Search This Blog

Monday, August 15, 2011

KING KENNY HAKUWA SAHIHI KUWAANZISHA WACHEZAJI WAPYA WANNE KWA WAKATI MMOJA

Luis Suarez akipaisha penelti ... lakini baadaye kidogo aliipatia Liverpool bao la kuongoza..

The Super Reds wameanza ligi kwa sare dhidi ya Sunderland kinyume na ahadi ambayo usajili wao ilitoa kwa mashabiki wao .

Watu wengi wanahangaika kujiuliza maswali ya Liverpool walifanya nini kisicho sahihi na kuiruhusu Sunderland kusawazisha huku wakiupotezea uwezo wa Sunderland.

Kosa kubwa alilolifanya kocha wa Liverpool mfalme wao Kenneth Daliglish ni kuidharau Sunderland . kivipi? Kenny aliidharau Sunderland kwa kuwapanga tangia mwanzo wachezaji wanne wapya waliosajiliwa msimu huu.

Stewart Downing, Charlie Adam , Jordan Henderson na Jose Enrique. Afadhali kwa kina Adam , Downing, na Jordan ambao angalau walipata nafasi ya kujenga ‘chemistry’ na wenzao kwenye mechi za pre-season lakini Jose Enrique ambaye usajili wake ulikuwa hauna hata siku tatu, kweli Kenny aliteleza hapo .

Labda ni kwa ufahamu wake mdogo wa masuala ya kiufundi ndio sababu kubwa iliyofanya akinyime kikosi chake mambo mengi ambayo yangeweza kuwemo kama angewaingiza wachezaji hawa wapya taratibu na kwa awamu na sio kwa mkupuo kama alivyofanya .

Hakuna asiyefahamu ‘influence’ na ‘spirit’ ya Man United kwenye kikosi cha Sunderland. Hii ni timu ambayo inafudishwa na ‘legend’ wa Man United Steve Bruce , ina wachezaji wasiopungua watano wa zamani wa Man United , Wesley Brown,John O’shea,Phil Bardsley,Kieran Richardson na Frasier Campbell.

Wote hawa wana damu ya Man United na dunia nzima inatambua uhusiano wa Man United na Liverpool na wachezaji hawa wote wamewahi kucheza dhidi ya Liverpool hivyo ni dhahiri wasingekubali kufa kirahisi mikononi mwa Liverpool .

Liverpool ilipokuwa mbele kwa bao moja walionekana kuridhika na wakakubali kukaa nyuma na kuwakaribisha Sunderland waje mpaka kwao ilhali kwenye kipindi cha kwanza walicheza kwa kushambulia mwanzo mwisho.

Stephan Sessegnon kiungo raia wa Benin mwanzoni kwenye kipindi cha kwanza alionekana kuwa nje ya mchezo na ni kwa sababu Sunderland hawakumiliki mpira kwa asilimia kubwa na jamaa huyu ni aina ya mchezaji anayekuwa ‘effective’ wakati timu ikiwa na mpira kwa kuwa yeye ndiye anayeiendesha timu kuanzia eneo la kiungo cha juu.

Sebastian Larsso akishangilia mara tu baada ya kuifungia Sunderland bao la kusawazisha...

Kwenye kipindi cha pili Sunderland walikuja kama mbogo na hapo ndio Sessegnon alionekana kuingia mchezoni dakika mpaka dakika .

Goli la kusawazishwa lililofungwa na Sebastian Larson lilitokana na pasi ya Sessegnon.

Na pia mabeki wa wa Liverpool walimpa ‘room’ kubwa sana mfungaji ya kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga moja kati ya mabao ya msimu .

Kenny Dalglish ana mtihani mkubwa wa kuipanga Liverpool kuwa na kikosi cha kwanza cha kueleweka ambacho kina ‘chemistry’ na maelewano baina ya wachezaji hasa kwenye ‘zone’ ya kiungo .

Ni lazima ajue nini atafanya kwa wachezaji kama Raul Meireles, Charlie Adam,Jordan Henderson na wengine na pia ni muhimu kwake kuwaingiza wachezaji wapya waliosajiliwa taratibu bila kukurupuka ili asiharibu ‘rhythm’ ya timu kwani timu iliyomaliza msimu haikuwa mbaya na kuna kila sababu ya kuendelea pale Liverpool ilikomalizia msimu uliopita badala ya kuanza upya .

1 comment:

  1. well said dauda, lakin kwa mtazamo wangu hunderson ndo asingetakiwa kuanza, kuyt angekuwa effective kama angekuwapo toka mwanzo bse ameshaelewa vizur style ya uchezaj ya liva, flanangan ndo alikuwa a leak kwenye defence. Enrque alikuwa kat ya gud performers kwenye ile game! Aurelio alikuwa mgonjwa so King Kenny hakuwa na option zaid ya jose kucheza game yake ya kwanza ndan ya 24 hours! Ni game ya kwanza so bdo kuna meng ya kurekebisha!

    ReplyDelete