Search This Blog

Friday, August 19, 2011

PREVIEW: ARSENAL VS LIVERPOOL

Siku zote mechi kati ya timu hizi mbili huwa za kusisimua sana . Kumbuka bao la kusawazsiha la Dirk Kuyt kwenye dakika ya 112 mwezi aprili , bao ambalo lilimaliza kabisa matumaini ya Arsenal kwenye mbio za ubingwa kwa msimu uliopita , ukiacha bao hilo la Dirk Kuyt kuna kosa alililofanya Pepe Reina kwenye mchezo wa raundi ya kwanza kosa lililoipa Arsenl pointi moja kwenye mchezo wa kwanza wa Roy Hodgson msimu uliopita .

Hakuna atakayesahau mabao manne ya Andrey Arshavin kwenye sare ya 4-4 kwenye uwanja wa Anfield mwaka 2009, mchezo wa Jumamosi unaweza kutazamwa kama mchezo wa kuwania nafasi ya 4 na timu zote mbili zina mengi ya kufanya ili kuridhisha mashabiki wake .

Liverpool inatarajiwa kuwatumia Dirk Kuyt na Martin Kelly kwenye upande wa kulia wa kiungo na beki,haya yakiwa mabadiliko tofauti na kikosi cha wiki iliyopita ambapo Liverpool ilianza na Jordan Henderson na John Flanagan kwenye upande wa kulia .

Zaidi ya hapo Kenny Dalglish anatarajiwa kuchezesha kikosi kile kile ambacho kwa kutazama kipindi cha kwanza cha mchezo dhidi ya Sunderland kilicheza vizuri sana lakini kikaja kufunikwa kwenye kipindi cha pili .
Liverpool inataraji kutumia mfumo rahisi wa 4-2-3-1 au wa 4-4-1-1 ambao unampa Suarez ‘free role’ kuzunguka uwanja mzima akitafuta nafasi. Kwa upande mwingine wachezaji wapya Stewart Downing na Jose Enrique wanajaribu kujenga’patnership’ kwenye upande wa kushoto na Lucas Leiva na Charlie Adam wanategemea kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwenye sehemu ya katikati mwa uwanja japo Dalglish ana watu wengine ambao anaweza kuwachagua kina Jay Spearing , Raul Meireles Jordan Henderson na Alberto Aquilani ambao wako kikosini.


Jammie Caragher na Daniel Agger wako katika kwenye nafasi zao kama mabeki wa kati wakimpa ulinzi kipa Pepe Reina.
Arsenal wana sababu chache za kuwa na matumaini kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Liverpool.


Ukiacha kumuuza aliyekuwa nahodha wao Cesc Fabregas kwa Barcelona huku Samir Nasri akiwa anafungasha kilicho chake akielekea Man City Arsenal wanaandamwa na issue ya majeruhi na baadhi ya wachezaji kufungiwa . Wenger anaingia kuwavaa Liverpool huku akiwakosa Abou Diaby , Alex Song , Gervinho, Johan Djorou , Jack Wilshere, Kieran Gibbs na Armand Traore.
Hii inamaanisha kuwa Arsenal watalazimika kumtumia Emmanuel Frimpong kiungo mwenye miaka 19 kuziba pengo la Alex Song anayelazimika kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu kwa kumkanyaga Joey Barton.Pamoja na Frimpong Arsenasl watalazimika kumpa mchezaji mpya Carl Jenkinson mechi yake ya kwanza akichukua nafasi ya Kieran Gibbs ambaye ameumia.


Andrey Arshavin na Theo Walcott wataanza kama viungo wanaoshambulia toka pembeni mwa uwanja japo Wenger amesema kuwa anaweza kuwatumia wachezaji wapya Alex Oxlade Chamberlain na Ryo Miyachi .
Riyo Miyachi ni winga toka Japan mwenye miaka 18 ambaye amekuwa akicheza kwa mkopo huko Feyenord Rotterdam na ana uwezo mkubwa huku akitumia sana mbio zake kama silaha yake kuulakini kama ambavyo imezoeleka kwa Arsenal mchezaji huyu ni kipaji ambacho hakijakomaa wala hakina uzoefu wa kutosha , hivyo anaweza kupewa nafasi ya kuingia toka benchi kuwakimbiza kina Martin Kelly na Jose Enrique.
Kwa macho ya haraka miundo ya timu hizi mbili inafana . Ila tofauti zipo ., Kwanza ni upande wa Luis Suarez ambaye kwa hakika lazima ataelekezwa kukaa sana upande wa juu wa uwanja ili kumuepuka Aron Ramsay , katika hali itakayosababisha Liverpool ionekane kama inacheza 4-4-2, huku Ramsay kwa upande wake atalazimika kuingia ndani kwenye ‘midfield’ ili kuipa Arsenal shape ya 4-3-3 wakiwa hawana mpira .


Mawinga wa Liverpool (kuyt na downing) pia watalazimika kushuka sana wakati timu yao ikiwa inalinda kwani Dalglish anapendelea sana kutumia mabeki wanne akiwa analinda . Walcott na Arshavin hawatakimbia sana nyuma kulinda kitu ambacho kinaweza kuwalazimu mabeki wa pembeni wa Liverpool (Enrique na Kelly) wawe macho na waegemee sana kwenye kulinda na si kupanda hali itakayowanyima Liverpool mashambulizi mengi ya pembeni .

