Search This Blog

Thursday, August 4, 2011

Amini usiamini ‘MISUMARI’ kwenye mchezo wa soka ipo!

Hizi ni malighafi zinatumika kutengenezea dawa...

suala la misumari limehalalishwa na viongozi wa soka hapa nchini..hayo ni maneno ya mganga maarufu hapa jijini Dar es Salaam kwa kuucheza mchezo nje ya uwanja, amejitambulisha kwa jina la sheikh Omary Alhad amefunguka na kulielezea suala hili kwa kina.
Sheikh Omary emezicheza mechi nyingi sana na amezifanyia kazi karibia timu zote za Dar Es Salaam.
Kila msimu huwa na timu moja ambayo husafiri nayo kila mahala iendako kucheza mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara au Visiwani.
Akafunguka kwa kusema yeye ni shabiki wa kutupwa kabisa wa klabu ya Yanga, na akasema kuwa suala la yeye kuwa shabiki wa Yanga halimzuii kuifanyia kazi timu pinzani.
‘’huwa naumia sana roho pindi napoishuhudia Yanga inafungwa tena na timu niliyoifanyia kazi ‘’.
Mechi ambayo hawezi kuisahau miongoni mwa mechi zote alizowahi kuzicheza ni mechi baina ya timu moja kutoka mkoani Mbeya ambayo imeshuka mwaka mmoja au miwili iliyopita dhidi ya timu moja ambayo HAIPENDI kabisa kutoka Dar es salaam,mechi hiyo ilikuwa ngumu kwasababu timu iyo ya Dar kila mara ilipoenda Mbeya ilikuwa ikichezea vichapo,mazingira ya utendaji yalikuwa magumu kwasababu kila upande ulifanya maandalizi kabambe,mechi hiyo ilimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.



Sheikh Omary Alhad akifanya mahojiano na Issa Maeda




Sheikh omary anasisitiza huwa hapendi kushirikiana na mtu pindi anapokuwa kazini,Kila mtu ana kanuni zake za utendaji, mimi kanuni yangu nataka nikiwa napiga ‘misumari’ niwe peke yangu sipendi kuchanganya utendaji wangu na wengine, nikichanganya mkono na mtu huwa sipati mafanikio nakumbuka miaka minne iliyopita timu moja kutoka kisiwani Pemba iliyopanda kwa kasi sana ila kwasasa imepotea, watu wa michezo mtaikumbuka na pemba inasifika kwa mambo haya, nilipelekwa kisiwani pemba niisaidie timu hiyo kupanda daraja kitu tulichogombana ni hicho cha kuchanganya madawa.
Kwani viongozi wa timu hiyo walitaka nishirikiane na wataalam kutoka Pemba kitendo ambacho binafsi sikuwa tayari.
ITAENDELEA….
Sikiliza pia Sports Xtra ya CLOUDS FM kila siku kuanzia saa tatu kamili usiku ili umsikie Sheikh Omary Alhad akiizungumzia ‘misumali’ michezoni.
NB
Misumari ni neno maarufu kwenye mchezo wa soka hapa nchini Tanzania likimaanisha KUROGANA.

No comments:

Post a Comment