Search This Blog

Thursday, August 11, 2011

MUTU AFUNGIWA SOKA MAISHA ROMANIA


Msahmbuliaji wa klabu ya Casena ya Italia Adrian Mutu amefungiwa kwa maisha kuichezea timu ya taifa ya Romania baada ya kugundulika kutumia pombe usiku wa kuamkia mechi ya kirafiki dhidi ya San Marino.

Adhabu hiyo pia imemkumba beki wa West Brom Albion Gabriel Tamas ambaye alikuwa na Mutu kipindi wakigonga kilaji.

Romania iliifunga San Marino 1-0 kwenye mechi yao kirafiki jana Jumatano, wachezaji wote wawili waliondolewa kwenye kikosi kabla ya kick off baada kutolewa kwenye vyombo vya habari zikisema walikwenda kulewa pombe usiku wa Jumatatu katika Pub ya Crawl.

Baada ya mchezo huo, Kocha wa Romania Victor Piturca alielezea sababu ya adhabu hiyo.

“Wachezaji hawa wawili wamefungiwa kwa maisha kwenye timu ya taifa, ni huruma lakini ni sheria inabidi tuzifuate, walitakiwa walitambue hilo.”

Mutu nae alijibu baada ya kuambiwa amefungiwa, “Tumeuelewa uamuzi wa Piturca.”

No comments:

Post a Comment