndio walioshinda mara mbili wakiwafunga Arsenal 2-0 mara zote.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana tangu mfumo mpya wa ligi kuu ya England kuanzishwa.
Arsenal ndio timu ya kwanza kwenye historia ya Ligi kuu kuwa na wachezaji watatu waliotolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi tatu za kwanza za msimu na hadi sasa ukuta wao umeonekana kuvuja sana kwa kufungwa mabao 10 katika michezo miwili tu .

No comments:

Post a Comment