Search This Blog

Thursday, August 4, 2011

UJUMBE TOKA KWA MDAU Patrick Semiono

Salaam mkuu,,
Pole na majukumu na hongera sana katika suala zima la kusogeza gurudumu la tasnia ya michezo hapa nchini mahususi soka kama mchezo wenye mashabiki wengi.
Natumai jina ni geni kwako lakini mie na wewe tunajuana sana haswa leaders club kwenye mabonanza ya kusukuma gurudumu la afya za wanamichezo wa zamani kabla sjahamia Loliondo kimajukumu.

Kusudio haswa la kukuandikia barua pepe hii ni kutaka kuchukua hatua za ulazima katika suala lilitokea jana la TBL kudhamini Klabu kongwe za Simba na Yanga.
Soka la sasa ni kweli laendeshwa kifedha zaidi lakini nataka niende juu ya upeo wa fikra za kawaida(beyond normal thinking) katika kuona hasara za udhamini wa TBL katika kuua soka la Tanzania.
Klabu za Simba na Yanga ni moja ya vilabu vilivyokaa mda mrefu bila mafanikio kuliko vilabu vyovyote katika Afrika Mashariki na Kati kulingana na umri ulionao.Klabu zenye umri sawa nazo ni El marrek na El hilal ya Sudan ambazo zimefanya mambo mengi nchini mwao na Afrika kwa ujumla.
Pamoja na udhamini kadha wa kadha (vodacom,kilimanjaro,magazeti) klabu za Simba na Yanga zimekuwa zikifanya vibaya kwenye mashindano makubwa na mbaya zaidi wadau(mashabiki na viongozi)wanadhani ni bahati mbaya kumbe ni uhalisia vilabu hivyo haviwezi kuleta medali zaidi ni majungu ya soka.

Arsenal ni klabu ambayo haijachukua kombe lolote zaidi ya miaka sita lakini kwenye viwango vya Fifa ni klabu ya 5 kwa ubora,unajua ni kwanini!?ni uwezo wa klabu husika kushiriki katika michuano,wanachama,malengo,uwezo wa uwanjani katika uchezaji na faida inayopatikana.Hata nchi ya Holland haijawahi kuchukua kombe la dunia ila uwezo wa kuushiriki unaifanya nchi hiyo isitoke 5 bora kwa mlongo mzima sasa.
Kumbe kuchukua kombe si silaha pekee ya mafanikio hata uwezo waushiriki hufanya klabu kuwa bora.Kwa mlongo sasa klabu za SImba na Yanga ni klabu za hatua za mwanzo katika michuano ya kimataifa.Na hamna mwaka tunaokosa visingizio achana na ndoto za kombe.

kuwalundikia vilabu hivi udhamini ili viongozi wao watajrike ni kuua Klabu nyingine kutokana na sababu zifuatazo:-
1.Kila mchezaji nchi hii atakuwa na malengo ya kucheza Simba au Yanga kwa sababu ndio klabu zenye uwezo wakati wanaenda kuua vipaji vyao.kumbuka wachezaji wa timu za mikoani wanashindwa kukaa katika vilabu vyao ugumu wa maisha,mfn AFC Arusha

2.Wimbi la uongezekaji wa rushwa lazima liongezeke kwani tofauti ya klabu za Vilabu hivyo na vilabu kama Villa Squad,Toto Africa utakuwa mkubwa na hamna mchezaji atakayekataa hongo nzuri kwa mapenzi ya soka wakati hana hela mfukoni.Mfn Siang'a alishairi hajui uwezo wa wachezaji wake kutokana na ununuzi wa mechi.

3.TFF ilishakiri haina uwezo wa kupandisha timu nyingi ligi kuu kwani nyingi hazina uwezo kiuchumi,kwahiyo tutabakia kuona klabu tajiri na si vilabu vyenye uwezo wa soka

Wasiwasi wangu ni kuwa fedha hizo ni asilimia 10% zitanufaisha wachezaji zilizobakia ni wajanja wa vilabu,kama huamini kawaulize wachezaji wa simba walipata Tshs ngapi baada ya mechi na TP Mazembe wakati klabu llilingiza mil 202 baada ya mgao.Je ni Kaburu na Rage walijaza mashabiki lukuki Taifa!? sjui

Sina nia mbaya na TBL ila kuna ulazima TFF kusimammia udhamini ili tuone vipaji vingine,angalia JKT ruvu na Mtibwa zilivvyolisha Simba na Yanga mafundi,lakini zisipopewa udhamini klabu hizo zitakufa na tutakosa mafundi kama ilivyokufa prosons na hatuoni tena Primus Kasonzo,Oswald Morris na Henry Morris,Godfrey Bonny'Ndanje'.

Mbona Zanzibar huwezi sikia Safari lager inadhamini michuano?ni sheria zinalinda,basi hata udhamini nao ungelenga na gaiwo kwa vilabu vingine tuone ushindani wa kweli kama msimu wa ligi ya 2010/2011

Kuna ulazima ya kikao cha wanahabari wa tasnia ya michezo kutoka vyombo tofauti kuufacha kikao na TFF,kam watafunga masikio ni sawa ila ujumbe ufike

Mtiifu wa soka bongo,
Patrick Semiono

No comments:

Post a Comment