Battle za pembeni mwa uwanja zinaweza kuwa muhimu kwenye mchezo huuhasa kwenye winga ya kulia ya Liverpool ambako Dirk Kuyt atapambana na Carl Jenkinson mchezaji ambaye amewahi kucheza mechi nane tu za ligi yoyte kwenye maisha yake ya soka (zote akiichezea Charlton Athletic kwenye ligi daraja la kwanza)Beki huyu aliingia kwenye dakika 20 za mwisho dhidi ya Udinese na japo baadhi ya mashabiki wa Arsenal walifurahishwa na kiwango chake alifanya makosa kadhaa ambayo yalitokana na uzoefu mdogo na Kenny Dalglish hakika atawaelekeza wachezaji wake watumie sana upande wake.
Tomas Rosicky amewahi kucheza kwenye upande wa kushoto wa midfield ya Arsenal kwenye michezo miwili ya mwisho ya timu yake lakini si mchezaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kulinda wala hana kawaida ya kurudi nyuma kusaidia wakati timu inashambuliwa na unaweza kusema hivyo hivyo kwa upande wa Andrey Arsharvin hivyo bwana mdogo Jenkisnon atajikuta mwenyewe kwenye upande wa kushoto .


Hapa ndio ile ‘free role’ ya Luis Suarez inapoweza kutumika na kuwa na madhara makubwa kwa Arsenal.Kwa vyovyote atakuwa anakimbilia upande wake wa kulia ili yeye na Kuyt wafanye ‘double team’’ kwa Jenkinson na kuiletea Arsenal matatizo.

Kama hii italazimu Arsenal kumtumia beki wake anayekuwa upande wa kushoto kwenye ‘central defensive patnership’ Thomas Vermalaen kusogea upande wa kushoto kumsaidia Jenkinson atakuwa anaacha shimo kubwa ambalo litakuwa nafasi muhimu kwa Andy Caroll au kiungo yoyote wa kati kama Charlie Adam kuingia na kuleta matatizo.
Arsenal walikuwa hatarini sana kufungwa kwenye hatua za mwisho za mchezo wao dhidi ya Udinese siku ya jumanne .


Pia dhidi ya Newcastle waliwaruhusu viuongo wao wa kati kuingia sana ndani kwenye nusu ya Newcastle huku wakiwa na matarajio kwamba mmoja wao atabaki na kuwa mlinzi wa mabeki .

Idea hii ya ‘total football’ iliwahi kufanya kazi msimu uliopita kwa Jack Wilshere na Alex Song ambapo wachezaji hawa walijenga uelewano mkubwa kati yao, ila kwa Udinese ilionekana kushindikana kidogo hasa kwa sababu Wilshere hakuwepo na Udinese waliweza kuingia kwenye nusu ya Arsenal wakiwa huru sana kwenye eneo la katikati huku wakiiweka defense ya Arsenal katika hali ya 2-vs-2 na 4-vs-4 .

Kwa mara nyingine Luis Suarez ana uwezo mkubwa sana wa kuwaletea madhara Arsenal kwenye hali kama hii akipata nafasi ya kuwakimbia mabeki .
Kitu kingine ambacho Arsenal imekuwa ikikifanya ni kuweka mstari wa ulinzi ambao unalinda kuanzia eneo la juu na hik ni ktu ambacho kinatarajiwa kurejewa kwenye mchezo dhidi ya Liverpool ili kujaribu kuuza makali ya Andy Caroll amnaye watahakikisha kuwa wanahimili mipira ya juu ambayo ndio silaha yake kubwa .


Mstari huu ambao unakabia juu ulipitwa kirahisi sana na na wachezaji wa Udinese Kwadwo Asamoah na Pablo Amero na mara zaidi ya moja kipa Wojciech Szczesny alilazimika kutokea ili kuokoa . Hili ni suala ambalo Liverpool watalitumia kama udhaifu kwa wapinzani wao.
Liverpool pia wana sababu za kuwa na wasiwasi na timu yao .


Wachezaji wapya bado wanahitaji muda zaidi kuzoea mazingira ya timu taratibu nah ii inamanisha kuwa watahitaji zaidi ya mechi mbili ili kuwa na ‘match fitness’ jambo limeonekana kuwa tatizo kubwa . Pia wanahitaji kufanyia kazi uwezo wao wa kuupata mpira pale unapopotea jambo liloonekana kuwa tatizo jumamosi iliyopita walipocheza na Sunderland .

Liverpool walimaliza mpira wakiwa na asilimia 39% ya umiliki wa mpira kwenye mara ya mwisho walipocheza na Arsenal na kwa soka lao ambalo ni la moja kwa moja wanaweza kupata tabu kwenye ‘ball possesion’ .

Kwenye mchezo ambao timu hizi mbili zilitoka sare ya 1-1 mwezi aprili goalkick nyingi alizopiga Pepe Reina alizielekeza kwenye kichwa cha Andy Caroll.
Kama mbinu ya kumtumia Andy Caroll kama Targetman haitatumika ipasavyo Liverpool watakuwa wanapoteza sana mpira kwa timu ya Arsenal ambayo inajua jinsi ya kumiliki mpira kwani ndio silaha yake kubwa .

Kama Liverpool haitamiliki mpira vya kutosha uwezo wa kupiga pasi za mbali wa Charlie Adam na krosi za Stewart Downing hautakuwa na faida yoyote .
Kama Liverpool hawatakuwa na mpango thabiti wa kumiliki mpira na kutengeneza nafsi wataonekana kupoteana kama walivyoonekana kwenye mchezo dhidi ya Sunderland . Arsenal wana mapungufu makubwa sana kwenye safu yao ya ulinzi na Liverpool wana kia sababu na uwezo wa kutumia mapungufu haya kwa faida yao lakini wanapaswa kuutazama mchezo wao dhidi ya Sunderland ili kutimiza hilo .

1 comment:

  1. ARSENAL tunakubali kikosi che2 akiko sawaaa but liveerr hiyoo keshoo wataisomaaaaaaa, 2makila sababu ya kumfunga liver japo majeruhii wengiiiiiii.

    ReplyDelete