Search This Blog

Friday, August 12, 2011

BENNY McCATHY AWASHA MOTO ORLANDO PIRATES


Benny McCarthy aanza kazi Orlando Pirates.

Mshambuliaji mpya wa mabingwa wa soka nchini Afrika Kusini Orlando Pirates Benny McCarthy ameanza vyema maisha yake ya soka kwenye klabu yake mpya baada ya kufunga kwenye mchezo wake wa kwanza wa ligi ya PSL dhidi ya Black Leopards .

McCarthy alifunga bao hilo akiwa ameingia kwenye kipindi cha pili ambapo ilimchukua dakika nane tu kufungua akaunti yake ya mabao kwa klabu yake mpya .

Orlando ilishinda kwa mabao 2-0 huku bao lingine likiwekwa wavuni na mshambuliaji mwingine wa Pirates Bongani Ndulula aliyefunga mapema kwenye dakika ya 10 ya mchezo

No comments:

Post a Comment