Search This Blog

Monday, August 29, 2011

Manchester United 8-2 Arsenal: Kipigo kizito kuliko vyote kwa Wenger kwenye maisha yake ya ukocha.

Timu zilizoanza.
Hakika ulikuwa mchezo wa kushangaza kwa matokeo yalitokea hadi mwisho .
Sir Alex Fergusson alianza na kikosi kile kile ambacho kiliwafunga Tottenham siku ya jumatatu na Danny Welbeck aliendelea kupangwa mbele akiwa na Wayne Rooney.
Arsene Wenger aliwakosa ThomasVermaelen na Bacary Sagna na ukiongeza wachezaji wanaokosekana kwa majeruhi na kufungiwa, hii ilimaanisha kuwa Carl Jekinson alicheza kama beki wa kulia na Johan Djorou alicheza kati na Francis Coquelin alipata nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza akianzia kwenye nafasi ya kiungo.
Mchezo huu ulikuwa kama wa kujifurahisha kwa Man United kwa jinsi walivyokuwa wanatengeneza nafasi na kuutawala. Arsenal walikuwa wameharibika toka mwanzo hadi mwisho huku wakishindwa kutumia wingi waliokuwa nao katikati mwa uwanja ambako walikuwa wamejaza wachezaji wengi kuliko United na pia walionekana kukosa mpangilio kwenye safu ya ulinzi.

Ulinzi/Beki

Unaanzia wapi kuchambua safu mbovu ya ulinzi ya Arsenal? Ni vigumu sana kutazama ubao wa matokeo unaoonyesha mabao 8-2 na kuanza kueleza sehemu moja baada ya nyingine yenye matatizo yaliyosababisha kipigi kama hicho kwa ‘Ze Ganaz’.
Walikuwa hovyo sana kiasi kwamba unaweza kufikiria hawakuwa wamejiaandaa kwa ajili ya kushindana , na utakuwa sahihi ukifikiri kuwa shida ya Arsenal haipo kwenye mbinu za mchezo bali zinaanzia mbali sana zaidi ya uwanjani ambako jumapili ya tarehe 28 /8/ 2011 wamefungwa mabao 8.

Hiyo siyo kusema kuwa hakuna matatizo ya kiufundi ,kwa kuanza tu , Arsenal walikosa umoja hasa pale ambako walikuwa hawana mpira . Baadhi ya wachezaji walionekana wanafanya vyema kazi ya ‘pressing’ yaani kumsukuma adui lakini wengine ni kama walikuwa wamesimama tu . Ulikuwa mchezo mkubwa na mgumu sana kwa kijana mdogo Coquelin ambaye alicheza kama kiungo wa chini akiwa na jukumu la kumkaba “ng’ombe pori” Wayne Rooney.

Cha kushangaza ni kwamba pamoja na kwamba Wayne Rooney alifunga ‘hat-trick’ Coquelin alifanya kazi yake vizuri. Kazi hii nzuri inatokana na ukweli kuwa ‘influence’ ya Wayne Rooney kwenye kipindi cha kwanza ilikuwa ndogo hasa kwenye jukumu la Rooney la kuufungua mchezo kwa wenzake.

Na kingine ni kwamba mabao yote ya Rooney yalitokana na mipira iliyokufa na si kwenye ‘open play’. Uamuzi wa Wenger kumtoa Coquelin wakati Arsenal wakiwa nyuma kwa 3-1 kwenye dakika ya 61 ulionekana kuwa na matokeo mabaya sana kwa Arsenal.
Hilo ndilo jambo pekee ambalo lilienda sawa kwa Arsenal. Tatizo la kushindwa kufanya ‘pressing’ ya maana lilimaanisha kuwa Arsenal walikuwa hawafanyi presha yoyote kwenye mpira hasa kwenye ‘midfield’ pamoja na kwamba walikuwa na mchezaji ( Coquelin) ambaye alikuwa amekaa kwenye ‘midfield’, kwa sababu Aaron Ramsay na Tomas Rosicky wangeweza kumkaba Anderson pamoja na Tom Cleverly.

Hili lilishindikana na Viungo hawa wawili wa United walikuwa wanamiliki mpira watakavyo na walikuwa wakipiga pasi wapendavyo.

Tatizo la pili lilikuwa kwenye mstari wa juu wa ‘defense’ ambao Arsenal walikuwa wanatumia kujilinda , kwa kawaida kukaba kwa mstari huu ni kama kujipiga risasi au kunywa sumu hasa pale inapokosekana presha ya kutosha kwenye mpira – lakini kikubwa ni jinsi wachezaji wanne wa safu ya ‘defense’ ya Arsenal walivyokosa umoja baina yao.


Wachezaji wawili mara zote walisogea juu na wengine wawili walibaki.
Wakati mwingine ilikuwa Ajabu jinsi United walivyopenya kwa urahisi na kufunga – bao la Nani ni mfano mzuri.


