Search This Blog

Friday, June 24, 2011

WAKENYA WAZIDI KUTIKISA USAJILI WA ULAYA


Baada ya juzi mdogo wa Mcdonald Mariga kuripotiwa kuzivutia klabu za Celtic na Aston Villa, sasa ni zamu mkenya mwingine Eric Odhiambo ametingisha soko la uhamisho nchini Scotland.

Odhiambo ambaye msimu uliopita alimaliza mkataba wake na klabu ya Inverness amekuwa akifuatilia na klabu kadhaa nchini baada ya kumalizika kwa ligi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa wakala wa mshambuliaji huyo aliyejiunga na Inverness mwezi January 2009, alifunga mabao 4 katika michezo 18 ya msimu uliopita likiwemo goli la kusawazisha alilofunga dhidi ya Glasgow Rangers, anasema mchezaji huyo wa zamani Leicester amezivutiwa klabu kadhaa nchini Scotland zikiwemo timu kubwa.

"Nafahamu kuna klabu nyingi zinamtaka Eric, kuna timu moja tayari wameshatuma ofa lakini Eric anasubiri kuona kama kuna timu nyingine zitaleta ofa halafu ataangalia ipi bora ya kuichukua."-alisema wakala wa mchezaji huyo Clive Hart.


No comments:

Post a Comment