Search This Blog

Tuesday, August 23, 2011

Man United 3-0 Tottenham: Movement za kipindi cha pili ziliipa United nguvu na Ushindi.

Timu zilizoanza.

Manchester United wamewafunga Tottenham 3-0 kwenye mchezo wa kusisimua na kuburudisha ambao ulimalizika kpindi cha kwanza huku timu zote zikiwa zimetoshana kwa karibu kila sehemu.

Sir Alex Ferguson alitumia wachezaji sita wa mbele wale wale aliowatumia kwenye mchezo dhidi ya Man City japo alifanya mabadiliko kadhaa upande wa ulinzi ambako United walionekana kukosa uzoefu.

Luka Modric hakuwepo kabisa hivyo Mcroatia mwenzie Niko Kranjcar alicheza kwenye nafasi yake akiwa na Jake Livemore

Ulikuwa mchezo ambao ulijaa burudani ya hali ya juu . Timu zote hazikuwa na washambuliaji wanaosubiri/wa kusimama wala hazikutumia viungo wakabaji na badala yake safu za kiungo na ushambuliaji ziliegemea kwenye ufundi na ubunifu ambao kwa ujumla ulitoa burudani kubwa ya soka.

Ball Possession

Game ilizunguka sana kwenye uwezo wa timu mbili kumiliki mpira . Uwanja ulikuwa wazi na viungo wa timu zote mbili walimiliki mpira kwa kiasi kikubwa wakicheza kama timu na ni kama walipeana zamu kushambulia na kuufungua mchezo .

Huku timu zote zikitaka kupasi mpira , viungo wa kati walijikuta wakiingia ndani na kuwakimbia wapinzani wao ili kumiliki mpira kwenye nafasi . Tom Cleverly na Jake Livemore wote walisogea karibu na mabeki wa wa kati kuchukua mipira na waliisambaza kwa ubunifu mkubwa.

Anderson alionekana kuwa na haraka kuliko wenzie mwanzoni na pasi zake zilikuwa za haraka haraka sana muda wote akiwa na malengo ya kuwahisha mpira mbele huku Kranjcar akiuchezea mpira sana lakini bila matunda nah ii inatokana na ukweli kuwa Kranjcar ni mchezeaji mzuri wa mpira lakini si kiungo wa kati .

Nafasi

Kwa upande mmoja mchezo huu ulionekana kama wa kizamani kimtindo. Timu zote zilichezesha makundi ya mabeki wanne , mshambuliaji mmoja anayemchezesha mwenzie kwa ubunifu na mwingine mwenye kasi.

Battle kwenye ‘midfield’ ilikuwa ya wazi sana huku viungo wa kati wakiingia ndani na kupanda mbele kuwabana wapinzani , hapa ilibaki nafasi kubwa sana eneo la kati ya mabeki na viungo , hali hii iliwafanya Wayne Rooney na Rafael Van Der Vart wacheze kwa starehe sana.

Hakuna timu yoyote iliyopata faida kutokana na hali hii ya uwanja kuwa wazi kama walivyopaswa kufanya japo ilionekana wazi kuwa ‘macentre half’ Johny Evans na Michael Dawson walipandwa na mzuka wa kutoka kwenye maeneo yao na kufuta mipira huku wakicheza rafu wakati mwingine.

Mabeki wa Spurs walikuwa na kazi kubwa kuliko wenzao nah ii ilikuwa kwa sababu ya ‘movement’ za kijanja za Man United hasa kwa wachezaji wanne wa mbele ambao walikuwa wamepanda sana huku Rooney na Welbeck wakisogea mpaka pembeni mwa uwanja na Ashley Young na Luis Nani wakiingia ndani.



Magolikipa

Moja ya vitu vya kufurahisha kwenye mchezo huu ilikuwa tofauti baina ya makipa wa timu zote. David De Gea mwenye umri wa miaka 20 na Brad Friedel mwenye miaka 40. Friedel alitia fora kuliko mwenzie kwani alionekana kuwa na sifa halisi za kipa ukiachilia mbali matokeo , lakini De Gea alivutia kwa uwezo wake mkubwa wa kutoa mipira yaani ‘Distribution’ labda kwa kuwa yeye anatokea kwenye kizazi cha magolikipa ambao ugawaji wa mipira tokea nyuma ni jukumu muhimu na si la ziada kama ilivyokuwa wakati Friedel alipokuwa na umri kama wa De Gea.