Nyakati Nyingine Arsenal wangemuacha beki mmoja akiwa amenasa nyuma ya wenzake na kulazimika kufanya ‘tackling’ ya mtu wa mwisho –Mchezaji aliyetolewa kwa kadi nyekundu Carl Jenkinson alikuwa mfano mzuri wa hili na hata kadi mbili za njano ambazo zilipelekea nyekundu alizipata kwa mtindo huu.

United walicheza soka la kupendeza machoni,na kiwango cha umaliziaji wao kilikuwa bora muda wote , lakini hawakuwa na haja ya kucheza vizuri kufanya maangamizi waliyoyafanya .

Pasi nyingi zilitembea kwa United kuliko kwenye mchezo uliopita dhidi ya Spurs na hata kwenye mchezo wa ngao ya jamii.
Baadhi ya magoli (mfano la Ji sung park na la Welbeck) yalikuja kwa sababu ya Arsenal kuruhusu muda mrefu na nafasi kubwa kwa wachezaji wa United kuanzisha na kumaliza’move’.


Mabao matatu ya Rooney yalikuja kwa jinsi Arsenal walivyokuwa wanatoa faulo nyingi kwa jinsi walivyokuwa wanajitupa kwa wachezaji wa United wakijaribu kuwakata kasi wakiwa kwenye ‘move’.

Mabao ya Young yalikuwa mazuri lakini kama yangekuwa ndiyo mabao pekee tungekaa hapa na kuhoji kwanini mchezaji anayetumia mguu wa kulia anayecheza upande wa kushoto alipewa nafasi ya kuingia ndani na kuhamishia mpira kwenye mguu wake wenye nguvu (wa kulia) na kufunga kirahisi . Karibu kila kitu kilikwenda hovyo kwa Arsenal.

Makosa ya msingi.

Kitu cha kushangaza kwenye ubao uliopo hapo chini ni kwamba sehemu za msingi kabisa ambazo mtu yoyote aliyewahi kucheza hata mechi moja tu ya mpira angeweza kukifanya kwa Arsenal zilikuwa hovyo.

Arsenal walichezewa kila mahali. United walifanya ‘tackling’ zenye mafanikio kwa asilimia 64% na Arsenal walifanya ‘tackling’ kwa asilimia 45 % tu.
Mfano mwingine ni kwamba pamoja na mpira kuwepo kwenye eneo la mita 18 la Arsenal , United waliweza kuzuia mashuti 6 na Arsenal walizuia 8 tu.

Kufanya ‘tackling’ na kuzuia mashuti si kitu kigumu au cha ajabu ambacho kinahitaji kufundishwa naMalaika toka Mbinguni ili kieleweke, sawa siyo mchezo wa Arsenal lakini pale unapokuwa unamiliki mpira kwa asilimia chache ni vizurri kuwa na mabeki ambao takwimu zao za ‘tackling’ na kuzuia mashuti ni nzuri.

Unapokuwa na timu ambayo haisimamishi mstari wa ‘off-side’ , ambayo haimiliki mpira na inawapa wapinzani mwanya wa kucheza ni lazima ufungwe na ndicho kilichotokea kwa Arsenal.

Mwisho.

Sehemu ya mchezo huu kwa maneno rahisi ni kwamba Arsenal hawakuwa na wachezaji waliokuwa ‘fit’ kuikabili timu kama Manchester United .
Hii ni kwa sababu ya kukosa uzoefu na wengine walikuwa wachezaji wasiojengwa kwa ajili ya michezo kama hii.


Laureant Koscielny alimaliza akiwa na asilimia 100% kwenye umaliziaji wa pasi zake. Lakini bado alikuwa anakamatwa sana eneo la juu la uwanja mahali ambako kwa hali ya kawaida beki hapaswi kuwa kwenye eneo kama hilo.
Carl Jenkinson alikuwa mchezaji bora kwa Arsenal kwa muda aliokuwa uwanjani na ndiyo maana Arsenal walikuwa nyuma kwa mabao macheche alipokuwa uwanjani lakini Tsunami ikawaangukia alipotoka na hata aliweza kutoa ‘assist’ moja lakini bado hakuweza kufanya ‘tackling’ hata moja .

Ramsay na Rosicky ni watengenezaji na si waharibifu na kwa mchezo wa leo Arsenal walikuwa wanahitaji mtengenzaji mmoja na muuaji mmoja ili ‘kubalance’ hesabu za midfield na kuwatumia wachezaji hawa ni lazima uumiliki mchezo lakini Arsenal hakuwa na umiliki wa mchezo huu.

United bado wanaendelea na mwanzo wao mzuri kwenye ligi japo hata wao lazima watakuwa wameshangazwa na jinsi mchezo huu ulivyokuwa rahisi kwao . Mfumo wao wa 4-4-2 ambapo washambuliaji wawili walikuwa wanashuka mpaka ndani unawapa nafsi ya kutengeneza’runs’ za kuelekea mbele na wanashambulia kwa pande tofauti za uwanja na si upande mmoja kama zamani na walikuwa hatari sana kwa sababu hii.

No comments:

Post a Comment