Search This Blog

Tuesday, July 19, 2011

NEYMER: NABAKI SANTOS


Mshambuliaji kinda wa kibrazili anayewindwa na European Giants Neymar Dos Santos amesema ataendelea kuwa mchezaji wa Santos msimu ujao.
Real Madrid, Chelsea, Man City na Barcelona wamekuwa wakipigana vikumbo kuwania saini ya mchezaji wa huyo wa mabingwa wa Libertadores Santos, anayetajwa kuwa thamani ya £40million.
Neymar ambaye alikuwa katika kikosi cha Brazil kilichoshiriki michuano ya Copa America inayoendelea nchini Argentina amesema anataka kuendelea kubaki Santos na kuitumikia klabu hiyo katika michuano ya klabu bingwa ya dunia itayofanyika mwezi wa 12.
"Nabaki Santos", Neymar aliwambia waandishi wa habari.
Neymar kwa sasa bado ana mkataba na Santos mpaka 2015

No comments:

Post a Comment