Search This Blog

Wednesday, July 20, 2011

CORINTHIANS WAJITOA KWENYE USAJILI WA TEVEZ


Jana usiku Corinthians walijitoa katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Kiargentina anayeichezea klabu ya Manchester City Carlos Tevez.
Klabu hiyo ya Brazil ambayo last week walitoa ofa ya £40million na wakaikataa kabla ya juzi kocha wa City Roberto Mancini kusema kuwa wapo tayari kuikubali ofa ya wakatoliki hao, lakini kutokana na dirisha la usajili nchini Brazil kufungwa leo dili hilo limeshindikana.
Taarifa rasmi ya klabu hiyo ilisema: "Bodi ya michezo ya Corinthians imeamua rasmi kutangaza kutokuwezekana kumsaini mshambuliaji Carlos Tevez.Tunatambua juhudi zilizofanywa na Manchester City na watu wote waliohusika na mazungumzo, muda zaidi unahitajika ili kuweza kukamilisha usajili lakini kutokana na dirisha la usajili kutoka nje ya nchi kufungwa Jumatano July 20.
Tunafahamu ndoto walizokuwa nazo mashabiki za kumuona mchezaji huyu akiwa hapa kwa mara nyingine, na sasa tunaangalia mbele huku tukiwa matumaini ya Carlos kuwa nasi katika siku chache mbeleni."



No comments:

Post a Comment