Magolikipa
Moja ya vitu vya kufurahisha kwenye mchezo huu ilikuwa tofauti baina ya makipa wa timu zote. David De Gea mwenye umri wa miaka 20 na Brad Friedel mwenye miaka 40. Friedel alitia fora kuliko mwenzie kwani alionekana kuwa na sifa halisi za kipa ukiachilia mbali matokeo , lakini De Gea alivutia kwa uwezo wake mkubwa wa kutoa mipira yaani ‘Distribution’ labda kwa kuwa yeye anatokea kwenye kizazi cha magolikipa ambao ugawaji wa mipira tokea nyuma ni jukumu muhimu na si la ziada kama ilivyokuwa wakati Friedel alipokuwa na umri kama wa De Gea.









Upigaji wa Friedel ulikuwa mbovu kwa kiasi fulanina wakati ambapo Jermaine Defoe alipokuwa anabaki mbele mwenyewe Spurs walikuwa wanashindwa kuwa hatari kwa kutumia mipira ya juu, hivyo wanayanfa wapinzani wao kuwasukuma wakati Friedel ana mpira na kumlazimisha apige mipira mirefu ambayo mara nyingi ilikuwa inapotea.

Gareth Bale ni mzuri hewani na anakuwa muhimu kwenye hali kama hii hivyo United walikuwa na bahati ya kumtumia beki wa kati anayecheza pembeni ( Chris Smalling) dhidi ya Bale ambapo Smalling alikuwa anampa tabu Bale kwenye mipira ya juu. Chris Smalling pia alizuia mipira anayopenda kuipiga Dawson kwa Bale.



Kipindi cha Pili.

Kipindi cha pili kilionekana kama kingeamuia na Wayne Rooney au Rafael Van Der Vart, kutokana na jinsi walivyokuwa wanajikuta kwenye nafasi .

Mwishowe ilikuwa Rooney . Kuna kipindi alianza kuingia ndani karibu kwenye dakika ya 30 hivi , lakini baada ya mapumziko alianza kuuendesha mchezo akipiga pasi za hatari kwa kina Cleverly na Andersonambao walikuwa wanaingia toka kwenye eneo la kati na kugawa mipira pembeni ili zipigwe krosi.

Hali hii ilisaidiwa na ukweli kuwa Michael Dawson alikuwa na kadi ya njano hivyo alijikuta akicheza kwa uangalifu hali iliyowafanya United kufaidika kwa kuwa Dawson alikuwa anacheza kwa woga .


















Van Der Vart alikuwa kwenye nafasi nzuri mara nyingi lakini washambuliaji wengine wa Spurs walishindwa kumtafuta , kwa mfano wakati ambapo Aron Lenon angeweza kurudisha mpira nyuma lakini akachagua kuendesha mpaka kwenye 6.

Spurs waliwakamata United kwenye 4v4 mara zaidi ya moja lakini maamuzi kwenye ‘final third’ yalikuwa mabaya.
Redknap alicheza kamari kwa kumchezesha mtu asiye fit Tom Huddlestone na Roman Pavluychenko pia wakati wakiwa nyuma , ambapo Harry aliwatoa viungo wake wa kati.


Hii iliufungua mchezo na kuuweka mikonini mwa United . Redknap angeweza kuwa na tahadhari kidogo wakati akijaribu kurejea mchezoni –Spurs walionekana kuchoka na United walianza kufunga zaidi hali iliyofanya mchezo uonekane tofauti na ulivyokuwa mwanzoni .


Mwisho.

Uwazi wa mchezo ulasababishwa na baadhi ya wachezaji-kulikuwa na makundi mawili ya wachezaji hasa viungo na washambuliaji ambao mara nyingi walitaka kuchezea mipira mguuni kuliko mipira mirefu .

United walionekana kufurahia mchezo hasa ukizingatia kuwa walianza na wachezaji wasio na uzoefu –kiufundi walionekana vile vile walivyokuwa kwenye mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Man City japo hakukuwa na mchengo mkubwa sana toka kwa mawinga wawili.

Spurs watapata moyo kutokana na mchezo huu ambapo kwa dakika 60 walicheza vizuri na wakauwawa kwenye dakika 30 za mwisho, kama Modric akirejea au watakapopata fedha na kuziwekeza kwa mrithi wake watakuwa na kikosi kinachocheza vizuri .

No comments:

Post a Comment