Search This Blog

Thursday, August 11, 2011

FABREGAS KUJILIPIA ADA YA UHAMISHO KWENDA BARCA



Cesc Fabregas yupo katika hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kwenda Barcelona.

Lakini kiungo huyo wa Kihispania itabidi alipe £4.5 kutoka kwenye mfuko .

Arsenal wapo tayri kukubali ofa ya £35.9 kutoka kwa Barcelona lakini watapata nyongeza ya peasa ikiwa Fabregas atashinda mataji makubwa 2@ Nou Camp.

Pia ofa hiyo itahusisha malipo ya £900,000 kwa mwaka ambayo Fabregas amekubali kuilipa Arsenal kutoka mshahara wake kutoka katika mkataba wake wa miaka 5 na Barca.

Kilichobakia kwa sasa ni kwa Fabregas kukubaliana matakwa binafsi ya Catalan club ili kukamilisha sakata la uhamisho huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 3.


Wakati huo huo, Samir Nasri anategemewa nae kuondoka Arsenal kujiunga na Manchester City.

Kiungo wa kifaransa yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Gunners, ingawa kocha wake Arsene Wenger alikuwa anataka kumbakisha lakini mabosi wa Emirates hawapo tayari kuona anaondoka bure msimu ujao.

City wanajitarisha kumlipa Nasri mshahara wa £180,000 kwa wiki huku wakiilipa Arsenal £25m.

Akizungumza na press striker wa Arsenal Marouane Chamakh alisema “Nafikiri wote wawili Cesc na Samir wataondoka ndani ya klabu hii.”

No comments:

Post a Comment