Samuel Eto’o anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya jijini Rome ili kuweza kujiunga na klabu ya Anzhi Makhachkala Alhamisi wiki hii, shirika la habari la Italia ANSA linaripoti.
Mshambuliaji huyo alitegemewa kufanyiwa vipimo vya afya Jumatatu , lakini sasa atasafiri kwenda Rome baadae wiki hii baada ya ratiba ya vipimo vyake kubadilishwa.
Eto’o hakushiriki katika mazoezi ya Inter jana na aliondoka katika uwanja wa klabu hiyo kabla ya siku ya ufunguzi wa msimu wa klabu hiyo haujaanza.
Inter wapo tayari kumuuza Mcameroon huyo mwenye miaka 30 na inasemekana tayari wamekubali ada ya uhamisho ya €35million kwa ajili ya Eto’o, ambaye anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka 4 wenye thamani ya €80million na Anzhi Makhachkala.
Eto’o alijiunga na Inter akitokea Barcelona mwaka 2009 na aliisaidia Milan kushinda makombe matatu katika msimu huo.

No comments:
Post a Comment