Search This Blog

Sunday, August 28, 2011

Tottenham 1-5 Manchester City: Dzeko afunga manne huku City wakitawala kila idara.


Timu zilizoanza.
Manchester City kwa mara nyingine wameonyesha ‘perfomance’ ya hatari ambayo imewapa matokeo ya asilimia 100% kwenye msimu wao .


Harry Redknapp alilazimika kuwatumia Niko Kranjcar na Luka Modric katikati ya uwanja huku Peter Crouch akisimama peke yake mbele.
Kwa upande wake Roberto Mancini alimpa Samir Nasri mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa Man City akichukua nafasi ya James Milner huku Nigel De Jong akikosekana kutokana na kuwa majeruhi.
City walitawala kila idara ya uwanja kwenye mchezo huu mwanzo hadi mwisho na hata matokeo yalionyesha hivyo.

City wanatawala kipindi cha kwanza.

Kipindi cha kwanza kilianza taratibu mithili ya mchezo uliowahi kuanza kwa wachezaji na mashabiki .
Ulikuwa mchezo ambao ulionekana kama mchafu kwa upande mmoja na hilo lilidhihirika kwa kadi za mapema zilitoka kwa pande zote mbili na pale ulipotulia City walishika hatamu na kutawala.
Huku timu zote zikionekana kucheza mchezo unaofanana kimfumo , ufanano huu ulionekana kwa jinsi walivyokuwa wanawatumia wachezaji wa pembeni, Spurs walikuwa na mawinga tena wa kizamani ambao walikuwa wanatambaa na chaki wakiwakabili mabeki wa pembeni na wachezaji wa Pembeni wa City Samir Nasri na David Silva walicheza pembeni lakini mara nyingi sana waliingia ndani kuomba na kutoa mipira na walichangia kujenga ‘move’ nyingi sana za timu yao.

Wakati mwingine inaweza kuwa tatizo unapochezesha mawinga wenye kawaida ya kuingia ndani kwa kuwa wanakuwa na mchezo unaotabirika huku wakiwa wanaufinya uwanja na wakati mwingine pia inapunguza eneo la uwanja ambalo linatumika kwa muda mrefu huku mabeki wa pembeni wakipata nafasi kubwa ya kupandisha timu.
Hili halikuonekana kwenye mchezo kwa kuwa Spurs walikosa kiungo mkabaji , sit u kiungo bali hawakuwa na mchezaji yoyote wa eneo la kati mwenye asili ya ulinzi . Tom Huddlestone alikuwa fit lakini alikuwepo bench na wakati Modric na Kranjcar walikuwa wazuri kwenye umiliki waliacha nafasi kubwa sana nyuma yao.
City waliwatumia Nasri na Silva , wote walisogea kwenye nafasi iliyoachwa wazi na wachezaji hawa wawili wa Spurs toka Croatia na waliidhuru Spurs tangu mwanzoni kwa nafasi ambazo City walianza kuzipata mfano kwenye dakika ya 7 kwa Silva na wakati Aguero alipokuwa anshuka mpaka katikati mwa uwanja Spurs walipata tabu sana .
Nasri hakuwa anaingia ndani mara kwa mara . Nasri alikaa eneo la kushoto wa uwanja lakini alicheza tofauti kidogo na alivyokuwa akicheza wakati yuko Arsenal, mara nyingi alikuwa akikimbia mpaka kwenye mstari na kupiga krosi , wakati mwingine akibadilisha miguu.

Mabao mawili ya City yalipikwa na Nasri ambaye pia ‘ ali-link’ vizuri sana na Gael Clichy ambaye wamezoeana tangu Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa.

Kipindi cha Pili.

Redknap alijaribu kumiliki mchezo hasa eneo la kati ambako alimuingiza Tom Huddlestone ambaye kwa upande wake alifanya kazi nzuri ya kuwalinda mabeki wanne ,City waliendelea kuwa timu bora na Dzeko alitupia bao linguine na kumaliza Hat-trick yake na Aguero alifunga bao safi ambalo kwa mara nyingine lilipikwa na Nasri.
Tatizo kubwa la Tottenham lilikuwa jinsi City walivyoziona na kutumia nafasi nyingi zilioachwa wazi na Spurs .Spurs Walilazimika kumtoa Modric na kumuingiza Jake Livemore ambapo kidogo mchezo ulianza kurudi kwa Spurs lakini ilipunguza mashambulizi ambayo kwa sasa yalikuwa yanaongozwa na Jermaine Defoe ambaye mara nyingi alikuwa akijipia nafasi mwenyewe .
Kiukweli mchezo ulimalizwa na bao la Dzeko la dakika ya 55 na kipindi cha pili hakikuwa na ladha yoyote . Dzeko alicheza vizuri sana , alionekana kuwa kwenye kiwango bora kabisa na akiwa anajiamini vibaya.


Muda wote wa mchezo alikuwa anaongoza mashambulizi ya City ambayo yalionekana kuleta hatari kwa Spurs na alikuwa na majaribio (goal attempts) 10 kwenye mchezo wote.
















Mwisho
Ulikuwa mchezo ‘excellent’ kwa City ambao waliwatumia vyema wachezaji watatu wabunifu kwenye timu yao.Mtu aliyefaidika na wachezaji hawa alikuwa Edin Dzeko ambaye kwa kutabiri ana nafasi kubwa sana ya kuwa mfungaji bora wa City na wa ligi kwa ujumla kutokana na ‘service’ anayopata.
Mipira ilipenya kwenye defence ya wapinzani , kulikuwa na krosi na pasi nyingine za aina nyingi sana . Kiukweli City wana silaha nyingi za maangamizi kwenye sehemu ya ushambuliaji.
Tottenham walikuwa kirahisi sana na kurahisisha kazi ya City na pia wachezaji wabunifu wa Spurs walishindwa kuja mchezoni.

No comments:

Post a Comment