Search This Blog

Saturday, August 13, 2011

ARSENAL: TEVEZ KWA NASRI

Arsenal jana usiku wameiambia Manchester City:Tupeni Carlos Tevez na nyie mchukueni Samir Nasri.

Carlos Tevez amekuwa akijaribu kwa muda sasa kutaka kuondoka Manchester ndani ya kipindi hiki chote cha usajili, na kocha wa Arsenal akiwa kwenye pressure ya kununua top players, sasa ameamua ghafla kuja proposal hiyo ya kushtua.

Kiungo Samir Nasrialikuwa na matumainiya kusainiwa na Man City jana mchana baada ya kuhadiwa dili la mshahara wa £180,000 per week, lakini Arsene Wenger akiwa katika hatua za mwisho za kuondokea na nahodha wake Cesc Fabregas aliuzuia uhamisho wa Nasri huku akipeleka proposal ya kubadilishana na Tevez.

Gunners wanaamini wakimtoa Nasri itawagharimu kiasi cha kuongezea cha £10m ili kumpata Muargentina Tevez ambaye timu yake ya City amemuekea gharama ya usajili kuwa £50m.

No comments:

Post a Comment